Dar: Watumishi wa TALGWU wafikishwa Mahakamani kwa ufujaji wa Tsh. Milioni 114.4

Dar: Watumishi wa TALGWU wafikishwa Mahakamani kwa ufujaji wa Tsh. Milioni 114.4

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Watumishi hao ni Jackson M. Ngalama ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa TALGWU SUPPORT LTD, Emmanuel G. Mdoe, Mhasibu Mkuu na Timothy P. Mashishanga, Dereva wa Kujitegemea wote wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu katika Mahakama ya Wilaya Ilala.

Wote kwa pamoja wameshtakiwa kwa makosa ya Matumizi Mabaya ya Madaraka, Kutumia Nyaraka kwa lengo la Kumdanganya Mwajiri, Ubadhirifu na Ufujaji wa Tsh. 114, 457,100 mali ya Chama cha Kusaidiana chini ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mtaa (TALGWU SUPPORT LTD).

Baada ya kusomewa Mashtaka, Washtakiwa wamekana kuhusika na kupelekwa Mahabusu kutokana na kushindwa kukidhi masharti ya Dhamana. Kesi imeahirishwa hadi Septemba 18, 2023 itakaporejea kwaajili ya kusoma Hoja za Awali.

===========

VIGOGO WAWILI TALGWU NA DEREVA WASHTAKIWA KWA RUSHWA - ILALA:

Shauri la Uhujumu Uchumi Na. 17/2023 - Jamhuri dhidi ya: -

1. Jackson Moses Ngalama - Mkurugenzi Mtendaji wa TALGWU SUPPORT LTD;
2. Emmanuel Gilbert Mdoe - Mhasibu Mkuu wa TALGWU SUPPORT LTD na
3. Timothy Peter Mashishanga - Dereva wa kujitegemea, limefunguliwa Septemba 12, 2023 mbele ya Mhe. Nestory Baro - Hakimu Mkazi Mkuu katika Mahakama ya Wilaya Ilala.

Washtakiwa wameshtakiwa kwa makosa yakiwemo; Matumizi mabaya ya madaraka; Kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri; Ubadhirifu pamoja na Ufujaji wa kiasi cha shilingi 114, 457,100 mali ya Chama cha Kusaidiana chini ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mtaa (TALGWU SUPPORT LTD), makosa ambayo ni kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329.

Washtakiwa wamekana Mashtaka na kupelekwa mahabusu baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama.

Kesi hii imeahirishwa hadi Septemba 18, 2023 kwa ajili ya kusoma Hoja za Awali.
 
Haya majina kwa ufisadiiii, elmu dunia
😂😂😂😂😂😂😂🤣🤣🤣🤣🤣
 
Haya majina kwa ufisadiiii, elmu dunia
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Kuna wenzako wamekamatwa india wakisafirisha madawa ya kulevya.
 
Back
Top Bottom