hizi ndio akili na maombi ya watzDarasa ni sikio la kufa na hana uwezo wa kukaa juu muda mrefu.
Msanii ana wimbo mkubwa lakini hana management.
Huu wimbo umekuwa mkubwa kumzidi na utamuangusha.
Atoe ukali mwingine.....
Jamaa kipindi hicho alikuwa anakitu cha kuelimisha jamii nadhani sasa hivi anaburudisha jamii
Tayari amekolabo na BenPol itatakiwa Collaboration zaidi na msanii Mwingine??
Darasa ni msanii wa muda mrefu sana, sema muanzisha uzi, umeanza kumfiatilia siku hizi ananyimbo nyingi sana kama sikati taa,sio mbaya, hahe hahe, kipindi hicho yupo am records, alivyohamia kwa mrttouch ndio akaswitch, kumbuka kuna muda utafika nyota inang'ara na unaanza kula matunda ya kazi yako basi ndio muda wake huu
wimbo wa hovyo kabisa, sema wengi mnastress nchini
Ni kweli, ila kumbuka kwamba alikuwa bado hajafika kwenye peak, sasa ndio yupo kwenye peak, mara nyingi ukiwa kwenye level hizo ndio inakuwa kazi kubwa kumaintain maana wasanii wengi wanatabia ya kujisahau na kuridhika. Mfano mzuri ni 20% alitoa ngoma nyingi kali ila raia walimpuuza, alipotoa tamaa mbaya karibu kila mtanzania alimuelewa, lakini baada ya hapo hakuna alichofanya. Je unadhani kipaji kiliisha? La Hasha, ndio hivyo wasanii wengi wanajisahau wanapokuwa peak. Ndio maana Darasa anatakiwa awe na management makini ili aendelee kuwa pale, hata Diamond asingekuwa na management nadhani tungekuwa tushamsahauUmenena vyema mkuu. Binafsi ngoma za darassa nnazozifahamu ni sikati tamaa, nishike mkono, hahe hahe ft blue, sio mbaya, komaa remix, kama utanipenda, too much and finally muziki. Ila binafsi nauona sikati tamaa kama nyimbo bora kabisa iliyowahi kuandikwa na darassa,na ndiyo ilifanya nimfahamu jamaa. baada ya kuswitch ndo zikaja kama utanipenda, too much na hatimaye muziki, ambazo zote ni hit songs. Kwa wanaomfahamu vizuri jamaa wanajua kua mziki anaujua kitambo, na naamini haitampa shida kumaintain alipo sasa. Inshort jamaa alikua anaudai mziki, na ilikua ni suala la mda tu kabla mziki haujaanza kumlipa.
Ni kweli...ana kazi kubwa kuja kuvunja hii rekodi...Darasa ni sikio la kufa na hana uwezo wa kukaa juu muda mrefu.
Msanii ana wimbo mkubwa lakini hana management.
Huu wimbo umekuwa mkubwa kumzidi na utamuangusha.
Nimekuelewa vizuri sana mkuu. Ngoja tusubiri tuone, time will tellNi kweli, ila kumbuka kwamba alikuwa bado hajafika kwenye peak, sasa ndio yupo kwenye peak, mara nyingi ukiwa kwenye level hizo ndio inakuwa kazi kubwa kumaintain maana wasanii wengi wanatabia ya kujisahau na kuridhika. Mfano mzuri ni 20% alitoa ngoma nyingi kali ila raia walimpuuza, alipotoa tamaa mbaya karibu kila mtanzania alimuelewa, lakini baada ya hapo hakuna alichofanya. Je unadhani kipaji kiliisha? La Hasha, ndio hivyo wasanii wengi wanajisahau wanapokuwa peak. Ndio maana Darasa anatakiwa awe na management makini ili aendelee kuwa pale, hata Diamond asingekuwa na management nadhani tungekuwa tushamsahau
Asiache kuchomekea hizo za mafunzoMi nadhani darasa ni mwandishi mzuri sana na kiukweli nyimbo kama Sikati tamaa au Nishike mkono zina ujumbe mzito kuliko hii iliyovuma kupita zote.. Kikubwa atambue wabongo wanapenda nyimbo za kuchezekachezeka zaidi kuliko mashairi yenye ujumbe conscious hivyo anaweza kukaa juu ili mradi aandike nyimbo zenye sample kama ya MUZIKI
Na watu wengi wanapenda sana labda sababu ya hali ya maisha au vpKuburudisha jamii ina uza mkuu.
Acha uongo hiyo ngoma imejipromoti yenyewe,wengi tumeijulia mitandaoni na sio redion, "mwenye mapembe muongezee mkia" au unao tayali?Huo Wimbo Uwewekwa Juu Na Clouds Maana Walikuwa Wanaupiga Kila Baada Ya Dk 2 - Kwasababu Walikuwa Wana Biashara Nae,
- Fiesta
- Salama Kondom
- After Skul Bash
Hayo Matamasha Ya Clouds Zimembeba Sana.
Huo Wimbo Uwewekwa Juu Na Clouds Maana Walikuwa Wanaupiga Kila Baada Ya Dk 2 - Kwasababu Walikuwa Wana Biashara Nae,
- Fiesta
- Salama Kondom
- After Skul Bash
Hayo Matamasha Ya Clouds Zimembeba Sana.
Sijui wale mademu wenye mishepu kwenye video zake sijui anawatoaga wapi darassa
Huyu jamaa kiukweli nilikuwa nasikia tu jina lake na ni msanii wa rap ila kama ingetokea tukapishana wala simjui kama ambavyo hanijui. Hata ungeniambia kaimba wimbo upi ningeshindwa kukutajia. Nawafahamu kina Godzilla, FA, Fid Q, etc. Sasa kama ilivyo kwa wengine naona nyota ya Jaha imemdondokea huyu msanii. Niliufahamu wimbo kupitia ile clip ya wale jamaa waliopagawa hadi kuachia usukani. Baada ya hapo nikaanza kumsikia kwenye vyombo vya habari. Nikasiliza na wimbo wake ila bado sikuona kipya.
Sasa ikawa kila nakopita nausikia huu wimbo. Boda boda, redio na tv, kwenye biashara za watu. kwenye simu za watu, n.k. Kiukweli nami taratibu nikaona unaanza kuniteka. Nikaupenda. Umekuwa wimbo wa taifa. nilipita duka moja kuna jamaa alikuwa kauweka huu wimbo na unajirudia rudia. Kwa muda niliopita pale ni kuwa ulishajirudia kama mara kumi hivi.
sasa baada ya kipindi hiki cha mpito we jamaa utafanyaje ukae hapo juu? Kwa sasa usichekelee sana. Anza kujiuliza utafanya nini? Kama ni matatizo basi ndio hayo umejitakia. Jipange tena
Kama kipaji kipo kipo tu atagonga hiy song zz kutosha tu ila kama ilikuwa zali ka mentali basi atakwama..
Ingawa promo ikipigwa vizuri hata kama nyimbo ni mbaya inaweza pendwa tu na wasikilizaji