Darasa la Saba kufanya mtihani kesho, unakumbuka nini ulipokuwa unafanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi?

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Wanafunzi 1,172,279 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi, uliopangwa kufanyika kesho na kesho kutwa nchini, wakiwamo wavulana 535,138 na wasichana 637,141.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 9, 2025, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Profesa Said Ally Mohamed, amesema watahiniwa hao wanatoka shule 19,441 Tanzania Bara.

“Watahiniwa 1,094,321 sawa na asilimia 93.35 watafanya mtihani kwa lugha ya Kiswahili na watahiniwa 77,958 sawa na asilimia 6.65 watafanya kwa lugha ya Kiingereza,” amesema.

Amesema watahiniwa 4,699 wenye mahitaji maalumu watakaofanya mtihani huo wakiwamo wasioona, wenye uoni hafifu, uziwi, ulemavu wa akili na wa viungo.

Amesema watahiniwa watafanya mtihani wa masomo sita ambayo ni Kiswahili, Kiingereza, Sayansi na Teknolojia, Hisabati, Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi pamoja na Uraia na Maadili
 
Kuandaa chakula cha kwenda nacho shule.

1.Hesabu
2.Maarifa
3.Lugha

Mawazo yalikuwa kupiga zaidi ya 120.
 
Nawatakia kila jema wakakumbuke yote waliyosoma wafaulu kwa kishindo.

Mimi nilikuwa nawaza marafiki wengi hatutaonana tena na ni kweli nilipotezana na wengi tangu nimalize sijawahi kuwaona.

Nimemaliza karibu miaka 40 sasa iliyopita wakati ambao hauna mawasiliano kama ilivyo sasa.
 
2009 hiyo.. time flies 😁
Paper la mwisho, me na rafiki angu tukaenda kumpiga mtu makonzi. Alizidisha mazoea
 
Nakumbuka ilikua mwaka 2004 hiyo nilikua darasa la sita. Mimi ndio nilikua kichwa cha darasa. Siku darasa la 7 wanajaza form za kuchagua shule wanazotaka kupangiwa form1, mwalimu mkuu aliniita ofisini kwake akaniambia nijaze zile form na darasa la 7 halafu nitafanya nao mtihani wa taifa kama nikifaulu nitaenda form 1, nisipofaulu nitaendelea darasa la 7 mwakani na darasa la 6 wenzangu. Nikaona sio mbaya, nikajaza form.

Siku ya mtihani imefika. Lile jina la "mtihani wa taifa" liliniogopesha kidogo nikajua ni mtihani mgumu kinoma. Ukizingatia sina uzoefu wa kufanya mtihani wa taifa kwa sababu mtihani wa taifa wa darasa la nne sikufanya maana nililukishwa darasa from std 3 to std 5.

Ile kupiga pepa la kwanza tu sijaona swali lolote la maana. Pepa la pili nalo sijaona changamoto yoyote. Nikasema kumbe mitihani ya taifa haina cha kutisha. Nikabamiza mitihani yote form 1 nikachagulia Azania secondary
 
Vipanga mnatutambia sana
 
Mimi nilisoma na kumaliza elimu ya msingi pale Chamazi primary school.

Nakumbuka miaka hiyo usafiri ulikua shida sana ,kulikua na vihiace na magari ya mchanga na sisi wanafunzi kwasababu ya manyanyaso ya makonda tulikua tunapewa sana lift kwenye magari ya mchanga.

Nakumbuka siku ya mwisho ya kufanya pepa tulipanda gari(Lori la mchanga nakumbuka liliandikwa Moto wa gesi) pale Mbagala Rangi 3. Dereva akatupeleka mpaka nje ya darasa pale ndo akaenda kutushusha ilikua vibe la hatari sana kipindi kile 😁
 
Wanafunzi 1,172,279 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi
Idadi kubwa sana hii, miaka 4 badae wanamaliza form 4, sehemu kubwa wataishia hapo wengi wakiwa na miaka 18, watu wazima kabisa.

Lakini elimu ya miaka 11 itakuwa haijawasaidia kupambana na maisha, watamaliza bila ujuzi wowote(vocation skills).

Pamoja na Serikali kuboresha mitaala, mzazi unawajibu wa kumjengea mwanao uwezo, kila likizo iwe ya yeye kujifunza ujuzi wowote, mfano; kushona, welding, kujenga, kupaka rangi, capentry, udereva, coding, land surveying n.k. Ili akimaliza aingie mtaani kupambana.
 
Wanafunzi 1,172,279 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi, uliopangwa kufanyika kesho na kesho kutwa nchini, wakiwamo wavulana 535,138 na wasichana 637,141.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 9, 2025, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Profesa Said Ally Mohamed, amesema watahiniwa hao wanatoka shule 19,441 Tanzania Bara.

“Watahiniwa 1,094,321 sawa na asilimia 93.35 watafanya mtihani kwa lugha ya Kiswahili na watahiniwa 77,958 sawa na asilimia 6.65 watafanya kwa lugha ya Kiingereza,” amesema.

Amesema watahiniwa 4,699 wenye mahitaji maalumu watakaofanya mtihani huo wakiwamo wasioona, wenye uoni hafifu, uziwi, ulemavu wa akili na wa viungo.

Amesema watahiniwa watafanya mtihani wa masomo sita ambayo ni Kiswahili, Kiingereza, Sayansi na Teknolojia, Hisabati, Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi pamoja na Uraia na Maadili
Uvutaji wa msuba. Nilianzaga toka la nne Patandi.

adriz The Consigliere Chaliifrancisco
 
Nakumbuka Kuna mdada alikuja na fish sato na ugali aisee mnafanya mitihani mnaskia harafu ya samaki🤣🤣 sahivi una watoto nimekukumbuka sana
 
Idadi kubwa sana hii, miaka 4 badae wanamaliza form 4, sehemu kubwa wataishia hapo wengi wakiwa na miaka 18, watu wazima kabisa.

Lakini elimu ya miaka 11 itakuwa haijawasaidia kupambana na maisha, watamaliza bila ujuzi wowote(vocation skills).

Pamoja na Serikali kuboresha mitaala, mzazi unawajibu wa kumjengea mwanao uwezo, kila likizo iwe ya yeye kujifunza ujuzi wowote, mfano; kushona, welding, kujenga, kupaka rangi, capentry, udereva, coding, land surveying n.k. Ili akimaliza aingie mtaani kupambana.
Wakati huo abdul na mamaye wakizidi kupulizia vijambio vyao perfume za mil 50..... na kununua gari za bil4
 
Back
Top Bottom