Daraja limekatika, Mto umejaa maji kuvuka ng'ambo ya Kanaani-Dereva anageuza kuelekea Misri

Daraja limekatika, Mto umejaa maji kuvuka ng'ambo ya Kanaani-Dereva anageuza kuelekea Misri

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2020
Posts
3,443
Reaction score
4,006
Wana Jukwaa nguli,

Gari limeshindwa kuvuka mto kwenda kanaani baada ya daraja kukatika kwa maji ya mvua iliyonyesha ghafla. Dereva anageuza gari kurejea Misri ambako uhuru na starehe zote zipo. Abiria ndani ya gari wanahoji tunaenda wapi? Dereva na konda wanajibu si mmedai mtakula wapi, nawapeleka mahali salama penye kila kitu na mfuko wenu tu.

Baada ya kukaribia ufukwe wa bahari mfu, baadhi ya abiria wanashuka na kuanza kupiga kelele ambazo hazikusikilizwa.

Baada ya gari kuwasili ufukweni mwa bahari mfu dereva anashuka kwanza akiwa amebeba mfano wa fimbo nyeusi ya mpingo na kuyagusa maji akitarajia yatagawanyika apite kurejea Misri, lakini cha ajabu fimbo inaonesha kama bua la mhindi mkavu, inakatika bila kuyashitua maji anasubiri kupewa upenyo avuke bila mafanikio. Abiria walifanya nini baada ya tukio hilo?

Abiria walivishwa barakoa na kuandaliwa kupata chanjo ili kuzimua mizimu lakini kuwazuia wasinene chochote mpaka watakapofanikiwa kupewa kibali cha kuvuka. Kila mmoja anaanza kutoa laana za kila aina kuanzia wazazi hadi walezi-mwisho wake ni upi?
 
Dereva huyu mjinga sana, bahati mbaya abiria hatuna sauti. Afadhali hata yule dereva mwingine japokuwa kila mtu ana kasoro zake
 
Kama barabara imemshinda bc asaidiwe na yule trafiki jina linaanzia na M
 
Kama barabara imemshinda bc asaidiwe na yule trafiki jina linaanzia na M
 
Team shetani mnapata shida sana.
Mlidhani mama atashindwa sasa mmeanza kulia lia
 
Mliozaliwa miaka ya 90 sio jukwaa lenu hili kaeni pembeni
 
Back
Top Bottom