Dark days 17/03/20...

Amini nakuambia hiyo move itakuja kutimia siku moja!

Hatupo mbali kabisa kufikia maamuzi hayo ni swala la muda tu,mawazo ya JPM ndio framework ya siasa zijazo huko mbeleni!!!
 
....moja HAIWEZEKANI! asilani
Moja inawezekana kabisa kama watanganyika na Wazanzibari na hasa Wazanzibari watakubaliana. Na wakawa na Nia ya dhati ya kuimarisha Pan-Africanism.

Tatizo Kuna "elites" kadhaa nadhani katika pande zote mbili za Muungano wanaonufaika na set up hii ya Muungano. Na kwa kweli siamini kama Mzanzibar wa kawaida/ raia wa kawaida anachukia kuungana na mtanganyika kutengeneza Serikali moja, kama yupo kweli basi huyo atakuwa ni " kada wa elite " ( tunajua kada wa mtu ni chawa).

Binafsi, na sisitiza kumaliza kero za Muungano ni ama kuwa na serikali mbili/ nchi huru mbili zinazojitegemea kwa Kila kitu yaani Tanganyika na Zanzibar ama serikali Moja ya Muungano wa hizi nchi mbili.

Sikubaliani na Muungano wa serikali Tatu kwa sababu kutaongeza gharama kwa raia. Na kutaendeleza kero za Muungano.

Tukiwa na serikali moja hakutakuwa na malalamiko ya kwa nini wanafunzi wa Zanzibar wanachukua mkopo HESLB na kadhalika na kadhalika. Vivo hivyo tukiwa na serikali mbili/ nchi huru mbili hambazo hazihusiani katika uendeshaji wake hakutakuwa na kero za Muungano.

Hakuna kinachoshindikana chini ya Jua. Tukubali kufuta KERO za Muungano moja kwa moja na asilani tusiongeze kero za Muungano kwa kutengeneza Serikali Tatu.
====
yoga utusamehe lengo la uzi limebadilishwa siyo fictional thread Tena ambayo inatumia codes. Lakini, nadhani baada ya kuahidi kuleta uzi mwingine (huu umetelekezwa) acha tuendelee kuelimishana kupitia hapa.

Kumradhi yoga .
 
Moja inawezekana kabisa kama watanganyika na Wazanzibari na hasa Wazanzibari watakubaliana. Na wakawa na Nia ya dhati ya kuimarisha Pan-Africanism.
Haiwezekani! , Wazanzibar hawataki kujitambulisha kwa Utanzania kwasababu Uzanzibar ni Bora kwao

Kuna 'egoism' kwamba Wazanzibar ni Watu muhimu sana na wanahitaji 'special treatment' katika Muungano.
Hiyo mentality wanayo na huwezi kuiondoa.

Kuna tatizo jingine, Zanzibar ni wamoja kukiwa na Tanganyika. Wakiwa wenyewe kuna wanaoamini mapinduzi ni haramu na hutawasikia hata wakitamka. Kundi hili linaamini katika Zanzibar ya nyakati hizo na lina 'theory' kwamba mapinduzi yameletwa na Tanganyika

Kuna Mapinduzi daima, wanaamini katika mapinduzi , hawa wapo tayari kwa Serikali moja na ndio hasa wanaotaka Serikali mbili kwa hofu kwamba Usultan utarudi. Unamkumbuka Mbunge Kassim alisema nini Bungeni? Serikali moja haiwezekani! na kwangu mimi ni wazo baya sana kuliko kuunja Muungano
Binafsi, na sisitiza kumaliza kero za Muungano ni ama kuwa na serikali mbili/ nchi huru mbili zinazojitegemea kwa Kila kitu yaani Tanganyika na Zanzibar ama serikali Moja ya Muungano wa hizi nchi mbili.
Hapa una maana kuvunja Muungano. Huwezi kuwa na nchi mbili bila kitu common.
Kama unahitaji kiunganisho, ni serikali ya JMT na hapo tayari una Serikali 3
Sikubaliani na Muungano wa serikali Tatu kwa sababu kutaongeza gharama kwa raia. Na kutaendeleza kero za Muungano.
Hili ni jambo linalohitaji mjadala, nashukuru sana umelileta. Kwa hili tumalize upotoshaji wa either side
Naomba unionyeshe ni wapi, kwa namna gani Serikali tatu itaongeza gharama.
Serikali moja haiwezekani si kwasababu ya Tanganyika ni kwasababu ya Zanzibar.
Hakuna kinachoshindikana chini ya Jua. Tukubali kufuata KERO za Muungano moja kwa moja na asilani tusiongeze kero za Muungano kwa kutengeneza Serikali Tatu.

