Dar yakusanya Tsh. Trilioni 13 kati ya 16.5 zilizokusanywa na TRA. Ni aibu kwa Tanzania kutegemea 80% ya Mapato kutoka Mkoa mmoja

Dar yakusanya Tsh. Trilioni 13 kati ya 16.5 zilizokusanywa na TRA. Ni aibu kwa Tanzania kutegemea 80% ya Mapato kutoka Mkoa mmoja

Tunaomba takwimu za mikoa mingne pia tuone n wapi pa kwenda kutaftia riziki mbali na dar...hatuezi kujirundika dar wote kisa kuna mzunguko wa pesa, uo ni ujinga. Hii mada n ngumu sana
 
Dar Es Salaam ndo Tanzania, ni Jiji muhimu Kwa Uchumi wa nchi
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema Mkoa wa Dar es Salaam ni wa kipekee katika ukusanyaji wa mapato nchini.

Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda alisema hayo Dar es Salaam juzi usiku wakati wa hafla ya kuwapa tuzo walipa kodi bora wa mikoa ya kikodi ya Dar es Salaam kwa mwaka 2023/2024.

Mwenda alisema Dar es Salaam ni mkoa wa kipekee kwa kuwa kuna mikoa mitano ya kikodi: Ilala, Temeke, Kinondoni, Tegeta na Kariakoo. “Licha ya kuwa na mikoa mitano ipo Idara ya Forodha na ina mikoa mitatu mikubwa, kuna Kituo cha Huduma Maalumu, Kituo cha Kukusanya Kodi za Mafuta na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambako tunakusanya kodi,” alisema.

Mwenda alisema sababu hizo na nyinginezo ziliwezesha TRA ikusanye Sh trilioni 16.5 kuanzia Julai hadi Desemba mwaka 2024 na kati ya fedha hizo trilioni 13 zilikusanywa katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Habari Leo

===

MY TAKE

Kitendo cha Nchi kutegemea asilimia 80% ya Mapato Kwa Mkoa mmja wa Dar ni jambo la ajabu na la kushangaza na inaonesha jinsi Nchi Ina uneven distribution of resources. Pia soma Miaka Zaidi ya 60 Baada ya Uhuru,Tanzania Imeshindwa Kuondoa Mizizi ya Ukoloni Kwa Nchi kuwa tegemezi wa Uchumi na Mapato Kwa Jiji Moja tuu la Dar

Hatuwezi kuendelea na utaratibu huu,ni muda muafaka sasa Kwa Serikali kutawanya maendeleo na economic centres kwenye Kila Kanda.

Kwamba Mikoa 25 inakusanya Trilioni 3.5 yaani hata nusu ya Mapato ya Dar hayafiki harafu Walioko kwenye Utawala wanaona sawa Dependency ya hivi Kwa Mkoa mmja Haina Afya kiuchumi na ni hatari sana kiusalama.

Hivi tuna watu wa Mipango kweli? Hivyo Vyuo vyenu vya Planning mnafundisha nini Sasa? Mambo kama haya ndio yanafanya watu waamini mtu mweusi hajatimia kichwani.

Ngoja ije itokee Dar kuwa paralysed siku Moja Kwa tukio.loloye ndipo akili zitawajia maana Mtu mweusi Huwa hajifunzi na hana akili za kesho Hadi apigwe tukio.

Soma hapa zaidi Mikoa 13 Kinara wa Kuchangia Kodi ya TRA mwaka 2023
 
alafu mikoani ambayo ina makada wengi na wanachama wanaobubujikwa na machozi kwa ccm ndio wavivu kupindukia,kuna haja ya CCM kutoa mitaji na elimu ya ujasiriamali kwa wanachama wake.
 
alafu mikoani ambayo ina makada wengi na wanachama wanaobubujikwa na machozi kwa ccm ndio wavivu kupindukia,kuna haja ya CCM kutoa mitaji na elimu ya ujasiriamali kwa wanachama wake.
Has nothing to do with uvivu,kwani wewe wa hapo Dar imefanya efforts ipi ya kujenga viwanja, Bandari nk?
 
Dar ndio sehemu pekee ambayo Ina Bahari na Bandari pekee? Kwa nini Bandari zingine zisiwe developed?

Harafu GDP sio hela na Wala haileti au.kuingiza hela.

Dar ikiwa paralysed hata kama mnazalisha huko ila mlango wa kuizia au.ku exports uko Dar Haina maana.
Uchumi umesoma wapi ...ulipata supp eeh?? GDP sio hela ni kitu gani
 
Hata USA pamoja na utajiri wao mkubwa GDP yao almost 35% inatoka California, Texas na NY states zingine 47 wanachangia 65% tu ni kawaida na sababu zipo kwanini.
Acha uongo
 
Kwani hayo matrioni ya pesa huwa yanaenda wapi ? C.A.G. kila mwaka ana baini madudu na upotevu wa hizo pesa. je,serikali huwa inawafanya nini hao waliotafuna hizo trioni? mnataka mikoa mingine iongeze mapato ili ziende kwenye matumbo ya wachache? bora hali iendelee kuwa hivi hivi.
 
Acha uongo
With last December's release of GDP numbers by the Bureau of Economic Analysis (BEA), the top five states – which contribute 41% of the total U.S. GDP in 2022 – were California, Texas, New York, Florida, and Illinois, in that order. Figure 1 shows the real GDP for these states in trillions of dollars. Size matters

Sijui kama utaelewa ila acha uvizu soma sio kukurupuka tu, ikiwa states 5 tu zinachangia 41% hiyo 59% gawa kwa states 45 au hesabu ngumu tukusaidie.
 
Sasa mada ni GDP au mapato ya kodi ...maana alicholeta mtoa uzi ni mapato ya kodi sio GDP ...sio ajabu kwa nchi kuwa na GDP kubwa kwenye eneo moja kuliko mengine ila ni ajabu kwa nchi kuwa na collection ya mapato kubwa eneo moja kuliko mikoa mingine
 
Tunategemea Dsm iboreshwe zaidi kuendana na uchumi wake, hasa Miundombinu yake hasa road etc, ili isaidie kukuza uzalishaji zaidi!
 
Uchumi umesoma wapi ...ulipata supp eeh?? GDP sio hela ni kitu gani
Jinga kweli,kama GDP ni hela Mwanza ingekuwa namba 2 Kwa kuchangia pesa nyingi ,badala yake inazidiwa Hadi na Songwe 😁😁
 
Back
Top Bottom