Hoja ya Serikali tatu kuwa na gharama ni hisia za watu wasiotaka Serikali 3 kwa kupotosha Umma
Nimekuuliza na bandiko hapo chini hujaweza kuanisha kwa uyakinifu wapi gharama zitaongezeka.
Kwamba gharama zinazongezeka kwa Raia wa nchi mbili si kweli.
Kwasasa gharama amezibeba Raia wa Tanganyika pekee kwa jina la JMT
Kwa mfano, kuna Wabunge 393 akiwemo AG. Kati yao, 80+ wanatoka Zanzibar gharama zao zinabebwa na Tanganyika kwa jina la JMT ikiwemo kuwapa fedha za Tanganyika kwa mfuko wa jimbo wa Zanzibar!
Pesa za mfuko wa jimbo ni za Tanganyika kwa jina la JMT
Rasimu ya Warioba inasema kutakuwa na Wabunge 50 kutoka Tanganyika na 20 kutoka Zanzibar na Rais atateuwa 5 kutoka kundi la Walemavu kwa jumla ya 75 ( Rasimu ya Warioba Sura ya Tisa 113 (a )(b)
Idadi ya Wabunge 75 ni ndogo sana ukilinganisha na Wabunge 80 pekee kutoka Zanzibar leo hii.
Gharama za Bunge la serikali 3 ni kidogo zaidi kuliko gharama za Wabunge 80 wa JMT kwa sasa.
Watu hawaoni gharama hizi kwasababu zinalipwa na Tanganyika kutoka Hazina.
Pili, nchi Washirika zitaamua idadi ya Wabunge kutokana na Uchumi.. Kwa mfano, Baraza la Wawakilishi lina Wajumbe 50, la kushangaza Wabunge wa JMT kutoka Zanzibar ni 80+.
Ikiwa utaiambia SMZ kulipia Wabunge 80 haitakubali kwasababu BLW linalipia 50, kwavile wanalipiwa na Tanganyika hata wakija 300 hakuna anayejali kwasababu gharama kazibeba Mtanganyika.
Niambie gharama zitaongezeka wapi ?
Nije kwenye hoja zako
Katika rasimu hiyo, hasa SURA YA SITA inayooelezea muundo wa Muungano utaona kabisa, kuwa Jamhuri ya Muungano itagharamiwa na raia hawa hawa wa nchi Mbili, pia wananchi hawa hawa watagharamia serikali za nchi zao.
Kwa muundo wa Serikali mbili Raia wa Tanganyika amebeba jukumu la kuendesha Muungano kwa Gharama.
Raia wa Zanzibar hawana gharama za kuendesha Muungano. Unaposema Raia wa nchi mbili si kweli.
Ikiwa ni kweli unachosema , tuonyeshe Zanzibar inachangia nini katika muundo wa sasa wa Muungano
Tena katika sura hii, raia hawa hawa watalazimika kutengeneza katiba mpya nyingine za nchi zao!!! Kwa hiyo, kwenye katiba Yao watakuwa na "Rais wao" atakayelipwa mshahara na masulufu mengine na raia hawa hawa! Kifupi, raia hawa hawa watawalipa mshahara Marais wa wawili. Huo ni mfano mmoja tu wa kuongeza gharama (watanganyika wameishazoea hili nadhani)!
Kwasasa ndivyo ilivyo, kwamba kila cha JMT kunahusu Tanganyika kwasababu Zanzibar wana Serikali yao.
Waziri Mkuu wa Tanzania si ndiye 'Rais wa Tanganyika kwasasa'. Tena ana Naibu Waziri mkuu mbona huoni hiyo ni gharama. Zanzibar wana admistrative structure yao. Hivyo hakuna kinachoongezeka hata senti tano.
Nitajie Taasisi moja ya Umma hata ulinzi na Usalama ambayo haina mbadala Zanzibar. Moja tu!
Pia kuhusu, Serikali Tatu kuongeza kero za Muungano (ambazo unasema ni Bora tuziite Malalamiko ya Muungano). Hili linajionyesha wazi kwenye sura hii ya SITA ya rasimu ya katiba mpya, sura ya SABA na kipengele cha Mambo ya Muungano (tafadhali yasome Tena uone kama kweli Yale yanaondoa malalamiko kwa Wazanzibari) yaliyotajwa ibara ya 63 na kuambatanishwa mwishoni mwa rasimu hiyo ya katiba mpya.
Rasimu imeorodhesha mambo 7 tu., nimeyaweka. Nionyeshe jambo moja tu ambalo Zanzibar watalalamika
Mambo 7 hayana gharama kwasababu hata sasa yapo na gharama zitabebwa na Tanganyika na hata sasa yanabebwa na Tanganyika. Zanzibar wanalalamika nini?
Orodhesha jambo moja unalodhani litakuwa kero, moja tu
Yaani itakuwa ni vurugu badala ya Malalamiko, maana Kuna mambo mengi ambayo yana mkanganyiko hayako wazi ambayo yataleta mgongano!
