Darassa akonga nyoyo za Wakenya, Mashabiki wa Muziki wamlilia akapige show Kenya

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506
Baada ya Wimbo wa Muziki kukonga mashabiki wengi hapa nchini, mashabiki wa muziki nchini Kenya wametoa kilio chao na kuomba Darassa akafanye show nchini mwao.

Msanii wa muziki nchini Kenya maarufu kama Nyota Ndogo akizungumzia ishu hii amesema amekuwa akipata wakati mgumu kutoka kwa mashabiki nchini humo pindi anapokuwa akifanya show zake mbali mbali, wengi wa washabiki wakitaka uchezwe kwanza wimbo wa Darassa kabla ya show kuanza au wakimsimamisha katikati ya show ili upigwe wimbo wa Darassa kwanza ndio show iendelee.

Nyota ndogo amesema juzi alikuwa na show mjini Malindi, mashabiki walimstopisha alipokuwa anamaliza show yake na kumtaka DJ acheze wimbo wa Darassa huku wakimlazimisha Nyota Ndogo acheze wimbo huo.

"darassacmg plz kuna pesa zako kenya zinakungoja.this was my show in malindi.nimemaliza kupiga show mashabiki wanamuomba dj acheze nyimbo yako na mimi ni dance.

Nipo na video yani mimi ni dance.kimbia huku mara moja kabla nyimbo haijaisha ufanye tour unamashabiki sio tz pekeake.do it now."

Wengi wa mashabiki mitandaoni nchini Kenya wamekuwa wakiwalilia ma-promoter nchini humo wamlete Darassa na kuna tetesi mipango imekwishaanza kufanyika nchini humo.
 
Something very amazing about this song muziki. Jamaa yangu mmoja yuko India anasema new year ilipigwa club huko ukumbi mzima ukalipuka. China na SA pia ni shida. Dogo akijipanga fresh ataenda juu sana.
Ni kweli mkuu, tatizo la wasanii wetu wa kibongo hawana mikakati ya kutchangamkia fursa kama hizi kutoka.

Angetakiwa ndani ya kipindi cha miezi mitatu hii azunguke nchi nzima na nje ya nchi kupiga show za ukweli kabla ya song halijapoa.

Akizubaa utaibuka wimbo mpya hapa kati, watu watamsahau.
 
Ndio muda wake huu. Ningependa kusikia huyu jamaa kapiga show kimataifa. Namkubali sana.
 
Ili afanikiwe zaidi akae na mdogo wake Diamond, apate mawili matatu..!

Kutoa ngoma kali ni jambo moja
Kuufanyia muziki wako biashara ni jambo jingine.
 
Sasa huu ndo wakat wake wakupga pesa apunguze bange na chupa apge pesa
 
Mbongo ata afanye kitu kizuri vipi kuna mbongo mwingne ata mind...
 
Hapo huwezi mlaumu msanii, nadhani mapromota ndio inapaswa waione hiyo fursa, ila na yeye Darasa inapaswa ajiongeze ikiwezekana kutengeneza connection Kenya kama mapromota hawajamfata
 
Something very amazing about this song muziki. Jamaa yangu mmoja yuko India anasema new year ilipigwa club huko ukumbi mzima ukalipuka. China na SA pia ni shida. Dogo akijipanga fresh ataenda juu sana.


Ashachelewa
 
Huu ni muda wa darasa kupiga hela....inawezekana asipate airtime kubwa kama hii...asiingie kwenye team zisizo na viwanja...meneja wake akae na mameneja waliovuka mipaka ya TZ wamweleze namna ya kupata shows huko....Rwanda wanamsubiri kwa hamu sana...a
 
Duuuu yani wimbo kusumbua kote kule, hajapga show hata Kenya....Anazidiwa na Manfongo kapiga show hadi south Africa....
CMG changamka
 
Darasa atafute walau management ya muda kwa ajili ya kipindi hiki tu...kuna karibu ya sh milioni 500 au zaidi zinamsubiri na asipokuwa makini hatozifikia.
 
Hapo huwezi mlaumu msanii, nadhani mapromota ndio inapaswa waione hiyo fursa, ila na yeye Darasa inapaswa ajiongeze ikiwezekana kutengeneza connection Kenya kama mapromota hawajamfata
Siku zote inaanza na wewe, mtegemea cha ndugu hufa masikini...kazi ni ya Darasa hivyo ana wajibu kuona ni nini kinafanyika sio kwa kuwa tu mapromoter wanalala basi naye akae na kusubiri.

Kwa hali ilivyo sasa Darasa ana nafasi kubwa ya kujaza uwanja popote pale Washabiki watakapojua anakuja...hivi ni kitongoji gani hapa bongo kwa sasa utacheza hii ngoma iache kuamsha?
 
Ni wivu ama nini nanusa hapa
Ni wivu ama nini nanusa hapa

Hakuna wivu mkuu najarib tu kuangalia yale mahojiano aliyofanya juzi kati pamoja na comment zetu mashabiki, kila msanii atakaefanya vzr now basi tutaanza kumtia ujinga na kumshawishi kuwa ye yupo juu zaidi ya wale walio juu yake, the way single yake inavyohit nadhan ingekuwa vzr sn kwa yeye ama management yake kutafuta channel za show kwa majiran zetu ss km hadi ss hv hajafanya hvo we unapata picha gn mkuu!! kwa hali ilivyo unahic jamaa naweza kwenda [HASHTAG]#wcb[/HASHTAG] kuomba ht ushauri!!! afu kumbuka ni single tu ambayo muda wowote inaweza ikatoka nyingine itakayofunika hii ya kwake.
 
duh. ama kweli. muziki ni kazi. kama ni msomaji atakuwa ameshapita humu kupata elimu.
sioni dalili ya hit ingine siku za usoni. so inabidi ajipange kwa hio hata kwa hela ya kukopa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…