Dar: Walemavu waliobomolea vibanda vya biashara waomba hifadhi UNHCR

Wametumwa na waajiri wao.
 
Matajiri wanaharibu sana taswira na sifa ya nchi ya Tanzania kwa kuendekeza ubaguzi kwa baadhi ya makundi yasilyo na kipato cha kueleweka wakiwemo walemavu, wamachinga, mama lishe, bodaboda, na mafundi wasio na mitaji ya kutosha.

Je, ni halali wananchi kuomba ukimbizi wa kijamii kwenye shirika la kimataifa huko nchi ikijinasibu imefungua milango ya kujipatia kipato wakifukuzwa huku na kule kama waharifu kwa kisingizio wanachafua mazingira wakati kila binadamu aliyehai hutembea na uchafu mwilini?
 
KUNA VITU TUNAVIENDEKEZA TU KUNA MSEMO WAZUNGU WANASEMA DISABILITY NOT INABILITY

PIA SIDHANI KAMA KUTUMIA ULEMAVU KUJIDAI WANATETEA UMACHINGA KUKAA SEHEMU ISIYO SAHIHI NI SAWA
 
Duhh. Kesho wataongezeka na siajabu ombaomba wooote watakusanyika kwenye hizi ofisi. Labda washindwe kutambua eneo zilipo. Ila itambulike kwamba kuna watu wanapongeza na wengine wanajiuliza hivi polisi wanashindwaje kuwakamata kwa kututia aibu kama hii. Hili nalo lina taswira yake miongoni mwetu kama watanzania.
 
Hao wametumwa. Ulemavu ndio utandike bidhaa barabarani? Je akikongwa na kupoteza maisha? Jamani hili suala la kupanga bidhaa mabarabarani lazima ipingwe kwa njia zote.
 
maneno ya bango lao:
"......mheshimiwa makamu wa...."
Kwani chifu Hangaya huko angani anakoshinda hawezi kuwasikia kupitia kwa wawakilishi wake?
 
Kwa hiyo wanataka waishi bila kufuata sheria au? Kama waliweza kutoka huko walikotoka na kufika mjini wanaweza kurudi walikotoka na sina maana ya kuwabeza. Najuwa mahitaji yao tofauti lakini walifikishaje bidhaa zao mjini kwanza? Hakuna mtu aliyefukuzwa ni kwamba waende maeneo yaliyopangwa inatosha ile ya bajaji kupewa ruhusa kuingia mjini na wako wakajifanya walemavu na magongo kuingia mjini. miji lazima sheria zifuatwe hakuna exception.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…