SI KWELI Daraja limeporomoka na kuua watu 30 huko California

SI KWELI Daraja limeporomoka na kuua watu 30 huko California

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Hii hapa video wakuu



1755764877602.png
 
Tunachokijua
Madai

Mtumiaji mmoja wa mtandao wa Instagram alichapisha kipande cha video kikionesha daraja linaporomoka na baadhi ya magari yakiwayanaanguka. Video hiyo imeambatanishwa na ujumbe unaoeleza kuwa daraja limeporomoka Calfonia na watu 30 wamejeruhiwa.

Uhalisia wa taarifa hiyo

JamiiCheck imefuatilia Taarifa hiyo na kujiridhsiha kuwa si ya kweli.

Ufuatiliaji kwa njia ya utafutaji wa maneno muhimu imebainika kuwa hakuna chanzo chochote cha kuaminia kilichochapisha taarifa hiyo kwa hivi karibuni (Agosti, 2025). Shirika la habari la AP April 2, 2024 walichapisha taarifa kuwa;

“A giant chunk of Highway 1 collapsed into the ocean following heavy weekend rains, stranding as many as 1,600 people in the coastal community of Big Sur, California” (Sehemu kubwa ya Barabara Kuu namba 1 imeporomoka na kutumbukia baharini kufuatia mvua kubwa zilizonyesha mwishoni mwa wiki, na kuwaacha watu takribani 1,600 wakiwa wamekwama katika jamii ya pwani ya Big Sur, California.).

Ufuatiliaji kwa njia ya google reverse image search imebainika kuwa kipande hiko cha video kimewahi kuchapishwa pia na watumiaji wengine wa mitandao ya kijamii ikiwemo TikTok, mathalani akaunti ya World AI ilichapisha video hiyo ikiwa na ujumbe tofauti ambao hautaji eneo la Calfornia kama sehemu ambayo tukio hilo lilitokea.

Aidha ufuatiliaji kwa kutumia nyenzo za kidijitali JamiiCheck imejiridhisha kuwa video hiyo imetengenenzwa kwa teknolojia ya Akili Unde. Ufuatiliaji umebaini mambo yafuatayo yanaoyodhihirisha hilo.

Mosi, Watu waliopo eneo la tukio hawaoneshi kushtushwa na tukio linaloendelea katika eneo hilo.

Pili, Miongoni mwa madereva waliopo kwenye baadhi ya magari hawaonekani kuwa ni watu halisi pia hawaoneshi ishara zozote za kibinadamu badala yake wameganda tu.

Tatu, Vumbi linaloonekana kutokea siyo halisi kutokana namna linavyotokea linaonekana kama maji.

Nne, Mara baada ya magari kuporomoka yanapotea na kuonekana yamekuwa vumbi pia.
Technology imekua ya ajabu sana

Fullstop, kwishaaaa
 
Back
Top Bottom