The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Wanafunzi 1,172,279 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi, uliopangwa kufanyika kesho na kesho kutwa nchini, wakiwamo wavulana 535,138 na wasichana 637,141.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 9, 2025, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Profesa Said Ally Mohamed, amesema watahiniwa hao wanatoka shule 19,441 Tanzania Bara.
“Watahiniwa 1,094,321 sawa na asilimia 93.35 watafanya mtihani kwa lugha ya Kiswahili na watahiniwa 77,958 sawa na asilimia 6.65 watafanya kwa lugha ya Kiingereza,” amesema.
Amesema watahiniwa 4,699 wenye mahitaji maalumu watakaofanya mtihani huo wakiwamo wasioona, wenye uoni hafifu, uziwi, ulemavu wa akili na wa viungo.
Amesema watahiniwa watafanya mtihani wa masomo sita ambayo ni Kiswahili, Kiingereza, Sayansi na Teknolojia, Hisabati, Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi pamoja na Uraia na Maadili
Binadamu si milima inaweza isiwe wote lakini ukakutana nao baadhiMimi nilikuwa nawaza marafiki wengi hatutaonana tena na ni kweli nilipotezana na wengi tangu nimalize sijawahi kuwaona.
Mlienda kumpga mkijua hatakua na pakuwasemeaPaper la mwisho, me na rafiki angu tukaenda kumpiga mtu makonzi. Alizidisha mazoea
Vipanga mnatutambia sanaIle kupiga pepa la kwanza tu sijaona swali lolote la maana. Pepa la pili nalo sijaona changamoto yoyote. Nikasema kumbe mitihani ya taifa haina cha kutisha. Nikabamiza mitihani yote form 1 nikachagulia Azania secondary
Idadi kubwa sana hii, miaka 4 badae wanamaliza form 4, sehemu kubwa wataishia hapo wengi wakiwa na miaka 18, watu wazima kabisa.Wanafunzi 1,172,279 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi
Uvutaji wa msuba. Nilianzaga toka la nne Patandi.Wanafunzi 1,172,279 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi, uliopangwa kufanyika kesho na kesho kutwa nchini, wakiwamo wavulana 535,138 na wasichana 637,141.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 9, 2025, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Profesa Said Ally Mohamed, amesema watahiniwa hao wanatoka shule 19,441 Tanzania Bara.
“Watahiniwa 1,094,321 sawa na asilimia 93.35 watafanya mtihani kwa lugha ya Kiswahili na watahiniwa 77,958 sawa na asilimia 6.65 watafanya kwa lugha ya Kiingereza,” amesema.
Amesema watahiniwa 4,699 wenye mahitaji maalumu watakaofanya mtihani huo wakiwamo wasioona, wenye uoni hafifu, uziwi, ulemavu wa akili na wa viungo.
Amesema watahiniwa watafanya mtihani wa masomo sita ambayo ni Kiswahili, Kiingereza, Sayansi na Teknolojia, Hisabati, Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi pamoja na Uraia na Maadili
Wakati huo abdul na mamaye wakizidi kupulizia vijambio vyao perfume za mil 50..... na kununua gari za bil4Idadi kubwa sana hii, miaka 4 badae wanamaliza form 4, sehemu kubwa wataishia hapo wengi wakiwa na miaka 18, watu wazima kabisa.
Lakini elimu ya miaka 11 itakuwa haijawasaidia kupambana na maisha, watamaliza bila ujuzi wowote(vocation skills).
Pamoja na Serikali kuboresha mitaala, mzazi unawajibu wa kumjengea mwanao uwezo, kila likizo iwe ya yeye kujifunza ujuzi wowote, mfano; kushona, welding, kujenga, kupaka rangi, capentry, udereva, coding, land surveying n.k. Ili akimaliza aingie mtaani kupambana.