Dar: Watu wawili mbaroni kwa mauaji ya Barke Rashid. Wivu wa mapenzi wadaiwa kuwa chanzo

Dar: Watu wawili mbaroni kwa mauaji ya Barke Rashid. Wivu wa mapenzi wadaiwa kuwa chanzo

Wewe habari za yeye kutolewa figo umezipata/ umezitoa wapi?

Chief hapo kabla kulikuwa na audio clip ikielezea hilo tukio kabla na ndio watu wengi walipojua juu ya kifo cha binti huyo...

Hii video imekuja ku clear hizo rumours, (hii video umeweka ndio naiona sasa)
 
Watu hawajifunzi kabisa. Ni nadra kuua mtu halafu ukabahatika usijulikane na kukamatwa. Utashikwa tu hata kwenye nchi maskini mifumo ya ya Sheria ni dhaifu.

Ila alipangiwa atakufa hivyo pindi tu alipozaliwa kwa iyo ni kuomba na wewe usipangiwe kutekeleza mauaji mtu mwengine alipangiwa pindi tu alipozaliwa.
 
Nimeshangaa sana kusikia habari ya kuhusu huyo binti kutolewa Figo maana toka jana ndugu zake walioenda kuutambua mwili walisema hakuna sehemu aliyoonyesha ametobolewa ikiashiria kwamba labda wamechukua hiyo Figo.

JF kuna watoto wamekuja kuibuka wanaleta Habari za udaku wanakera sana kwakweli.

JF imekuwa ya waswahili nadhani moderators hawako serious habari Kama hii ipelekwe jukwaa la mizaha huko au wafungue jukwaa la uswazi.

Siku hizi tunashindwa kupata habari au taarifa zenye kuwa na mantiki zaidi ya vijana kuja na udaku na hawajui hata kujadili zaidi ya kurusha lugha zisizofaa humu jukwaani.

Zamani ilikuwa mtu Kama huyu anayeleta Habari za uongo namna hii alikuwa anakula ban kwa kuleta taharuki namna hii.
Mbaya zaidi ni kuona wakongwe wakizirudia hizo habari za figo kunyofolewa!

JF imeshuka sana viwango aisee!

Ndugu wa marehemu wamehojiwa na vyombo vya habari. Ndugu hao ndiyo walioukagua mwili wa marehemu. Wao hawajaona chochote kinachoashiria alinyofolewa figo.

Halafu bado wapo wanaodai alinyofolewa figo.

WTF!!
 
Chief hapo kabla kulikuwa na audio clip ikielezea hilo tukio kabla na ndio watu wengi walipojua juu ya kifo cha binti huyo...

Hii video imekuja ku clear hizo rumours, (hii video umeweka ndio naiona sasa)
Hiyo audio clip ilikuwa na sauti ya nani? Any idea?
 
dah 🤦🏿‍♂️🙆🏿‍♂️Ukatili wa kusikitisha wapate adhabu kali iwe fundisho kwa wengine
 
Hiyo audio clip ilikuwa na sauti ya nani? Any idea?

Hakujitambulisha...ilikuwa tu ni mwanamke kwa sauti anaonekana ni wa makamo anatoa tahadhari kwa mabinti kwamba wawe makini, maana kuna mwenzao (ambaye ndio huyu marehemu) kauawa na kutolewa figo...

Hata hapa JF habari ya kutolewa figo ipo..

Kwenye kumtafuta wakaenda hospitali zote kufika Amana wakaambiwa "Bwana, hapa ililetwa maiti ya mwanamke tarehe 1, baada ya kukaa sana imechukiliwa imepelekwa Muhimbili" ndugu walivyoenda Muhimbili wakautambua mwili wa Barke na walipomchunguza wakakura ametolewa figo.
 
Kweli katiba mpya ni muhimu ili ije na suluhisho la ajira kwa vijana, yani mil 1.7 saba unalipwa kuua mtu!!!? Jamani huyo ni mtu au mbwa kuchaa?
Wanaume, ni rahisi sana kutambua kuwa mwanamke ulienae hakupendi ila pesa yako kwanini umgharimikie? Nyie wanawake wenye tamaa za fisi kama humpendi mtu kwanini umkubalie? Siukatae tu ili uwe huru na maisha yako?
 
Mwamba alicheatiwa sana lakini hakuzoea.
Bora kujua tabia za mwanamke kwanza kuliko kushobokea uzuri.
 
Hakujitambulisha...ilikuwa tu ni mwanamke kwa sauti anaonekana ni wa makamo anatoa tahadhari kwa mabinti kwamba wawe makini, maana kuna mwenzao (ambaye ndio huyu marehemu) kauawa na kutolewa figo...

Hata hapa JF habari ya kutolewa figo ipo..

I see!

Ulichokiwekea maneno mekundu na kilichopo kwenye video ni tofauti kabisa.

Nakiamini zaidi kilichopo kwenye video.
 
Mbaya zaidi ni kuona wakongwe wakizirudia hizo habari za figo kunyofolewa!

JF imeshuka sana viwango aisee!

Ndugu wa marehemu wamehojiwa na vyombo vya habari. Ndugu hao ndiyo walioukagua mwili wa marehemu. Wao hawajaona chochote kinachoashiria alinyofolewa figo.

Halafu bado wapo wanaodai alinyofolewa figo.

WTF!!
Ni kweli either ukongwe wao unafanya wasiwe na wasiwasi sababu anakuwa anahisi ni Ile JF ya zamani ambayo tulikuwa tunaheshimiana na kuleta mada zenye uhalisia na ukweli.

Anyway ndio vizazi tunaoviachia nchi yetu 🤷
 
Duh hatari sana, jamaa adai kabisa hela yake iliyobaki kabla ya hukumu
 
Back
Top Bottom