Dar: Watu wawili mbaroni kwa mauaji ya Barke Rashid. Wivu wa mapenzi wadaiwa kuwa chanzo

Wewe habari za yeye kutolewa figo umezipata/ umezitoa wapi?

Chief hapo kabla kulikuwa na audio clip ikielezea hilo tukio kabla na ndio watu wengi walipojua juu ya kifo cha binti huyo...

Hii video imekuja ku clear hizo rumours, (hii video umeweka ndio naiona sasa)
 
Watu hawajifunzi kabisa. Ni nadra kuua mtu halafu ukabahatika usijulikane na kukamatwa. Utashikwa tu hata kwenye nchi maskini mifumo ya ya Sheria ni dhaifu.

Ila alipangiwa atakufa hivyo pindi tu alipozaliwa kwa iyo ni kuomba na wewe usipangiwe kutekeleza mauaji mtu mwengine alipangiwa pindi tu alipozaliwa.
 
Mbaya zaidi ni kuona wakongwe wakizirudia hizo habari za figo kunyofolewa!

JF imeshuka sana viwango aisee!

Ndugu wa marehemu wamehojiwa na vyombo vya habari. Ndugu hao ndiyo walioukagua mwili wa marehemu. Wao hawajaona chochote kinachoashiria alinyofolewa figo.

Halafu bado wapo wanaodai alinyofolewa figo.

WTF!!
 
Chief hapo kabla kulikuwa na audio clip ikielezea hilo tukio kabla na ndio watu wengi walipojua juu ya kifo cha binti huyo...

Hii video imekuja ku clear hizo rumours, (hii video umeweka ndio naiona sasa)
Hiyo audio clip ilikuwa na sauti ya nani? Any idea?
 
dah 🤦🏿‍♂️🙆🏿‍♂️Ukatili wa kusikitisha wapate adhabu kali iwe fundisho kwa wengine
 
Hiyo audio clip ilikuwa na sauti ya nani? Any idea?

Hakujitambulisha...ilikuwa tu ni mwanamke kwa sauti anaonekana ni wa makamo anatoa tahadhari kwa mabinti kwamba wawe makini, maana kuna mwenzao (ambaye ndio huyu marehemu) kauawa na kutolewa figo...

Hata hapa JF habari ya kutolewa figo ipo..


 
Kweli katiba mpya ni muhimu ili ije na suluhisho la ajira kwa vijana, yani mil 1.7 saba unalipwa kuua mtu!!!? Jamani huyo ni mtu au mbwa kuchaa?
Wanaume, ni rahisi sana kutambua kuwa mwanamke ulienae hakupendi ila pesa yako kwanini umgharimikie? Nyie wanawake wenye tamaa za fisi kama humpendi mtu kwanini umkubalie? Siukatae tu ili uwe huru na maisha yako?
 
Mwamba alicheatiwa sana lakini hakuzoea.
Bora kujua tabia za mwanamke kwanza kuliko kushobokea uzuri.
 
I see!

Ulichokiwekea maneno mekundu na kilichopo kwenye video ni tofauti kabisa.

Nakiamini zaidi kilichopo kwenye video.
 
Ni kweli either ukongwe wao unafanya wasiwe na wasiwasi sababu anakuwa anahisi ni Ile JF ya zamani ambayo tulikuwa tunaheshimiana na kuleta mada zenye uhalisia na ukweli.

Anyway ndio vizazi tunaoviachia nchi yetu 🤷
 
Duh hatari sana, jamaa adai kabisa hela yake iliyobaki kabla ya hukumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…