Hakuna kero za Muungano, kuna malalamiko ya Wazanzibar. Malamaiko yamejikita katika kutaka kupewa na si kuwajibika. Huwezi kudai kero ya ajira halafu ukapewa 21% kisha ukakimbia kuwalipa mishahara. Hiyo si kero

Wanadai mapato ya Visa yabaki Zanzibar, mishahara ya Uhamiaji itoke Tanganyika. Hiyo si kero
Wanataka mikopo ya nje wapate mgao Maalumu, halafu hawalipi mikopo hiyo. hiyo si kero
Wanataka kutumia umeme hawataki kulipa. Hiyo si kero
Wanapougua wanakuja Wizara ya Afya Tanganyika ili wakatibiwe India. Hiyo si kero
Wanataka bidhaa ziingie kutoka Zanzibar wasikokusanya kodi. Hiyo si kero

Orodha ni ndefu, naomba unitajie kinachoitwa kero moja genuine tuaijadili hapa

Mwisho, naomba utushawishi Watanganyika kwamba tunahitaji Muungano

 
Naomba unionyeshe ni wapi, kwa namna gani Serikali tatu itaongeza gharama.
Asante sana, Mkuu, kwa kuendelea kutoa Elimu juu ya masuala haya ya Muungano.

Umeniuliza swali ni kwa namna gani serikali Tatu zitaongeza gharama. Kuongezeka kwa gharama kwa raia Kuna jidhihirisha katika rasimu ya katiba mpya iliyoandaliwa na "Tume ya Katiba" iliyoongozwa na Mheshimiwa Jaji Warioba. Ukweli, gharama nilizosema zilikuwa zime"kokotolewa" kutoka kwenye rasimu hiyo ya Katiba.

Katika rasimu hiyo, hasa SURA YA SITA inayooelezea muundo wa Muungano utaona kabisa, kuwa Jamhuri ya Muungano itagharamiwa na raia hawa hawa wa nchi Mbili, pia wananchi hawa hawa watagharamia serikali za nchi zao. Tena katika sura hii, raia hawa hawa watalazimika kutengeneza katiba mpya nyingine za nchi zao!!! Kwa hiyo, kwenye katiba Yao watakuwa na "Rais wao" atakayelipwa mshahara na masulufu mengine na raia hawa hawa! Kifupi, raia hawa hawa watawalipa mshahara Marais wa wawili. Huo ni mfano mmoja tu wa kuongeza gharama (watanganyika wameishazoea hili nadhani)!

Pia kuhusu, Serikali Tatu kuongeza kero za Muungano (ambazo unasema ni Bora tuziite Malalamiko ya Muungano). Hili linajionyesha wazi kwenye sura hii ya SITA ya rasimu ya katiba mpya, sura ya SABA na kipengele cha Mambo ya Muungano (tafadhali yasome Tena uone kama kweli Yale yanaondoa malalamiko kwa Wazanzibari) yaliyotajwa ibara ya 63 na kuambatanishwa mwishoni mwa rasimu hiyo ya katiba mpya.

Yaani itakuwa ni vurugu badala ya Malalamiko, maana Kuna mambo mengi ambayo yana mkanganyiko hayako wazi ambayo yataleta mgongano!

Mfano, ni Ibara ya 65 na ibara ndogo zake nne ambayo inahusu mahusiano ya Nchi mshirika wa Muungano na jumuiya za kikanda na kadhalika. Yaani ibara ndogo ya nne ya ibara hii ya 65 inaelekeza Bunge ndilo litatunga Sheria ya namna Bora ya utekelezaji wa Ibara hii.

Sasa kama nchi mshirika kupitia Bunge lake ( maana watatunga katiba Yao na watakuwa na Bunge lao) itakuja na sheria tata kuhusu jambo hili itakuwaje! Maana ibara ndogo ya 3 ya ibara hii ya 65 inasema mshirika "anaweza" (siyo lazima) kumshirikisha Serikali ya Muungano juu ya Nia yake yakuwa na mshirika wa kikanda nakadhalika!!!!

Na katika kuweka sawa utata huu utakapojitokeza huko mbeleni gharama zote atabebeshwa raia hawa hawa wa nchi hizi mbili kwa kuunda matume na task forces!!!

