Daraja la mto Mara (Serengeti NP) liangaliwe upya!

Daraja la mto Mara (Serengeti NP) liangaliwe upya!

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Kuna daraja lenye urefu wa kama meta 50 hivi ambalo limejengwa ndani yamaji (yaani wamemimina maji yapite juu). Huo mto Mara ni mkubwa sana ambapo ndio watalii hufurika kuona Nyumbu wakivuka (crossing). Changamoto ya daraja ni kuwa , maji yakiongezeka kidogo, daraja huwa halionekani na hivyo kuvuka hapo ni Kwenda kwa bahati nasibu.

Ajali kadhaa zimekuwa zikitokea hapo na hata wiki iliyopita gari la wageni (watalii) lilianguka hapo bahati nzuri watalii walitoka salama

Utatuzi wake;
Kuweka nguzo kwenye kingo za daraja kila urefu wa kama meta 8hivi ili madereva waone kingo za daraja na pengine ziwekwe mark mahala ambapo maji yakifika sio salama kwa gari kupita

Mara nyingine napata wasiwasi na hawa wakandarasi wetu kwani daraja limekarabatiwa hivi karibuni japo tatizo KUBWA KABISA ambalo niweka alama za kuonesha Kingo za daraja wakati maji yameongezeka halikufanyiwa kazi!
 
Kogatende near rangers post?
Daraja lipo karibu kabisa na uwanja wa ndege wa Kogatende (sio ranger post)

Lipo daraja moja tu refu na ni maarifu sana kwani hakuna namna nyingine ya kupita ng'ambo ya mto kwenda upande wa pili bila kupita hapo
 
Back
Top Bottom