Mimi sio mwandishi mzuri ila kwa kweli inasikitisha sana nimepita mara kadhaa daraja hili lililopo mkoani Lindi barabara kuu ya Dar-Lindi, linamaliza ndugu zetu wa malori.
Ukitokea Lindi ni km 70, kuna mteremko sio mkali sana ila una kona kidogo, chini ya mteremko huo ndio kuna daraja ambalo liliathiriwa na mvua na hivyo magari kupita kwenye mchepuko. Kwa kipindi chote hicho cha miezi 5 hivi kuna malori kadhaa yamepata ajali mbaya sana.
Kuna alama mbili tu, yaani vibao vidogo vya 30km/hr vilivyochorwa kwa mkono na ambavyo vimewekwa kwa mti mfupi sana kiasi kwamba haviko visible, dereva akishuka na lory ghafla anakutana na mchepuko hivyo hulazimika kutupa gari motni ama sehemu nyingine na hivyo kusababisha ajali.
Mwezi wa sita nilishuhudia ajali kwa macho yangu ambapo lori lilidumbukia mtoni likiwa limebeba sulphur, ni watu wangapi walikunywa maji yenye sulphur? Ni madhara kiasi gani yamepatikana? Hakuna ila pia gari lile lilikua liligonge basi la baraka kwa nyuma na hivyo madhara yake yangekua makubwa zaidi.
Leo tena nimekuta ajali ya lory lingine (la nne hili sasa kama sio la tano) hapo hapo liliwa limeng'oka engine, tairi yaani limekua vipande tupu. Kuna siku atakuja kutumbukia kiongozi huenda ndio tutajenga.
Picha chini ni lorry ambalo ajali yake ingelimaliza Basi la Baraka kwa Nyuma hivyo dereva kuamua kuingia huko majini, hapo liko chini zaidi ya mita 25-30 kutoka juu na hiyo ni sulphur.
Pia soma ~ Serikali yasaini mikataba Ujenzi wa madaraja 13 yaliyoathiriwa na mvua - Lindi, Tsh. Bilioni 140 kutumika