Vipo vipengele vingi kwa kweli katika muundo wa Muungano wa serikali Tatu mbali na kuongeza gharama kwa raia lakini pia vitasababisha kero/malalamiko ya Muungano kuwa vurugu na kuhatarisha Amani na tengamano wa Raia. Tuepuke Muundo wa serikali Tatu.

Mkuu, nadhani nimejitahidi kujibu swali lako! Asubuhi njema.
 
Hao jamaa ni nyoro nyoro!Cha msingi ni kuhakikisha wanaanza kutumia ipasavyo misuli Yao kupata riziki!!


Serikali inalea hisia zao,kazi ya serikali sio kulea hisia za MTU Bali kilichobora ambacho ni utaifa wa Tanzania!!
 
Hapo kwenye siasa nipo pamoja na wewe ..Siasa imefanya Vijana kuondoa confidence na ubunifu wao, wamegeuka ma changudoa wa siasa...Imeua kabisa taifa hili...Siasa ifanywe na watu ambao wameshatumikia taifa na sasa wanafanya back stoping isiwe profession. Maana mtu mwenye kuamua vizuri ni lazima awe experienced na awe mature ..Watoto hawa wanaoenda kwenye siasa wanawaza V8 tu na kupiga basi!
 
Hoja ya Serikali tatu kuwa na gharama ni hisia za watu wasiotaka Serikali 3 kwa kupotosha Umma

Nimekuuliza na bandiko hapo chini hujaweza kuanisha kwa uyakinifu wapi gharama zitaongezeka.

Kwamba gharama zinazongezeka kwa Raia wa nchi mbili si kweli.

Kwasasa gharama amezibeba Raia wa Tanganyika pekee kwa jina la JMT

Kwa mfano, kuna Wabunge 393 akiwemo AG. Kati yao, 80+ wanatoka Zanzibar gharama zao zinabebwa na Tanganyika kwa jina la JMT ikiwemo kuwapa fedha za Tanganyika kwa mfuko wa jimbo wa Zanzibar!
Pesa za mfuko wa jimbo ni za Tanganyika kwa jina la JMT

Rasimu ya Warioba inasema kutakuwa na Wabunge 50 kutoka Tanganyika na 20 kutoka Zanzibar na Rais atateuwa 5 kutoka kundi la Walemavu kwa jumla ya 75 ( Rasimu ya Warioba Sura ya Tisa 113 (a )(b)

Idadi ya Wabunge 75 ni ndogo sana ukilinganisha na Wabunge 80 pekee kutoka Zanzibar leo hii.

Gharama za Bunge la serikali 3 ni kidogo zaidi kuliko gharama za Wabunge 80 wa JMT kwa sasa.
Watu hawaoni gharama hizi kwasababu zinalipwa na Tanganyika kutoka Hazina.

Pili, nchi Washirika zitaamua idadi ya Wabunge kutokana na Uchumi.. Kwa mfano, Baraza la Wawakilishi lina Wajumbe 50, la kushangaza Wabunge wa JMT kutoka Zanzibar ni 80+.

Ikiwa utaiambia SMZ kulipia Wabunge 80 haitakubali kwasababu BLW linalipia 50, kwavile wanalipiwa na Tanganyika hata wakija 300 hakuna anayejali kwasababu gharama kazibeba Mtanganyika.
Niambie gharama zitaongezeka wapi ?

Nije kwenye hoja zako
Katika rasimu hiyo, hasa SURA YA SITA inayooelezea muundo wa Muungano utaona kabisa, kuwa Jamhuri ya Muungano itagharamiwa na raia hawa hawa wa nchi Mbili, pia wananchi hawa hawa watagharamia serikali za nchi zao.
Kwa muundo wa Serikali mbili Raia wa Tanganyika amebeba jukumu la kuendesha Muungano kwa Gharama.

Raia wa Zanzibar hawana gharama za kuendesha Muungano. Unaposema Raia wa nchi mbili si kweli.

Ikiwa ni kweli unachosema , tuonyeshe Zanzibar inachangia nini katika muundo wa sasa wa Muungano

Kwasasa ndivyo ilivyo, kwamba kila cha JMT kunahusu Tanganyika kwasababu Zanzibar wana Serikali yao.

Waziri Mkuu wa Tanzania si ndiye 'Rais wa Tanganyika kwasasa'. Tena ana Naibu Waziri mkuu mbona huoni hiyo ni gharama. Zanzibar wana admistrative structure yao. Hivyo hakuna kinachoongezeka hata senti tano.

