Dar: Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amsimamisha kazi kaimu Mkurugenzi wa DAWASA, Shaban Mkwanywe kwasababu ya uzembe kazini

Dar: Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amsimamisha kazi kaimu Mkurugenzi wa DAWASA, Shaban Mkwanywe kwasababu ya uzembe kazini

Jamaa wana ujinga sana...maji yapo, umeme upo, madawa ya kutibu maji yapo. ILA SASA: Maji Dar es salaam hayapatikanaji, yakitoka machafu. Huyo ilitakiwa atumbuliwe na acharazwe viboko 12 right on the spot. Hafu mbona kama alikuwa kanywa wanzuki!
 
Kuna mahali vingunguti Bomba limepasuka huu mwaka wa pili hakuna kilichofanywa.
Yanatoka TU.
Je, hapo ni kosa la serikali?
Pale ni kuweka joint tu mchezo umeisha.
Kuna mahali keko maji yalivunja kwa zaidi ya miaka 3 na kila siku watumishi wa DAWASA wanapita hapo kwenda na kutokea kazini.
Hawa watumishi na mabosi wao ni washenzi.
Kama unabisha nitafute nikuonyeshe linkages zinazotoa maji kwa zaidi ya miaka 2 hapa Dar. Ziko nyingi
 
Hakuna Logic ya kumfuta kazi mkurugenzi suala la ukosefu wa maji nchi hii ni suala la kufeli Kwa serikali iliyopo madarakani, pamoja na waziri wake
Lini umesikia Marekani waziri wa maji amemfuta kazi Mkurugenzi, haya mambo ni hayo hayo mambo ya aweso anajua Mkurugenzi sio mtu wake na amemzidi mshahara hivyo anamtafutia zengwe Ili aweke mtu wake, kama alivyoweka Mkurugenzi wa muwasa Moshi asiye na vigezo taratibu za vyeo zinataka Mkurugenzi awe na masters ya mambo hayo ya maji na degree juu, ila tunaendelea kuvunia katiba . Tunajua hata huyo mtu wako utakayemuweka matatizo hayataisha, kwasababu haya ni matatizo ya serikali, hivyo uonevu ni kawaida ya wanasiasa.

Nchini hii Ina matatizo makubwa ya kiutawala yaliyochangiwa na umaskini wa nchi hii pia.
Kuna utofauti gani kati ya ulichokiita 'masters na degree ya juu'?
 
Pole Sena mkuu naona ndugu Yako kibarua kimeota nyasi Sasa hasira unamalizia Kwa waziri tulishasema uchawa unamwisho haya jiandae kutafuta kazi ya kufanya hata kuuza genge
 
Ungejua jinsi mambo yanavyokuwa magumu katika utendaji kwakuwa serikali kuu Haina msaada, hii tengua teua Haina faida yoyote kwasababu si kiini Cha tatizo. Ni sawa na wewe tukuambie ukalime jangwani lazma ufeli ndo nchi yetu.
Mwambieni baba yenu kwamba kazi za kuteuliwa sio za moja kwa moja, akipigwa chini asiendekeze majungu, atafute kazi nyingine, kazi iendelee. Mnadhani angekaa hapo maisha yake yote..?
 
Sio ndugu yangu Wala simjui, ila nimeona Kwa habari, nachukia uonevu , unadeal na watu badala ya kudeal na tatizo. Niliona Kwa Millard Ayo hii habari
Huwezi kuchukia kutumbuliwa kwa mtu mzembe ambaye anakubali kufanya kazi sehemu ambayo ni mji mkubwa kama Dsm na maji yanashindwa kutoka na yeye comfortably yupo tu ofisini. Huo utakuwa upumbavu, atulie benchi aone wenzake kazi watakayofanya.
 
Ungejua jinsi mambo yanavyokuwa magumu katika utendaji kwakuwa serikali kuu Haina msaada, hii tengua teua Haina faida yoyote kwasababu si kiini Cha tatizo. Ni sawa na wewe tukuambie ukalime jangwani lazma ufeli ndo nchi yetu.
Sasa wewe na masters yako umeshindwa kufanya ubunifu wananchi wapate maji, umekaa ofisini unapiga mshahara wako mrefu.
Urefu wa mshahara wako uendane na huduma nzuri kwa wananchi.
 
Sasa wewe na masters yako umeshindwa kufanya ubunifu wananchi wapate maji, umekaa ofisini unapiga mshahara wako mrefu.
Urefu wa mshahara wako uendane na huduma nzuri kwa wananchi.
Hii nchi tatizo ni serikali iliyopo madarakani
 
AWESO AIPANGUA DAWASA, AIWEKA CHINI YA UANGALIZI MAALUM

View attachment 3030087
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amemtaka Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA), Kiula Kingu akae pembeni kwa muda, pia amemsimamisha kazi, Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji-DAWASA, Shaban Mkwanywe na kuanzia leo June 30,2024 ameiweka DAWASA chini ya uangalizi Wizara ili kuboresha utendaji wake kufuatia uzembe uliopelekea visima kukosa maji na kufanya Wakazi wa Dar es salaam kukosa maji.

