Dar: Watu wawili mbaroni kwa mauaji ya Barke Rashid. Wivu wa mapenzi wadaiwa kuwa chanzo

Dar: Watu wawili mbaroni kwa mauaji ya Barke Rashid. Wivu wa mapenzi wadaiwa kuwa chanzo

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawashikilia Watu wawili wanaodaiwa kula njama na baadaye kumuua Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Barke Pesa Rashid (30) mkazi wa Ilala Utete Jijini Dar es salaam kisa madai ya kwamba Mwanamke huyo aligharamiwa na Mwanaume hadi kumpangishia nyumba lakini akawa na Wanaume wengine.

"Tukio hilo limetokea January Mosi,2022 Tabata Segerea kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo Maridadi ambako tarehe hiyo Mtuhumiwa wa kwanza Mwanaume, Jonsiner Bounser( 34), Mkazi wa Segerea Kalabash Pub alifanya mipango ya mapenzi na Mwanamke aliyemuua baada ya kula njama na Mtuhumiwa mwingine wa pili aliyekamatwa Mwanaume anayeitwa White (33) Mfanyabiashara ya Lori la kuzolea taka Mkazi wa Tabata Segerea"

"Mwanamke huyo alikabwa shingo mpaka kupoteza maisha akiwa katika nyumba hiyo ya kulala wageni, Bounser alikodiwa na White kwa malipo ya Tsh.Milioni 1.7 ili amtongoze na baadaye aende kumuua Mwanamke huyo kwa madai kuwa White alimgharamia sana na kumpangishia nyumba lakini Mwanamke huyo ana Wanaume wengine"

"Bounser amekiri kupewa Tsh. Milioni 1.2 kwa nyakati tofauti kabla na baada ya kutekeleza mauaji hayo na kwamba alikuwa bado anadai Tsh. Laki tano kwa White kwa mauaji ya Mwanamke huyo, uchunguzi wa tukio hilo unakamilishwa na watafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo" ——— Jumanne Muliro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam
 
Kuna habari Ililetea humu kwamba kuna Mwanamke aliuwawa tarehe 1.1.2022 maeneo ya Tabata Segerea na kutolewa figo.

Jeshi la polisi limewakamata watuhumiwa 2 waliokiri kuhusika na mauaji hayo.

Chanzo cha kifo ni wivu wa mapenzi ambapo mtuhumiwa namba 1 aitwae White ambae ni mpenzi wa marehemu alimkodi mtuhumiwa wa 2 Bw. Jonsiner Bounser (John Cena Baunsa) kwenda kumtongoza Marehemu na kisha kwenda kulala nae na kumuua kwa maelezo kwamba mtuhumiwa wa kwanza white amekua akimtuhumu Marehemu kua na wanaume wengine na sio muaminifu na yeye White amemgharamia sana ila marehemu haridhiki.

Hivyo White akakodi mtu amtongoze mpenzi wake na kisha amuue kwa malipo ya shilingi milioni 1.7 na hadi mauaji yanafanyika mtuhumiwa namba 2 alikua ameshalipwa kiasi cha 1.2m na bado anadai 500k kwa mtuhumiwa namba 1.

Mauaji ya mapenzi yameshika kasi sana.
This makes more sense…..I mean hiyo habari ya gazeti la Mwananchi.
 
I see!

Ulichokiwekea maneno mekundu na kilichopo kwenye video ni tofauti kabisa.

Nakiamini zaidi kilichopo kwenye video.

Upo sahihi...

Utofauti ni kuwa wengi wetu tulikuwa na taarifa ya awali, ambayo hadi wakati huo hakuna aliyekanusha...(tar 18 na 19 Jan)

Hii ambayo ndugu wanaonekana wanahojiwa imekuja baadaye, wengine hatujapata fursa ya kuiona...(tar 21 Jan)

Anyway kila kitu kipo wazi sasa...bila shaka marehemu na ndugu zake wataona haki ikichukua mkondo wake
 
Nimeshangaa sana kusikia habari ya kuhusu huyo binti kutolewa Figo maana toka jana ndugu zake walioenda kuutambua mwili walisema hakuna sehemu aliyoonyesha ametobolewa ikiashiria kwamba labda wamechukua hiyo Figo.

