Protector
JF-Expert Member
- May 20, 2019
- 422
- 893
Habari wanajukwaa,
Nimekuwa nikijiuliza Maswali mengi sana juu ya utumishi wa wabunge ambao ni darasa la saba. Muongozo wa ajira Serikalini ni kwamba wanaajiri kuanzia kidato cha nne na kuendelea, kama huna cheti cha form four huna sifa ya kuwa mtumishi wa umma.
Ninavyoelewa mimi inawezekana isiwe hivyo, mtumishi wa umma ni yule anayelipwa mshahara wake na serikali (kupitia kodi za wananchi). Kama serkali iliamua kuwatoa kwenye ajira watumishi wake ambao walikuwa na elimu ya darasa la saba, kwa nini wabunge wa darasa la saba hawakuguswa ili hali nao ni watumishi wa umma.
Mtumishi aliyekuwa dereva au mfanya usafi akaondolewa kwenye ajira kwa sababu ya darasa la saba, serikali haioni kuwa ilimuonea mtu huyo wakati kuna mbunge ambaye ana majukumu makubwa ya kitaifa ikiwamo kutunga sheria na kuishauri serikali. Utampate kazi mtu wa darasa la saba ya kutunga sheria na kushauri serkali wakati huohuo mfanya usafi na dreva ambaye anatolewa kwenye ajira kwa elimu ileile ya darasa la saba.
Serikali ipitie upya hii mifumo na ikiwezekana waongeze ufaulu wa elimu kuwa na sifa ya kugombea ubunge angalau iende mpaka kidato cha sita au stashahada (Diploma).