Dark days 17/03/20...

[emoji1787][emoji1787][emoji1787] mbuyu unadondoka
 
Tuliosoma Cuba tumekuelewa
 
Mkuu... Deep siteti.. Ni ngumu kujua undani wake... BT anajua baadhi ya members tuu... Yeye BT hana shida nao... Amejifunza toka zamani kuishi na jamii vizuri...

Ukiwa CEO wa kampuni... Huwa unakuwa na kazi nyingi sana... sasa inategemea washauri unaowachagua...
Ukiwa Ceo... Huwezi kuvuruga kila kitu cha nyuma na kujiona wewe ndio mwenye uwezo mpana wa fikra kuliko wenzako...

Kampuni inaangalia mapato na matumizi ...kampuni ilishaanza kuwa hohehahe... Na kukimbilia account binafsi za waweka mitaji...
Kampuni ingefilisika... Kutokana na sera za ceo na uoga alioupandikiza kwa wafanyabiashara.....
 
Sure pale kwenye uzinduzi amemiss point za bure kabisa, kwanza ilikua ni nasibu tu kupata nafasi ya kuongea, angetumia nafasi hiyo kutupoteza maboya wakina sisi kwa kumpa sifa the late.
Kila mtu leo alikua attention kusikia jina la mr late linatajwa kwa namna gani.

State kwa ujumla ilifunika sana jina tarajiwa kutajwa, walao mwenye nyumba mpya ametambua jina lile lilitakiwa kutamkwa sana kwenye shughuli ile.

Pale mr bt angechukua pointi za bure kabisa kama asinge skip mwandamizi wake, ameanza vizuri kwa teacher akaja kidogo kwa rks halafu kwa kiasi kikubwa akasimama kwenye engo yake, mwishoni akamalizia kwa kwa aliyepo, kwa bahati mbaya sana au kwa kujisahau au ni makusudi aliskip awamu ya mkono!

Lakini nadhini ndio kawaida yake , tukizingatia hotuba ile msibani kwa bwm , alipopewa tu nafasi alijifagilia sana, hata kule geita alipopewa nafasi alijifagilia sana, hata la leo sio makusudi au kujisahau bali ndio moyoni mwake alivyo.
 
Ndio mkuu.
Kina kirefu ambacho kukipima wahitaji vifaa maalum.

Mwamba plans zake kutoka akiwa monduli ndizo anazoziishi sasa. BT ndiye CEO aliyeukwa uCEO kwa kuuchorea ramani toka kitambo sio kitu cha kubahatisha.
Naam , kitu pekee alichojaliwa ni uvumilivu na tabasamu la aina yake, lakini ni mtu mwenye abc za kutosha kwenye hii state, mwanzo wake sio jana wala leo, kama alikua tayari kuwania uceo kati kati ya miaka ya 90 na aliwini kwa kiasi kikubwa dhidi ya ngome kubwa kipindi kile, aliwini dhidi ya teacher ambae ndio yake ilikua ndio na hapana yake ilikua hapana kweli. Itoshe kusema huyu mr sio wa kupika nae chungu kimoja, kosa kubwa late ceo haukuzingatia ukubwa wa huyu mtu, alidhani ukiisha kiwa chief executive officer basi hakuna yoyote juu yako wala kando yako anaweza sumbua, kumbe bwana alipo lala leo mwenzie aliamka jana, ni kusema kitanda ulicholala unajua kunguni wake!

So ilimpasa mr late akae darasani sana kabla ya kufanya aliyoyafanya mwisho wa siku imekua Garama kwake, familia na sisi sote.

Binafsi mpaka leo sijaweza kupona sawa sawa kutokuwepo kwa late ceo, pale ndio ilikua sehemu pekee ya kuvuka sisi kama campuni lakini huwenda ikatugharimu miaka hata 50 ijayo kurudi 2015-2021!
 
11. Ni nchi muhimu since it was PART OF EDEN

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Follow the MONEY utawajua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
The MoNA kama 1st CEO kwamba hakuijua yote,
1. je Mwasisi wa dip steti Tanzania ni nani?

2. Dip steti ilianzishwa mwaka gani Tanzania?

3. Malengo ya kuanzishwa Tanzania ni yapi?

Nijibu kwa fikra zangu. Wengine watajazia nyama.

Nianze kwa kusema; kuna mambo matatu yanaongoza dunia,

1. Dini.
2. Siasa.
3. Uchumi.

Kwenye angle hizi tatu, ndipo hasa dip stet imejikita.
Sasa yenyewe dip stet = PEOPLE, POWER & AUTHORITY.

Hivyo tunaona hapo dip steti ni watu wenye nguvu na mamlaka katika kuongoza nyanja tatu zinazoongoza dunia, dini, siasa na uchumi. Kwa muktadha huu tunaweza kuona dip steti ina historia ndefu kwan vitu hivi vilikuwepo tangu enzi.