Nitajie Taasisi moja ya Umma hata ulinzi na Usalama ambayo haina mbadala Zanzibar. Moja tu!
Rasimu imeorodhesha mambo 7 tu., nimeyaweka. Nionyeshe jambo moja tu ambalo Zanzibar watalalamika

Mambo 7 hayana gharama kwasababu hata sasa yapo na gharama zitabebwa na Tanganyika na hata sasa yanabebwa na Tanganyika. Zanzibar wanalalamika nini?

Orodhesha jambo moja unalodhani litakuwa kero, moja tu
Yaani itakuwa ni vurugu badala ya Malalamiko, maana Kuna mambo mengi ambayo yana mkanganyiko hayako wazi ambayo yataleta mgongano!
Yaorodheshe hapa usiseme kwa ujumla. Taja moja tu at minimum
Yes na kuna Wabunge 50/20 plus 5 kutoka kila upande. Hata sasa hivi kinachoitwa Tume ya kumaliza kero ndiyo itakayokuwa sekretariet. Rejea rasimu 117(1) madaraka ya kutunga sheria
Kuna Sekretariati ya kuratibu mambo ya nchi Washirika. Kuna sheria zimeanishwa katika rasimu zitakazokuwa chini ya Bunge la JMT. Kuna madaraka ya Rais wa JMT na yameanishwa. n.k.
Na katika kuweka sawa utata huu utakapojitokeza huko mbeleni gharama zote atabebeshwa raia hawa hawa wa nchi hizi mbili kwa kuunda matume na task forces!!!
Unaposema Raia wa nchi mbili unapotosha. Hakuna , narudia tena HAKUNA Raia wa Zanzibar anayebeba gharama hata senti tano ya kuendesha Muungano. Kwasasa gharama zote zinabebwa na Tanganyika 100%

Narudia tena, tuonyeshe mchango wa Raia wa Zanzibar kwa muundo wa sasa kabla ya Serikali 3.
Hakuna kipengele kinachoongeza gharama ndiyo maana hujaweza kutaja idara, taasisi, Wizara itakayoongeza gharma. Tukijadili hili nina uwezo wa kukuonyesha kwamba hakuna hata senti tano itakayoongezeka

Kinachotokea kwa serikali 3 ni kupunguza gharama kwa Tanganyika.

Kwamba Zanzibar itawajibika kwa mambo yake na Raia wake na Tanganyika pia.
Kwasasa Tanganyika imejibeba na kubeba mzigo wa ziada wa Zanzibar isiyo na mchangi wowote kiuchumi

Suala la gharama za Serikali 3 linapotoshwa kwasababu kuna mambo mengi tunajifanya hatuyaoni

1. Mafao ya viongozi Wastaafu kuanzia Marais, Makamu wa Rais na Mawaziri Wakuu na ma- Spika wa Bunge ambazo ni kubwa sana na analipia Raia wa Tanganyika. Mbona hatuoni hili

Gharama za malipo ya Wastaafu hawa kwa mwaka ni kubwa kuliko gharama za Wizara ndogo ya JMT

2. Tunawezaje kupata pesa za kulipa Wake wa wastaafu halafu tunadai serikali 3 inagharma . Yaani tunalipa wanandoa lakini hatuoni hizi ni gharama. Kuna Wake wa Wastaafu wangapi.

3. Tunapoteza pesa (CAG) kwa matrilioni hatuoni kama ni gharama anazobeba Raia

Kusema serikali 3 ina gharama si KWELI, kwa muundo wa sasa bado tuna serikali 3 zilizojificha ndani ya 2.
Serikali ya JMT ni ya Tanganyika pamoja na ya Muungano halafu tuna SMZ.
Kuzitengenisha kutasaidia kupunguza gharama kwa Tanganyika arguably Zanzibar itabaidi walipe gharama

Kwanini watu wanaogopa serikali 3? Ni kwamba itafunua utegemezi wa Zanzibar. Itaondoa free ride ya Zanzibar katika ku abuse Muungano kwa jina la JMT.

Jibu la Kweli ni Kura ya maoni kwa Zanzibar, wakitaka tuwe na 3 ili wawajibike, wakikataa njia nyeupe

Mwisho, naomba unishawishi kwanini na kwa faida gani Mtanganyika anahitaji Muungano na kubebea gharama kubwa peke yake.
 
Mwisho, naomba unishawishi kwanini na kwa faida gani Mtanganyika anahitaji Muungano na kubebea gharama kubwa peke yake.
Asante sana, Mkuu. Na kwa kweli mwenye masikio na asikie.

