Dar: Wanafunzi 19,000 waliojiunga Kidato cha Kwanza, wakosa Madarasa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, ameeleza kuwa mkoa wa Dar una upungufu wa Madarasa 381 huku Temeke pekee kukiwa na Upungufu wa Madarasa 120 kwani watoto waliofaulu kuingia kidato cha kwanza kwa Mwaka 2020 wapo 5,970 kwa Wilaya ya Temeke pekee. Vilevile tunajenga Shule Mpya nne kwaajili ya Wanafunzi hawa waliofaulu

Ameyaeleza hayo hii leo Jumanne Januari 21, 2020 Wakati akipokea msaada wa ndoo 500 za rangi kutoka kiwanda cha rangi cha Billion Paints kama msaada wake kwa Serikali ili kukamilisha ujenzi wa Madarasa hayo huku akihimiza wadau wengine kujitokeza.

"Kutokana na tatizo hilo Mkoa uliona katika kulishughulikia suala hilo ni vema tukajumuisha Mkoa mzima ili kutekeleza maelekezo ya Wizara ya Elimu ya darasa moja wanafunzi 50". Hizi rangi si ndogo, katika ujenzi huu zitatusaidia kupiga hatua na tunawahakikishia katika shule ambapo rangi hizi zitafika, darasa moja tutachora jina la kiwanda ili wanafunzi wajue kuna watu waliwachangia,” amesema.

Katika Ujenzi huu ambao unatakiwa Ukamilike 28 February 2020, hakuna mzazi atakaye changishwa chochote. Na lengo ni kuhakikisha Tarehe moja Machi 2020 wanafunzi wote wawe Wanayatumia madarasa haya.
 
Hivi ni kwamba tunakosa projection au vipi , inakuaje Kama mnajua idadi ya watahiniwa kwa mwaka mnaijua na mnakuwa mnajua probability ya watoto kiasi gani watafaulu mitihani Yao ... Iweje wakose madarasa.

Kwasababu idadi ya watahiniwa ulionao ndio inakupa picha ya Kama madarasa yatatosha au la hata kabla hawajafanya mtihani ... Sasa inapokuja watoto wamefaulu na wanakosa vyumba vya madarasa ina maana kazi ya wahusika ni kuwafanya wanafunzi wafaulu tu na sio kufanya projection ya vyumba vitakavyowachukua wanafunzi ??


Ngozi nyeusi kama ni hivi Basi tuna matatizo ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…