Yaorodheshe hapa usiseme kwa ujumla. Taja moja tu at minimum
Mfano, ni Ibara ya 65 na ibara ndogo zake nne ambayo inahusu mahusiano ya Nchi mshirika wa Muungano na jumuiya za kikanda na kadhalika. Yaani ibara ndogo ya nne ya ibara hii ya 65 inaelekeza Bunge ndilo litatunga Sheria ya namna Bora ya utekelezaji wa Ibara hii.
Yes na kuna Wabunge 50/20 plus 5 kutoka kila upande. Hata sasa hivi kinachoitwa Tume ya kumaliza kero ndiyo itakayokuwa sekretariet. Rejea rasimu 117(1) madaraka ya kutunga sheria
Sasa kama nchi mshirika kupitia Bunge lake ( maana watatunga katiba Yao na watakuwa na Bunge lao) itakuja na sheria tata kuhusu jambo hili itakuwaje! Maana ibara ndogo ya 3 ya ibara hii ya 65 inasema mshirika "anaweza" (siyo lazima) kumshirikisha Serikali ya Muungano juu ya Nia yake yakuwa na mshirika wa kikanda nakadhalika!!!!
Kuna Sekretariati ya kuratibu mambo ya nchi Washirika. Kuna sheria zimeanishwa katika rasimu zitakazokuwa chini ya Bunge la JMT. Kuna madaraka ya Rais wa JMT na yameanishwa. n.k.
Na katika kuweka sawa utata huu utakapojitokeza huko mbeleni gharama zote atabebeshwa raia hawa hawa wa nchi hizi mbili kwa kuunda matume na task forces!!!
Unaposema Raia wa nchi mbili unapotosha. Hakuna , narudia tena HAKUNA Raia wa Zanzibar anayebeba gharama hata senti tano ya kuendesha Muungano. Kwasasa gharama zote zinabebwa na Tanganyika 100%
Narudia tena, tuonyeshe mchango wa Raia wa Zanzibar kwa muundo wa sasa kabla ya Serikali 3.
Vipo vipengele vingi kwa kweli katika muundo wa Muungano wa serikali Tatu mbali na kuongeza gharama kwa raia lakini pia vitasababisha kero/malalamiko ya Muungano kuwa vurugu na kuhatarisha Amani na tengamano wa Raia. Tuepuke Muundo wa serikali Tatu.Mkuu, nadhani nimejitahidi kujibu swali lako! Asubuhi njema.
Hakuna kipengele kinachoongeza gharama ndiyo maana hujaweza kutaja idara, taasisi, Wizara itakayoongeza gharma. Tukijadili hili nina uwezo wa kukuonyesha kwamba hakuna hata senti tano itakayoongezeka
Kinachotokea kwa serikali 3 ni kupunguza gharama kwa Tanganyika.
Kwamba Zanzibar itawajibika kwa mambo yake na Raia wake na Tanganyika pia.
Kwasasa Tanganyika imejibeba na kubeba mzigo wa ziada wa Zanzibar isiyo na mchangi wowote kiuchumi
Suala la gharama za Serikali 3 linapotoshwa kwasababu kuna mambo mengi tunajifanya hatuyaoni
1. Mafao ya viongozi Wastaafu kuanzia Marais, Makamu wa Rais na Mawaziri Wakuu na ma- Spika wa Bunge ambazo ni kubwa sana na analipia Raia wa Tanganyika. Mbona hatuoni hili
Gharama za malipo ya Wastaafu hawa kwa mwaka ni kubwa kuliko gharama za Wizara ndogo ya JMT
2. Tunawezaje kupata pesa za kulipa Wake wa wastaafu halafu tunadai serikali 3 inagharma . Yaani tunalipa wanandoa lakini hatuoni hizi ni gharama. Kuna Wake wa Wastaafu wangapi.
3. Tunapoteza pesa (CAG) kwa matrilioni hatuoni kama ni gharama anazobeba Raia
Kusema serikali 3 ina gharama si KWELI, kwa muundo wa sasa bado tuna serikali 3 zilizojificha ndani ya 2.
Serikali ya JMT ni ya Tanganyika pamoja na ya Muungano halafu tuna SMZ.
Kuzitengenisha kutasaidia kupunguza gharama kwa Tanganyika arguably Zanzibar itabaidi walipe gharama
Kwanini watu wanaogopa serikali 3? Ni kwamba itafunua utegemezi wa Zanzibar. Itaondoa free ride ya Zanzibar katika ku abuse Muungano kwa jina la JMT.
Jibu la Kweli ni Kura ya maoni kwa Zanzibar, wakitaka tuwe na 3 ili wawajibike, wakikataa njia nyeupe
Mwisho, naomba unishawishi kwanini na kwa faida gani Mtanganyika anahitaji Muungano na kubebea gharama kubwa peke yake.