Aweso ametangaza uamuzi huo leo baada ya kufanya ziara ya kimkakati na ya kushtukiza katika Ofisi za DAWASA zilizopo Ubungo Dar es salaam ili kupata maelezo ya Watendaji ya sababu za Watu kukosa maji na baada ya kushindwa kuridhishwa na majibu aliamua kuzungukia matanki ya maji katika maeneo manne tofauti ikiwemo la Ardhi UDSM na Kibamba huku akituma Timu nyingine kwenda kukagua matanki ya Kigamboni ambapo matanki hayana maji huku mengine yakiwa na maji kidogo ukilinganisha na mahitaji ya Wananchi huku Watendaji wa DAWASA wakishindwa kueleza sababu iliyopelekea uhaba huo wa maji.

Aweso amesema “Mwanzoni kulipokuwa kunakosekana maji tulikuwa tunasema shida ni vyanzo vya maji vimekauka hakuna maji, TANESCO umeme hamna lakini leo vyanzo vyote vina maji, umeme upo, niambieni kwanini hatuna maji kwenye matenki?, kwanini Wananchi wanateseka, wanalalamika wanapiga kelele kwenye Serikali?”

Ziara ya Aweso leo imekuja baada ya ziara ya Katibu Mkuu wa Maji aliyoifanya kwa siku mbili kujionea utendaji kazi wa DAWASA na hali ya upatikanaji wa maji ambapo amebaini uzembe aliouwasilisha kwa Waziri Aweso leo ikiwemo miundombinu ya maji kuwa chakavu, maji kupotea bila usimamizi, Watendaji wa DAWASA wa ngazi za chini kutopewa stahiki zao muhimu na kupelekea kufanya kazi bila hamasa nzuri na hata kupelekea kuwajibu vibaya Wateja, ziara hiyo ya Aweso na Katibu Mkuu itaendelea katika maeneo mbalimbali ya Nchi ili kuboresha upatikanaji wa maji.

Pia soma;

1. KERO - Wakazi wa Tegeta Azania (Kwenye Nyaya za Umeme wa Zanzibar) hatuna Maji kwa Muda Sasa, DAWASA shida ni nini?

2. KERO - DAWASA mna nini na wakazi wa Mbezi Beach? Hatuna maji siku ya 3 sasa

3. KERO - DAWASA mnazingua, mimi si wa kuamka usiku kukinga maji ya mvua ya matumizi ya nyumbani

4. KERO - Waziri Juma Aweso atoke hadharani na kusema kwanini Ubungo mpaka Kimara maji ni shida

5. KERO - Waziri Aweso, Jiji la Dar Sasa wanakunywa na kuoga maji ya kwenye mifereji. DAWASA pakavu

6. KERO - Kinyerezi kuna shida kubwa ya maji, group la DAWASA WhatsApp halifanyi chochote kutatua kero hii

7. KERO - Maji Malamba Mawili ni mgao mkali, baadhi ya Wakazi walio kwenye miinuko wana miezi hawapati maji kutokana na kasi ndogo ya maji. DAWASA wafafanua

8. DAWASA kwanini mvua ni nyingi lakini tunakosa maji?

9. KERO - DAWASA kuna rushwa kwenye ufungaji wa maji

10. KERO - DAWASA maji ya makazi mapya Mbezi Beach yana udongo mwezi sasa, nini shida?

11. KERO - Maji ya DAWASA yana harufu na ladha ya Dawa kali sana, ni salama kweli?

12. Mnyika: DAWASA mnataka tufanye maandamano ya Maji DSM ndio mtoe majibu?

13. Hivi DAWASA haina msimamiz?

14. Dar: Maeneo ya Segerea hadi Kinyerezi hakuna Maji

15. DOKEZO - Tabata Bonyokwa hatujaona tone la maji wiki ya tano sasa, DAWASA mnatuona manyani?

16. DOKEZO - DAWASA, Segerea kuna mgao wa maji kimyakimya? Wiki ya pili mitaani hakuna maji!

17. ACT Wazalendo: Kutofanyiwa kazi matatizo ya upatikanaji wa maji safi Dar es Salaam; Tunamtaka Waziri wa Maji kuiwajibisha DAWASA
Na imesaidia sana, tatizo la maji jijini limebaki historia!
 
Back
Top Bottom