Dar: Wakazi wa eneo la Kunduchi Mtongani ambao nyumba zao zimepitiwa na ujiuji wa volcano ya tope, watakiwa kuhama

Ondoa bango la uongo hili. Mjiolojia ameshatoa ufafanuzi kuwa hiyo sio volkano, wewe unatunga yako kuwatia hofu wananzengo!! Vipi wewe!!??
 
Ondoa bango la uongo hili. Mjiolojia ameshatoa ufafanuzi kuwa hiyo sio volkano, wewe unatunga yako kuwatia hofu wananzengo!! Vipi wewe!!??
Pale wamekuja wataalamu watatu kwa nyakati tofauti.

Lile ni tope Pascal Mayalla amefafanua vizuri!
 
Wataalam Jiolojia wamegota na wanaanza kutoa maelezo yasiyo na kina juu ya tope la Kunduchi. Hawatoi chanzo chake wala kulielezea tatizo kwa kina.

Litazame eneo lote la Kunduchi kama ambavyo mimi nitalielezea.

Barabara ya Bagamoyo ndio iko juu zaidi katika eneo lote la Kunduchi na hii ni kwa sababu, kuli na kushoto maeneo yote yalichimbwa kokoto na kubaki mashimo. Ukielekea Bagamoyo, kushoto kwako karibia nusu kilometa kuna ziwa la msimu linalotunza maji mengi sana. Kulia kwa barabara ya Bagamoyo, limevamiwa na ujenzi holela na sasa ni makazi ya watu.

Yale maji ya kushoto mwa barabara HAYANA mahali pa kutokea, na sasa kwa miaka mingi yanaingia ardhini. Muelekeo wa maji hayo ni baharini.

Sasa tushishangae kuona maji hayo yakiibukia Kunduchi, pamoja na kubeba udongo wa chini ya ardhi. Tukumbuke kuwa eneo la KKKT Kanisani na maeneo ya karibu, ni ardhi oevu miaka yote. Na sasa eneo limeongezewa mkondo uliofumuka kutokana na dimbwi linalotoka kushoto mwa barabara ya Bagamoyo.

Kwa kifupi hayo ndio maelezo ya kisayansi, mtu unaweza kuyapinga kisayansi vile vile.

UTATUZI WAKE: Kwa sasa hakuna!
 
Simple tu tatzo Ni hayo machimbo.

Watu wa geologist enzi izo walikataza kuchimba,watu wakaendelea kuchimba mawe/kokoto mpaka na kuletewa polisi Ila bado walikua wabishi.

Ghafla miaka ya 2007 kwenda mbele watu wakaanza ujenzi wa makazi.Sijui nani alibariki kujengwa Hilo eneo,Sasa hivi Ni nyumba zimetapakaa sanaaaaaaa
 
mkuu 2003 ilitokea hadi ndege ziliungua, ila haikuwa deadly kama hiyo unayosema ya Italy ambayo sijawahi kuisikia kabla ngoja nikatafute huko youtube najua wenzetu lazima wali record

Mji wa kale wa Pompeii nchini Italy ulijengwa jimboni Naples - mlipuko mkubwa wa Valcano ya mlima Vesuvius ulitokea tarehe 24 October,79AD (yaani, miaka 79 baada ya Yesu kuzaliwa) walikufa wengi lakini wengine walinusurika kwa kukimbilia sehemu salama - mwanzo nilisema walikufa wote hiyo si sahihi, nafikiri sikumsikiliza vizuri mwalimu wangu wa Historia wakati nikiwa form two miaka mingi sana iliyo pita, niliachana na somo la Historian miaka iliyo fuata nikaingia mkondo wa sayansi.
 
Hii taarifa niliona juzi kwenye taarifa ya habari ya ITV, ni kweli kabisa uji uji unatokea ardhini, na kuna dogo alijaribu kukanyaga hizo tope akazama kidogo, halafu mwezake akampiga kofi la tako.
 
Hili tatizo bado mimi sijaona mtaalamu husika. Hao wote walioonekana kwenye eneo la tukio ni Geolodists. Hili tatizo linahitaji mtu mtaalamu wa Geophysics au Seimology. Nashauri Dr. Isaac Marobhe (mstaafu kutoka Idara ya Jiolojia, UDSM) pamoja na Dr. R. F. Wambura (Seimologist, Idara ya Jiolojia, UDSM) wapewe fursa nyingine ya kufika kwenye eneo la tukio na washirikishwe katika kutoa ushauri wa kitaalamu. Hao ndiyo wataalamu hasa wa mambo haya. Hata hao geologist nao pia ni wataalamu lakini utaalamu wao hauko hasa kwenye eneo hili. Wenye utaalamu kwenye eneo hili ni hao niliowataja
 
Dah! Ni wewe kweli umeandika huu ujinga!??
 
Kwa Mara ya kwanza sikupingi hoja yako.
 
Mkuu sidhani kama upo sahihi (unaweza nisahihisha)...

Kwenye sheria za ardhi za kimataifa, ardhi ni mali ya serikali na hata kukiwa na uwepo wa natural resources, hilo eneo linachukuliwa na serikali.

Kama kuna mkazi au wakazi basi wanapewa ardhi sehemu nyingine.
 
Wakikuta bangi ndio utajua ardhi Ni ya nani
 

Hapana, hiyo ni kweye Communism, lkn Capitalistic system unamiliki ardhi unayoinunua na mtu hawezi kuja kuichukua, kuhusu kilicho chini ya ardhi unayoimiliki inategemea na Sheria za nchi husika wengi husema labda hii ardhi ni mali yako na urefu wa mita kadhaa chini ni mali yako, baada ya hizo mita siyo yako hivyo kama madini au rasilimali yoyote ikipatikana ndani ya mita zako kwenda chini ni mali yako.

Nchi za Kikapitalisti Serikali haiwezi tu kusema kama vile Tanzania kwamba tutawapatia viwanja sehemu nyingine, hivyo viwanja Serikali inavitoa wapi ? Capitalistic system hakuna mahali pasipo na mwenyewe hata kama ni msitu una mmiliki hivyo kama serikali inataka ,,kuwagawia ''watu viwanja ni aidha iwanunulie na kuwapa au Serikali ichukue maeneo ya Hifadhi labda ambapo pia kuna sheria zake.

Tofauti kubwa kati ya Capitalistic system na Communism, ni kwamba Capitalistic system unamiliki ardhi ni mali yako kama umenunua una hati ni mali yako, wakati communism kama Tanzania ardhi siyo mali yako unaikodisha kwa miaka kadhaa, ...
 



Volkano za matope ni miundo ya uso iliyoundwa na mlipuko wa matope kutoka kwa uso mdogo. mifano ya kawaida. mlipuko wa kawaida ni mchanga mzuri wa mchanga, maji, na gesi, CO2 na methane. Vipande vya mwamba wa nchi pia wakati mwingine huingia ndani. Zinatoka saizi kutoka <1 m, kawaida ya volkano za matope zilizoundwa na kuyeyuka kwa kina kirefu, hadi kwenye majengo ambayo ni ya urefu wa mita mia chache au hupanuka baadaye kwa zaidi ya kilomita 1. Milipuko mikubwa huleta matope kwa uso kutoka kwa kina kinachozidi zaidi ya kilomita 1 .Katika sura hii tunazingatia milipuko mikubwa; Milipuko midogo inayotokana na uso mdogo kabisa ni dhihirisho la kimiminika cha 'jadi'.
 
Ile tulisoma kwenye geography shuleni wanaita mudflow sio hii. Maana hilo tope halifanani na la volcano na sioni uwepo wa chanzo cha volcano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…