Dar: Yanga walala mabao 3-2 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya

Mavindozii

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2012
Posts
2,111
Reaction score
2,781
Hello GT.
Mwenye kujua matokeo ya hii MECHI please let's me know .Niko Kijijini ,
Nadhani hii timu yangu itafanya vizuri Leo wakuu ,

======

Kikosi cha Yanga dhidi ya Gor Mahia FC kuelekea mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika

1. Youthe Rostand
2. Juma Abdul
3. Gadiel Michael
4. Andrewa Vincent
5. Abdalah Shaibu
6. Papy Tshishimbi
7. Yusuph Mhilu
8. Raphael Daudi
9. Matheo Antony
10. Pius Buswita
11. Deus Kaseke

Kikosi cha akiba

12. Benno Kakolanya
13. Haji Mwinyi
14. Said Juma
15. Said Mussa
16. Emmanuel Martin
17. Juma Mahadhi
18. Ibrahim Ajibu

Kikosi cha Gor Mahia FC dhidi ya Yanga kuelekea mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika

1. Boniface Olouch
2. Philemon Otieno
3. Godfrey Walusimbi
4. Joash Onyango
5. Haroun Shakava
6. Humphrey Mieno
7. Samuel Onyango
8. Francis Kahata
9. Jacques Tuyisenge
10. Kelvin Omondi
11. George Odhiambo

Kikosi cha akiba

12. Shaban Odhoji
13. Charles Momanyi
14. Cercidy Okey
15. Boniface Omondi
17. Benard Ondiek
18. Ephrem Gulkan
19. Lawrence Juma

Dakika 90 za mchezo kati ya Yanga na Gor Mahia zimemalizika Uwanja wa Taifa Dar es salaam,Gor Mahia 3 Yanga 2.Mchezo wa Kundi D kombe la shirikisho Afrika

Baada ya USM Alger kutoka sare ya kufungana 1-1 na Rayon Sports, Yanga hana nafasi tena ya kufuzu robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika anasubiri kucheza game mbili za kukamilisha ratiba

Habari zaidi.....

WINGA Deus Kaseke aliyerejeshwa Jangwani akitokea Singida United usiku huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam alifungua akaunti yake ya mabao kwa kuifungia timu hiyo bao la kufitia machozi wakati wakilala mabao 3-2 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

Yanga ilikumbana na kipigo hicho cha pili mfululizo mbele ya K'Ogalo katika mechi za Kombe la Shirikisho Afrika na kuzidi kupoteza matumaini ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo kutokea Kundi D linaloongozwa na USM Alger ya Algeria.

Kaseke alifunga bao hilo dakika ya 60 akiwahi mpira wa kichwa cha Pius Buswita uliotemwa vibaya na kipa Boniface Oluoch, likiwa bao la kwanza tangu ajiunge na Yanga akitokea Singida iliyomsajili kwenye msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara.

Katika pambano hilo, Yanga walishtukizwa na bao la mapema la sekunde 38 lililowekwa kimiani na George Odhiambo 'Blackberry' baada ya mabeki wa Yanga na kipa Youthe Rostanda kufanya uzembe kuokoa krosi ya Samuel Onyango.

Rostand ambaye amekuwa kilalamikiwa na mashabiki wa kushindwa kuwa makini langoni, aliupangulia nyavuni mpira wa kichwa cha Odhiambo kabla ya kufanya makosa tena na kuruhusu bao la pili dakika ya 41 baada ya Jacques Tuyisenge kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Francis Kahata na kutinga wavuni bila kipa huyo kujishughulisha. Adhabu hiyo ilitokana na makosa ya kipa huyo kuurusha mpira kisha kuudaka tena akiwa langoni na mwamuzi Ahmad Imrhaz Heeralali kuamuru adhabu hiyo.

Gor waliandika bao lao la tatu dakika chache baada ya Kaseke kufunga bao la Yanga, baada ya Haruna Shakava kumalizia mpira wa kona uliowapita mabeki wa Yanga kabla ya Raphael Daud kufunga bao la pili la Yanga dakika ya 80.

Bao hilo lilipatikana baada ya Yanga kufanya mabadiliko kwa kumtoa kipa Rostand na kumuingiza Beno Kakolanya, huku mapema Juma Mahadhi aliingia badala ya Yusuf Mhilu na Kaseke kumpisha Ibrahim Ajibu.

Kwa matokeo hayo Yanga imeendelea kubaki mkiani ikiwa na alama moja tu licha ya kucheza mechi nne, huku ikifunga mabao mawili na kufungwa 11.

Chanzo: Mwanaspoti
 
Last edited by a moderator:
Kamusoko Thaban atacheza leo? Mbona first eleven hayupo
 
Kikosi cha Yanga dhidi ya Gor Mahia FC kuelekea mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika
1. Youthe Rostand
2. Juma Abdul
3. Gadiel Michael
4. Andrewa Vincent
5. Abdalah Shaibu
6. Papy Tshishimbi
7. Yusuph Mhilu
8. Raphael Daudi
9. Matheo Antony
10. Pius Buswita
11. Deus Kaseke
Kikosi cha akiba
12. Benno Kakolanya
13. Haji Mwinyi
14. Said Juma
15. Said Mussa
16. Emmanuel Martin
17. Juma Mahadhi
18. Ibrahim Ajibu
 
Hik umetoa wap mkuu kuna wat ciwaon apo
 
Kikos cha ndondo cup hiki
 
Mmh tutapata tabu sanaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…