Dar: Walemavu Wamkataa Waziri Bashungwa, wataka atengue tamko la bajaji na bodaboda kufanya kazi mjini kati

Dar: Walemavu Wamkataa Waziri Bashungwa, wataka atengue tamko la bajaji na bodaboda kufanya kazi mjini kati

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
WALEMAVU, BODABODA WAANDAMANA WAKITAKA WAZIRI BASHUNGWA KUTENGUA TAMKO LAKE*.

Kufuatia katazo wa Waziri wa TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa kuhusu sakata la bodaboda na bajaji kuingia mjini, Walemavu na Bodaboda wameandamana mpaka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam wakishinikiza Waziri Kutengua tamko alilotoa.

Hatua ya Walemavu na Bodaboda kuandamana imekuja Kufuatia Tamko la Waziri Bashungwa kukinzana na Makubaliano ya pamoja na utaratibu mzuri uliokuwa umewekwa tangu mwanzo baina ya Waendesha Bajaji Wenye ulemavu na Waendesha bodaboda.

Miongoni mwa Makubaliano hayo ni pamoja na Bajaji za watu Wenye ulemavu kuruhusuwa kuingia katikati ya mji na kuegesha kwenye Vituo vitatu walivyopangiwa, Bajaji za wasio na ulemavu kutoruhusiwa kuingia katikati ya mji, Bodaboda zilizosajiliwa na kukidhi vigezo kuruhusuwa kuegesha kwenye Vituo Saba katikati ya mji na Bodaboda zisizokuwa na Vibali kuruhusiwa kuingia mjini Kwa kigezo Cha kushusha abiria na kugeuza.

Katika jitiada za kutuliza maandamano hayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amelazimika kufanya mawasiliano ya simu na Waziri Bashungwa na kumuelezea Hali halisi ya maandamano hayo na madai ya waandamanaji kushinikiza kutumika kwa utaratibu waliokuwa wamejiwekea awali ambapo Baada ya kuridhika na utaratibu mzuri uliokuwa umewekwa, Waziri Bashungwa ameridhia kuendelea kwa utaratibu uliokuwa ukitumika awali wa Pikipiki na Bajaji kuingia Katikati ya mji Kwa mujibu wa makubaliano na maridhiano ya pamoja yaliyokuwa yamewekwa baina ya Waendesha Bajaji Wenye ulemavu na waendesha bodaboda.

Uamuzi huo umepokelewa kwa mikono miwili na Wandamanaji hao ambao wameahidi kuendesha Shughuli zao pasipokuvunja makubaliano na utaratibu wa pamoja waliokuwa wamejiwekea awali kwakuwa umehusisha na *kukidhi matakwa ya pande zote.

Pia soma > Kanusho: Bodaboda na Bajaji hawajapigwa marufuku kuingia katikati ya Jiji kuanzia Alhamisi 21 Aprili, 2022


1.jpg
2.jpg
3.jpg
 
Wabongo taratibu tunaanza kujitambua sio kila tamko la serikali ni lakufuatwa na raia
 
CHAWAAAAAA....mnaitwa huku kumsifia Mama kwa kuupiga mwingi kuwepo democracy ya kuandamana [emoji851]
 
Enzi zile hapo ni viboko na mabomu ya machovu...
 
Back
Top Bottom