JF kuna watoto wamekuja kuibuka wanaleta Habari za udaku wanakera sana kwakweli.

JF imekuwa ya waswahili nadhani moderators hawako serious habari Kama hii ipelekwe jukwaa la mizaha huko au wafungue jukwaa la uswazi.

Siku hizi tunashindwa kupata habari au taarifa zenye kuwa na mantiki zaidi ya vijana kuja na udaku na hawajui hata kujadili zaidi ya kurusha lugha zisizofaa humu jukwaani.

Zamani ilikuwa mtu Kama huyu anayeleta Habari za uongo namna hii alikuwa anakula ban kwa kuleta taharuki namna hii.
Niliwaambia hakuna siku Jerry Banks ataleta taarifa ya ukweli humu JF. Miaka yote threads zake ni uongo tu. Ile thread watu tulivyohoji namna gani mtu anatolewa figo kienyeji tukaonekana wapuuzi tu. Humu JF wajinga ni wengi, taarifa yoyote hawachuji ndio maana matapeli hawakosi. A critical thinker asingeamini ule uzushi
 
Kumpangishia chumba tu alafu akamkacha ndo unamuuwa mwenzie,je'angetoa figo kama yule mwamba ingekuwaje!
 
Msitufanye wajinga, hapo kilichokuwa kinalengwa ni hiyo FIGO tu. Hayo mengine ni porojo za kusherehesha hadithi tu. Nilisema toka mwanzo, kwamba Figo ukiitoa bila utaalam ni useless, hivyo lazima surgeon mtaalam alikuwepo kuitoa kitalaam, which haiwezekani kwa guest house, hivyo baada ya mauaji na huo mwili kupelekwa mortuary, huko ndiko walipoitoa kitaalam.
Ushahidi wako kuwa hiyo figo ilitolewa spitali uko wapi? Au unamwaga hisia zako tu hapa?
 
Ni huzuni mno🥺🥺
Binadamu haaminiki tena.
Ni bora kujua huyu ni simba unaweza kukaa nae mbali kuliko kuwa karibu na kiumbe binadamu ambae moyo wake umejaa vichaka 🥺🥺
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawashikilia Watu wawili wanaodaiwa kula njama na baadaye kumuua Mwanamke mmoja
Mkuu mbona tunatoa hukumu before being proven Guilty ?
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawashikilia Watu wawili wanaodaiwa kula njama na baadaye kumuua Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Barke Pesa Rashid (30) mkazi wa Ilala Utete Jijini Dar es salaam kisa madai ya kwamba Mwanamke huyo aligharamiwa na Mwanaume hadi kumpangishia nyumba lakini akawa na Wanaume wengine.

"Tukio hilo limetokea January Mosi,2022 Tabata Segerea kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo Maridadi ambako tarehe hiyo Mtuhumiwa wa kwanza Mwanaume, Jonsiner Bounser ( 34), Mkazi wa Segerea Kalabash Pub alifanya mipango ya mapenzi na Mwanamke aliyemuua baada ya kula njama na Mtuhumiwa mwingine wa pili aliyekamatwa Mwanaume anayeitwa White (33) Mfanyabiashara ya Lori la kuzolea taka Mkazi wa Tabata Segerea"

"Mwanamke huyo alikabwa shingo mpaka kupoteza maisha akiwa katika nyumba hiyo ya kulala wageni, Bounser alikodiwa na White kwa malipo ya Tsh.Milioni 1.7 ili amtongoze na baadaye aende kumuua Mwanamke huyo kwa madai kuwa White alimgharamia sana na kumpangishia nyumba lakini Mwanamke huyo ana Wanaume wengine"

"Bounser amekiri kupewa Tsh. Milioni 1.2 kwa nyakati tofauti kabla na baada ya kutekeleza mauaji hayo na kwamba alikuwa bado anadai Tsh. Laki tano kwa White kwa mauaji ya Mwanamke huyo, uchunguzi wa tukio hilo unakamilishwa na watafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo" ——— Jumanne Muliro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam
Polisi hawana akili, Johnsiner Bounser ni jina official kweli?
 
Back
Top Bottom