Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
Option ni kurudisha tu hizo nyumba, mimi nina nyumba ya kuishi ila nilivutiwa kuchukuwa moja kule kwenye mradi wa Pspf wa Buyuni Chanika, nyumba niliyochukuwa ni category three ya million 74 kwa miaka 15.Kabla hujarukia sababu zako, jaribu kufika eneo la tukio kupata ukweli.
Kuna tatizo kubwa sana kwenye hii NSSF tangu enzi za Dau kuhhsu zile nyumba pale.
Ukweli ni kwamba, wale wamepangishwa kwa kodi inayozidi Tshs milion 1 kwa mwezi na wanapaswa kuilipa NSSF milioni tatu kila baada ya miezi mitatu, ikifika kuanzia milioni 120 na kuendelea ndo unapewa nyumba yako.
Nyumba yenyewe hata kwa Tshs 300,000 kwa mwezi haipangishiki labda kwa bei ya juu ya Tshs 200,000 kwa mwezi.
Nimejaribu kukuelezea uhalisia ambao Bodi ya NSSF inajutahidi kuuficha kwa gharama kubwa na kuidanganya mamlaka ya juu nchini.
Nilitowa deposit ya million 5 nikamuweka mtu akae baada ya mwaka mmoja ndio vikaanza kuja vikokotoo na nilivyopiga hesabu kwa miaka 15 maana yake unawalipa million 100 na kitu, na hapo ndio wakafosi kila mwezi tulipe laki sita au zaidi, kumbuka kipindi hicho tayari Magufuli ameshaharibu uchumi wa nchi tukapewa demand note na dalali wao nikaona isiwe tabu nikarudisha na aliyeiomba kuingia tukafanya makubaliano akanilipa gharama zangu za grill nikairudisha nyumba niliona hapa natafuta stress bure.
Ila taarifa nilizonazo bei ya hizo nyumba zimeshushwa baada ya Jenister Mhagama kufanya vikao vingi na wakazi, tatizo kubwa la miradi ya nyumba ni ya kifisadi na kuover rate, ukiwa na kiwanja chako million 40 unajenga nyumba ya kisasa kabisa.
Kingine hizo nyumba kabla ya watu kuingia hawawapi elimu ya kutosha maana wengi kwa ufahamu wangu naona kipengele cha kulipa kila mwezi hawakijui wameaminishwa deni lilipwe ndani ya miaka ya mkataba na si lazima kila mwezi utowe pesa, shida iko hapo kwa kipato cha Mtanzania wa kawaida aachane na hizi nyumba za miradi hazipo kwa ajiri ya kusaidia Watanzania ni za upigaji tu kwenye vitengo vya investment, hao National housing wenye jukumu lao ndio mafisadi namba moja wapangaji wao wa mijini sasa hivi wanauza flat zao wanachukuwa upangaji watu wapya wenye msuli wa kulipa kodi mpya za NHC.