Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Dar es salaam, 12, Oktoba, 2021
KUKAMATWA KWA WATU WATATU KWA TUHUMA ZA MAUJAJI YA MTENDAJI WA SERIKALI YA MTAA.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya afisa mtemtendaji wa Serikali ya mtaa wa Mbezi Msumi aliyefahamika kwa jina la Kelvin Costa Mowo (38), Mkazi wa Bunju, Afisa mtendaji wa Msumi.
Majina ya watuhumiwa hao yanahifadhiwa kwa saababu za kiupelelezi.
Tukio hili limetokea tarehe 11/10/2021 saa 11:54 asubuhi huko eneo la Msumi Mbezi wilaya ya Ubungo katika ofisi za Serikali ya mtaa, ambapo marehemu akiwa ofisini kwake anaskiliza mgogoro wa ardhi.
Ghafla watu wapatao wanne waliingia ofisini na mmoja wao akatoa panga na kumshambulia mtendaji huyo kitendo kilichopelekea kupata majeraha makubwa na baadae akapoteza maisha wakati akikimbizwa hospitalini, watu watatu wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo wanahojiwa kwa kina na watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.
MULIRO J. MULIRO- ACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM, DAR ES SALAAM