Daraja la Busisi kupewa jina la Rais Magufuli ili akumbukwe katika Utawala wake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mwanza. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema daraja la Kigongo- Busisi limepewa jina la Rais John Magufuli ili aendelee kukumbukwa milele kutokana kazi kubwa aliyoifanya kwenye utawala wake.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Desemba 18, 2020 alipotembelea na kukagua ujenzi wa daraja hilo ulioanza mwaka 2020 na kutarajiwa kukamilika mwaka 2024.

Daraja hilo lenye urefu wa kilometa 3.2 litakuwa na nguzo 67 na litagharimu Sh699.2 bilioni. Linajengwa na kampuni ya CCECC ya nchini China.

"Limepewa jina lake ili aendelee kukumbukwa milele," amesisitiza Majaliwa.

Amesema ujenzi wa miradi mbalimbali ya kimkakati inayoendelea nchini lengo ni kurahisisha wananchi kufanya shughuli zao za kiuchumi katika mazingira mazuri.

Amewataka watanzania kupuuza kauli za baadhi ya watu kwamba serikali inajali zaidi vitu badala ya kuleta maendeleo ya watu.

"Tupuuze hizi taarifa hizi ni za watu wenye nia ovu, huwezi kupata maendeleo bila kuirahisishia mambo kama haya ya usafiri," amesema
Amesema mbali na kuboresha miundombinu hiyo lakini kupitia miradi hiyo inaongeza ajira kwa watanzania.
 
Ndio...

IMG_20201212_065536.jpg
 
Binafs ingenishangaza endapo isingefikiriwa kuitwa jina lake coz mkuu kafanya mengi yaliyoonekana awali hayawezekaniki.
Mwenye atakuja na resistance ya hilo atakuwa amebeba agenda ya chuki binafc tu
 
Huwa nakereka sana ninapotoka Geita mjini saa 4 asubuhi na kufika Mwanza mjini saa 11 jioni. Yaani sehemu ya masaa yasiyozidi ma2 natumia masaa 7 kisa foleni kusubiria vivuko. Nasema hivi wasiliite John Pombe Magufuli pekee, Bali waongeze na His Excellency Dr. John Pombe Joseph Magufuli Bridge.
 
Tukishamuondoa tutatoa jina stahili. Daraja hata kuisha bado tayari na majina mmeanza kugawiana?
Hii ni kununua mbeleko kabla ya mtoto kuzaliwa.
Mbona tumejawa na kiherehere namna hii?
Halafu Majaliwa namuona kama PM wa kwanza nchi hii tokea tupate Uhuru ambaye badala ya kutimiza majukumu yake yeye anazunguka nchini kumsifia na kumuabudu mteule wake sijui kwa nini?
Jee kuna anayejua historia yake sahihi atuwekee hapa!
 
Kumbe kuna watu huwa wanampigia simu mhe. au kumtumia msg na anazipata?

Japo hajubu kwa wakati wanaotarajia wahusika ila kibonzo chatukumbusha watu kadhaa aliwasamehe na wengine kuwapa nafasi tena kwenye "ufalme wake".

JK msimu wake alikuwa na namba ambayo baadhi ya wananchi walimfukia moja kwa moja. Hata Mungu wa mbinguni huwa kuna nyakati sala zetu anazipata moja kwa moja.

Kama kuna issue imekwama huku kwa Ma-DC, Ma-RC au mawaziri, huyu alie juu kabisa anafikiwaje ili tujenge uchumi wa viwanda jumuishi kwa kutumia rasimali za ndani, tupunguze imports, ikiwezekana tuongeze exports; in the course tunapanua tax base na kuongeza ajira ikiwamo michango kwenye mifuko ya pensheni kupitia waajiriwa ambao watafanya kazi kwenye fursa za uwekezaji.

Wasalaam
 
Lakini ujenzi utachukuwa muda mrefu sana,je huyu mkandarasi ni masikini au malipo ndio shida?
Tunajenga kwa fedha zetu za ndani usihofu.Hii nchi ni tajiri Sana wapinzani wametuchelewesha Sana maadamu tupo wenyewe litakamilika
 
Tukishamuondoa tutatoa jina stahili. Daraja hata kuisha bado tayari na majina mmeanza kugawiana?
Hii ni kununua mbeleko kabla ya mtoto kuzaliwa.
Mbona tumejawa na kiherehere namna hii?
Halafu Majaliwa namuona kama PM wa kwanza nchi hii tokea tupate Uhuru ambaye badala ya kutimiza majukumu yake yeye anazunguka nchini kumsifia na kumuabudu mteule wake sijui kwa nini?
Jee kuna anayejua historia yake sahihi atuwekee hapa!
Unamuondoa wewe na nani?
 
Huwa nakereka sana ninapotoka Geita mjini saa 4 asubuhi na kufika Mwanza mjini saa 11 jioni. Yaani sehemu ya masaa yasiyozidi ma2 natumia masaa 7 kisa foleni kusubiria vivuko. Nasema hivi wasiliite John Pombe Magufuli pekee, Bali waongeze na His Excellency Dr. John Pombe Joseph Magufuli Bridge.

Uongo mbaya! Mkuu anafanya kz zitakazo kumbukwa milele.
 
Binafs ingenishangaza endapo isingefikiriwa kuitwa jina lake coz mkuu kafanya mengi yaliyoonekana awali hayawezekaniki.
Mwenye atakuja na resistance ya hilo atakuwa amebeba agenda ya chuki binafc tu

Tutajenga mnara wa kumbukumbu za watu waliotekwa na kuuwawa kwenye awamu hii, pendekeza jina tuute mnara wa nani?
 
Huwa nakereka sana ninapotoka Geita mjini saa 4 asubuhi na kufika Mwanza mjini saa 11 jioni. Yaani sehemu ya masaa yasiyozidi ma2 natumia masaa 7 kisa foleni kusubiria vivuko. Nasema hivi wasiliite John Pombe Magufuli pekee, Bali waongeze na His Excellency Dr. John Pombe Joseph Magufuli Bridge.
Sasa hao wasukuma watayatamukaje hayo makishelense? Unataka wajiume maulimi?
 
Back
Top Bottom