Dar: Watuhumiwa 17 wakamatwa wakitaka kuwafanyia Mtihani Wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria

Dar: Watuhumiwa 17 wakamatwa wakitaka kuwafanyia Mtihani Wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Prof. Elifas Bisanda ameliomba Jeshi la polisi kuwafikisha Mahakamani haraka iwezekenavyo watuhumiwa 17 waliokamatwa wakijaribu kuwafanyia mtihani wanafunzi mbalimbali chuoni hapo.

Prof. Bisanda ameyasema hayo Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari akizungumzia kukamatwa kwa watuhumiwa hao.

Profesa Bisanda amesema chuo kipo tayari kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ikiwemo vielelezo.

Video: Azam TV
Degree na masters fake za kibongo.
 
Most ya wanaofanyiwaga mitihani huwa ni wale wanafunzi ambao wapo kazini/kwenye ajira.

Anachokuwa anakitaka yeye ni cheti chake cha degree tu au master yake au diploma yake ili apeleke ofisini asubirie barua yake ya kupandishwa cheo.

Na victim wa hii issue ni wanafunzi ambao hawana kazi wenzang na mie umetoka zako home una buku tu ya nauli na bado una usongo ule wa kusoma/ ujohn kisomo ukipewa kali 3 unaona bonge la hela unajitoa muhanga
Duuuh hii sasa kaliii, Poler yao hao wahusikaa. Wawatajee waliowapa kazi hiyo. Sheria ipite nao woteee.
 
sio Mitihani tu hata practical za sayansi wanaenda kufanyiana unakuta mhusika yupo zake bukoba lakini anamtuma mtu aliye karibu DSM
 
Wamechomeshana!!! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hela inatafutwa kwa namna yoyote ile, hivi hao wanaofanyiwaga mitihani huwa wao hawana uwezo? Sasa chuo wanafanya nn? Khaaah
Hii ni hatari sana, mtu anatamani aitwe msomi, kumbe box
 
Hii ni hatari sana, mtu anatamani aitwe msomi, kumbe box
Nashangaa hapo, ndo maana utendaji ni hafifu huko makazini kumbe wahusika hawana uelewa wala ufahamu wa kazi husika.

Hii nchi aliyeiroga kafa, na alikotupia ndumba hapaonekani. Lol
 
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Prof. Elifas Bisanda ameliomba Jeshi la polisi kuwafikisha Mahakamani haraka iwezekenavyo watuhumiwa 17 waliokamatwa wakijaribu kuwafanyia mtihani wanafunzi mbalimbali chuoni hapo.

Prof. Bisanda ameyasema hayo Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari akizungumzia kukamatwa kwa watuhumiwa hao.

Profesa Bisanda amesema chuo kipo tayari kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ikiwemo vielelezo.

Video: Azam TV

Ndo maana tunawasomi ambao wapo empty kichwani.....
 
Tuacheni utani tuwe wa kweli maana tunakuwa huru kweny nafsi zetu .

Ishu za watu wanasoma kutokea kazi yaani wanajiendeleza huku wanafanyakazi ni mwiba tena utapeli mkubwa sana , unakuta mtu yupo ofisini mpaka jioni kila siku unamuona ila unakuja kusikia eti anagraduate Masters .

Tuacheni unafiki elimu ni rahisi sana haswa nchi zetu hizi ukiwa na pesa hizi masters na Phd unaokota tu , ni bora watu wapewe mda wa kwenda kusoma kama walimu ila wafanyakazi wa Taasisi ni mwiba mkubwa kuzorotesha elimu kwa kuendekeza uwizi ili wapate ufaulu .

Chuo HURIA wanjifunze zaidi kama wamekamata 17 basi 80% ya wanafunzi wa hapo haswa MASTERS wanafanyiwa mitihani ..Msters za mchongo ni nyingi sana kwa kweli .
 
Wamechomeshana!!! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hela inatafutwa kwa namna yoyote ile, hivi hao wanaofanyiwaga mitihani huwa wao hawana uwezo? Sasa chuo wanafanya nn? Khaaah
Wanakuwa
 
Back
Top Bottom