Wadau wa Jf naombeni ushauri.Mimi ni Mwalimu katika Halmashauri ya Wilaya ya SHINYANGA VIJIJINI.Nilipandishwa daraja/cheo tangu mwezi November,2011.Lakini mpaka sasa sijabadilishiwa mshara,si mimi tu kwani wapo na wengine kadhaa naowafahamu wenye tatizo kama langu.Nikifuatilia Ofisi ya DED naambiwa taarifa zimeshatumwa nisubirie mabadiliko lakini ndio hivyo tena.Hali hii imefanya morality yangu ya kazi ishuke down to the earth.
Hatujapeleka malalamiko CWT rasmi ila hii case wanaifahamu.Mwezi Machi walitoa fomu kwa Afisa Elimu kwa ajili ya kuorodhesha majina ya walimu wenye tatizo hilo na tunaambiwa walikuwa wanafuatilia Utumishi,bado hatujapata feedback.vipi cwt umepeleka lalamiko lako? maana moja ya kazi yao ni hiyo na wanakukata pesa kila mwezi hivyo nakushauri wewe na wenzako muende cwt , lkn kabla nenda kwa mkurugenzi na wakujibu kwa barua kuwa lini walituma taarifa ili kama unaweza ufuatilie hadi wizara ya tamisemi kwa baadae.