Nitachelewa kidogo kuja kujibu hoja zako lengo kuwapa wasomaji wa uzi huu kutafakari kwa kina hoja ulizoweka hapa jukwaani nao watoe maoni.

Kwa mara nyingine nakushukuru sana.
 
Dah? Kwasasa mkono umekuwa mrefu acha wajikune sehem zilizokuwa zinawasha!
 
😆😆😆 Mke tena?
 
Brother Pascal Mayalla kama Zanzibar ni mke kwa Tanganyika na Simiyu ni miongoni mwa watoto, hivi ndoa ikija kuvunjika kwa mke huyu huyu mume atakuwa na faida?
Kwa sababu mke aliyeolewa anapewa maendeleo akiwa kwao wala si kwenye himaya ya mume, ndoa ikivunjika mume si itakuwa imekula kwake gharama zoooote alizotumia kwa mke huyu Zanzibar?
 
Mkuu Nguruvi3 kwamba mapato ya Zanzibar bilioni 200 ni kwa mwaka au?
 
Mkuu Nguruvi3 kwamba mapato ya Zanzibar bilioni 200 ni kwa mwaka au?
Kiasi hicho si halisia ni kikubwa sana ukilinganisha na uhalisi. Kilikuwa kwa ''mjadala'' Uhalisia ni huu hapa

Kwa taarifa ya ZRA ya 02 April 2023, kaika kipindi cha miezi 9 (July 2022- March 2023) mamlaka ilikusanya 449 Bilioni chini ya lengo la 460 Bilioni. Yaani makusanyo yalikuwa Tsh 54 Bilioni kwa mwezi

Tufanye kwamba kiasi cha 54 Bilioni kitaongezeka na kuwa Bilioni 80 kwasababu zozote zile.
Kwa mwaka ni sawa na Bilioni 960. Hiyo ni baada ya ku-inflate figure. Bajeti halisi ni hii hapa chini

Bajeti ya Zanzibar kwa mujibu wa Waziri wa fedha wa Zanzibar, ni Tsh 2.8 Trilioni. Kati ya hizo 1.3T ni matumizi ya kawaida na 1.5 ni kwa maendeleo. Matumizi ya kawaida ni kulipa mishahara ambapo hakuna gharama za ulinzi na usalama, mambo ya ndani, nje, Wizara za Muungano na taasisi zake. Hizo ni kwa mambo ya SMZ

Kwa maneno mengine hata kama watakusanya 1 Trilioni, bado kuna upungufu wa 1.8 Trilioni.
Hizi wanazipata kutoka wapi?

Usisahau kuwa kuna 4.5% wanapaa kutoka Tanganyika kila mwezi.
Ikiwa Tanganyika watakusanya 1 Trilioni kwa mwezi Zanzibar wanapata Bilioni 40 karibia sawa na makusanyo yao.

Pia kumbuka, Bajeti ya 2.8T inakaribiana na Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Usalama ambayo ni 2.T

Kituko ni pale wanataka kuwe na account ya pamoja ya fedha. Rais Mwinyi kawaambia ukweli Desemba 11 2022 kwamba account ya pamoja itabidi Ichangiwe na Zanzibar pia. Sasa wana kipi cha kuchangia ?
 
Kuna tatizo jingine, Zanzibar ni wamoja kukiwa na Tanganyika. Wakiwa wenyewe kuna wanaoamini mapinduzi ni haramu na hutawasikia hata wakitamka. Kundi hili linaamini katika Zanzibar ya nyakati hizo na lina 'theory' kwamba mapinduzi yameletwa na Tanganyika

Kuna Mapinduzi daima, wanaamini katika mapinduzi , hawa wapo tayari kwa Serikali moja na ndio hasa wanaotaka Serikali mbili kwa hofu kwamba Usultan utarudi. Unamkumbuka Mbunge Kassim alisema nini Bungeni? Serikali moja haiwezekani! na kwangu mimi ni wazo baya sana kuliko kuunja Muungano
Nguruvi3 ni kweli usemayo, Watu Waunguja wanaupenda muungano kuliko watu wa Pemba.
Ikubaliwe kura ya maoni wanaotaka muungano au hawautaki, kama wameshinda wenye kuukataa njia nyeupe, Kisiwa cha Unguja kama watataka kuendelea na muungano kuwe sasa na makubaliano mapya, ya serikali moja au tatu.
Na hivi gharama za kuihudumia Zanzibar na gharama za kulinda mipaka ya baharini ipi gharama kubwa?? Nguruvi3 , Brother Pascal Mayalla
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…