Darasa la saba Dar kufanya mitihani 16 Jan 2020, Necta watoa ufafanuzi

Darasa la saba Dar kufanya mitihani 16 Jan 2020, Necta watoa ufafanuzi

Mi naona hapa mkazo uwekwe kwa Elimu ya awali tu kwani huko ndio wanafunzi huandaliwa.
Kwa uelewa wangu mdogo mkoa ambao umefanya vibaya zaidi ndio hii semina ilitakiwa ipelekwe.

Halafu utungaji mitihani sidhani kama una uhusiano na kufaulu, shida kubwa niionayo mimi ni wanafunzi kutomaliza mitaala na upungufu wa walimu ndio unaofanya matokeo kuwa mabaya.

Unforgetable

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TataMadiba,
Kwa nini iwe dar pekee,

kwa nini isiwe Rukwa na Simiyu?

Au ndiyo kampeni za kuishusha Kilimanjaro kuwa kinara wa Elimu?
Hili swali lilimuhitaji Dr ajibu na ni mojawapo ya maswali konki sana yanayoulizwa kwenye defending ya proposal au thesis academically
 
Kucheka kwenye msiba ni upunguani, na kulia kwenye tafrija ni uchuro. Sasa, NECTA, mnataka kuliaminisha taifa letu kwamba serikali yetu tukufu, iliajiri Walimu , ambao hawakufaulu kabisa somo la Tathimini na Upimaji vyuoni? Semina 'miradi' hizi zitakomeshwa lini hapa nchini?
 
Vipi kuhusu ufundishaji? Wanafunzi wanafundishwa kukariri mitihani na si uelewa wa walichofundishwa darasani muda wote!

Sent using Jamii Forums mobile app
Matokeo ya kukaririshwa mtihani tunayaelewa vizuri sana. Mwanafunzi anakwenda kidato cha tano ana daraja la kwanza la alama saba. Mnapoanza masomo anakuwa anashangaa katika baadhi ya masomo ya "combination" yake kiasi cha kwamba wengine wanamshangaa kapataje hizo alama. Ni mwendo wa kukaririshwa mtihani toka Januari hadi mwisho wa mwaka, na hivyo hata maswali yakitungwa vipi lazima watapasua tu.
 
Wanafunzi wamefungua shule tarehe 6 january, kesho ni tarehe 16
Hivi ndani ya huo muda, walimu na wanafunzi wanaweza kuwa wamesoma kiasi cha kucover mada zote za darasa la saba?
Aliyekwambia watatoa topic zote nan...? Na kuna ubaya gan wakitunga topic zote?
 
Back
Top Bottom