Muasisi wa kampuni hii sio wa kwanza kutaka uhuru wa kampuni hii, wapo wengi wa makabila walipigana kutaka kuutokomeza utawala ulioenda kinyume na mila zao. Hapa ni zama za ma chief, lkn walishindwa kwa sababu ya kuzidiwa mambo kadhaa.
Muasisi wa kampuni alikuta tayari kuna wana harakati wakiwa wanaipigania kampuni kupata uhuru. Huku hasa ndio dip steti ilianza kwani watu hawa walikuwa na nguvu na mamlaka (ki uchumi, kisiasa na kidini).

Kwa Kampuni yetu dip steti ilianza kuundika kwa muasisi wa kampuni kwan alitengeneza mifumo kadhaa ya kuisimamia kampuni, mpaka kukabidhiwa kampuni hii kulikuwa bado na uangalizi wa wakoloni wale. Sasa wale aliowakuta wakipambania uhuru wa kampuni tayari wana nguvu na mamlaka pia. Hivyo indirectly wakawa miongoni mwa dip steti pamoja na muasisi na wawakilishi wa wakoloni. Ndipo tunakutana dip stet ndani ya dip steti ndani ya dip steti.

Hivyo swali lako namba moja naweza kusema.
Dip steti ilijianzisha yenyewe automatic kutokana na mahitaji ya kampuni na kwa wakati huo ili kuilinda kampuni ndipo taasisi rasmi zikaanzishwa mpka kwa tulipofikia leo hii.
Kwan toka kabla hata ya ujio wa Yesu Kristo na Mtume Muhammad dip steti ilikuwepo, kwa kuangali nyanja tatu hizo huko juu.

Kupata data hizi ni ngumu kwa kampuni yetu maana ni mambo nyeti haswa ndani ya kampuni.

Kwa muktadha huo mkuu, muasisi haswa wa dip stet simjui kusema ni fulani ila kuna kundi la watu ndilo naweza kusema ni waasisi, ambao walikuwepo kipindi cha ukoloni na kipindi cha uhuru. Baada ya huru

Najua wapo wenye taarifa rasmi, ila hizi zangu ni kunyofoa nyofoa tu.

Malengo ya dip steti ni kuilinda kampuni kiuchumi, kisiasa na ,kuhakikisha kuna usalama tele. Bahati mbaya sana mifumo ya dip stet imehitilafiana kiasi imekosa nguvu iliyokuwa nayo. Ila kwa mbaaaaali imeanza kurudi kwenye mikao yake ya awali. Mambo ni mengi sana yanafanyika ya kiusalama mipakani ila inakuwa siri ili kuondoa sintofahamu kwa wateja wa kampuni.

Kwa ukanda wa maziwa makuu kampuni yetu ina nguvu sana ndio maana Pk anahaha kumwangusha BT, maana ni mwiba kwake toka enzi. Hii ndio moja ya kazi ya dip steti.

Kama sijakujibu nisamehe kuu. Watakuja kutujibu kwa data vizuri.
Ahsante
 
Mkuu umeeleweka vizuri sana kwa upande wangu.
Nina wasiwasi sana na wale wazee wa mzizima aliokua akizungumza nao kila mwezi mr bt kwamba wanaweza kuwa moja wapo wa deep.
Ikumbukwe hao wazee wa mzizima chimbuko lao ni enzi za mwasisi, kipindi hicho the founder kila alichokuwa akifanya lazima ilikua aripotishe kwao, mfano mzuri mapigano yale dhidi ya nduli.

Pengine hao wazee waliundwa na mwasisi,au hao wazee walijuunda, maana mwasisi alikuja tu mjini kutokea huko vijijini akakuta kuna wazee wa mji wako na harakati zao nao wakamwingiza kwenye harakati, japo aliwazidi kete kwa mujibu wa nyuzi za memba mwenzetu hapa jukwaani.

Hao wazee ukiachilia mbali kuzaliwa mjini, pia walikuwa na nguvu ya kiuchumi walikua na nguvu ya kidini na pia walikua na nguvu ya kiroho haswa upande wa pili wa imani, tukumbuke ile taa inayozungushwa ilipo anzia.

Kwa hiyo tunaweza kusema hao wazee ni moja wapo ya ki segment katika depstate.
 

Yes..!!! Nilitaka kugusia huko ila nikaacha pawe wazi kwa watu kama wewe kufungua zaidi.

Hii dip steti ilianza kwa waliokuwapo nyakat za ukoloni na baada ya uhuru. Ambao hao wazee nao wamo.

Sahihi kabisa.
 
Aiseee hatari sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…