Darasa la Saba na Ubunge

Darasa la Saba na Ubunge

Protector

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Posts
422
Reaction score
893
Habari wanajukwaa,

Nimekuwa nikijiuliza Maswali mengi sana juu ya utumishi wa wabunge ambao ni darasa la saba. Muongozo wa ajira Serikalini ni kwamba wanaajiri kuanzia kidato cha nne na kuendelea, kama huna cheti cha form four huna sifa ya kuwa mtumishi wa umma.

Ninavyoelewa mimi inawezekana isiwe hivyo, mtumishi wa umma ni yule anayelipwa mshahara wake na serikali (kupitia kodi za wananchi). Kama serkali iliamua kuwatoa kwenye ajira watumishi wake ambao walikuwa na elimu ya darasa la saba, kwa nini wabunge wa darasa la saba hawakuguswa ili hali nao ni watumishi wa umma.

Mtumishi aliyekuwa dereva au mfanya usafi akaondolewa kwenye ajira kwa sababu ya darasa la saba, serikali haioni kuwa ilimuonea mtu huyo wakati kuna mbunge ambaye ana majukumu makubwa ya kitaifa ikiwamo kutunga sheria na kuishauri serikali. Utampate kazi mtu wa darasa la saba ya kutunga sheria na kushauri serkali wakati huohuo mfanya usafi na dreva ambaye anatolewa kwenye ajira kwa elimu ileile ya darasa la saba.

Serikali ipitie upya hii mifumo na ikiwezekana waongeze ufaulu wa elimu kuwa na sifa ya kugombea ubunge angalau iende mpaka kidato cha sita au stashahada (Diploma).
 
Hao Wabunge Darasa la Saba Walitakiwa wawe Wachunge Ng'ombe au Kufuga Kuku wa Kianyeji maana wa Kisasa Wangewapa Hasara as they are not risk takers, basi tu Umbumbu wa Watanzania Umewabeba.
 
Kanuni za kugombea nafasi za Udiwani na Ubunge zinataka mgombea ajue walau Kuandika, Kusoma na Kuhesabu. Basi!
Kanuni zibadilishwe, Diwani aanzie form four na mbunge form six au Diploma.
 
Kuhesabu haipo! Ni kusoma na kuandika, kiswahili au kiingereza au vyote
Inaniuma sana kuona darasa la saba wamepewa sehemu nyeti kama bunge huku wengine wakinyimwa hata fursa ya kufanya usafi majengo ya serkali
 
Hao Wabunge Darasa la Saba Walitakiwa wawe Wachunge Ng'ombe au Kufuga Kuku wa Kianyeji maana wa Kisasa Wangewapa Hasara as they are not risk takers, basi tu Umbumbu wa Watanzania Umewabeba.
Hakuna usawa kabisa.
 
Tungeanza kwa kuondoa viti maalum vya ubunge halafu tupandishe kiwango cha elimu ya mbunge.
 
Hao Wabunge Darasa la Saba Walitakiwa wawe Wachunge Ng'ombe au Kufuga Kuku wa Kianyeji maana wa Kisasa Wangewapa Hasara as they are not risk takers, basi tu Umbumbu wa Watanzania Umewabeba.
Unaposoma halafu ukawa na matarajio makubwa bila kujibidiisha,lazima uwaonee wivu ambao hawakusoma na wanapiga maisha baada ya kujibidiisha.
 
Unaposoma halafu ukawa na matarajio makubwa bila kujibidiisha,lazima uwaonee wivu ambao hawakusoma na wanapiga maisha baada ya kujibidiisha.
Ishu sio kusoma sana uanze kuona wivu kwa wabunge wa darasa la saba. Hapa tunaongelea maslahi mapana ya taifa na kazi wanazozifanya kama watunga sheria wakuu.
 
Ishu sio kusoma sana uanze kuona wivu kwa wabunge wa darasa la saba. Hapa tunaongelea maslahi mapana ya taifa na kazi wanazozifanya kama watunga sheria wakuu.
Mkuu, busara ya uwakilishi wa wananchi haihitaji kiwango kikubwa cha elimu ya darasani. Hakuna ushahidi wa Mbunge "aliyesoma" ndio anakuwa Mwakilishi mzuri wa wananchi. Sana sana Wabunge waliosoma wanaviaGA uwaziri tu.
 
Hawa jamaaa hawana impact yoyote kwa wananchi , hivi kweli Babu tale na yeye Mbunge anatakiwa aishauri na kuikosoa Serikali kweli?
 
Mkuu, busara ya uwakilishi wa wananchi haihitaji kiwango kikubwa cha elimu ya darasani. Hakuna ushahidi wa Mbunge "aliyesoma" ndio anakuwa Mwakilishi mzuri wa wananchi. Sana sana Wabunge waliosoma wanaviaGA uwaziri tu.
Ni kweli kabisa maana wakati mwingine uongozi ni kipaji.
Nilichokuwa nahoji hapa kwa nini mfanya usafi au dreva wa darasa la saba hapaswi kupewa kazi serikalini wakati kazi yake haihitaji kujieleza au kuongoza?
 
Back
Top Bottom