DOKEZO Daraja la Mbwemkuru-Lindi linamaliza malori na watu, Serikali fanyeni jambo

DOKEZO Daraja la Mbwemkuru-Lindi linamaliza malori na watu, Serikali fanyeni jambo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Juzi kati nimemkuta jamaa alijiachia na Vw yake akapiga shimo zake mbili,, rimu tatu zikapinda,
Nikawa namuonea tu huruma, rimu tatu halafu gari ya kijerumani anapata wapi nangurukuru, ailikuwa na very long breakdown porini.
Hahahahhaaha ,mimi saa nane usiku nilikutana na jamaaa ako na prado TX na yeye kapiga shimo zake kadhaa hapo kapasua tairi mbili, ana wheel spana mbovu, hana kile chuma cha kufungulia tairi chini kule, hana spare tairi. nikamsaidia kufungua nikamuacha
 
Kujenga daraja mbali sana, mbwemkuru panataka kuwa well posted ili madereva wachukue tahadhari kabla hawajafika kwenye diversion.
Hili ndio kubwa na muhimu kwa sasa
 
Duh nakumbuka mara ya mwisho kupita huko kama 2013 njia ilikuwa tamu hio na haina magari kabisa.
Kipindi hicho ulichopita barabara ilikuwa bado mpya hasa kipande cha kutoka nyamwage (rufiji) mpaka somanga (kilwa), siku hizi malori yamekuwa mengi sana , dangote na yale yanayobeba makaa ya mawe
 
Mdau uko vizuri,unaona changamoto za wananchi na kupaza sauti,lakini serikali sikivu imeshindwa kutatua changamoto,sasa gari la DODOMA JIJI FC limepata ajari hapo.
 
Back
Top Bottom