Nyie hii dunia muione hivi. Nikiwaza kuna wakati nawaza mengi maana mimi nasoma sana riwaya.
Nasisitiza hii ni riwaya. Nilivyosoma ile riwaya na mimi nikajikuta navaa uhusika yaani kama vile naota ndoto.yaani nilikuwa naota kupitia kwenye ile riwaya
Kwamba wakati late CEO wakati anausaka u CEO mr new culture aliona customers wale vijana wake ambao wako chini yake wale wapiga kelele wanaojita mabrigedia bila elimu,aliona hawamfai.
Akaamua kutengeneza team ya mutu kama 90 hivi, iliitwa team " wherever you're we are there".
Kazi yake ilikuwa ni moja. Kushika stil waya na kusugua masufuri yatakate haswa!! hii yote ni kimsafisha mr bright. kumbuka kwenye hiyo ndoto na mimi nilikuwa kwenye hiyo team.
So hiyo team ya wenye elimu ya kuweza kueleza uwezo na uzuri wa mr bright ilibidi itembee mguu kwa mgu, nyumba kwa nyumba.
Maskini kwakuwa na mimi nina ka elimu basi nikifika kwenye kaya hapo nimeambatana na vijana kama watano hivi wale wapiga kelele wasiokuwa na elimu, basi mimi ndo naananza kujieleza.
Kwenye kujieleza lazima uwe umesoma vizuri ile ripot ya mr bright kuachia ngazi. Kwa kifupi sisi wenye ka elimu ile ripoti tuliimeza so ukifika kwenye kaya ambako kuna wasomi walikkuwa wakituhoji, ilikuwaje mr new culture akampokea mr bright?
Basi nashusha nondooooo, na vipeperushi kibao tunahamia nyumba nyingine. Jamani kumbukeni hapa nilikuwa naota.
Basi wakuu tulizunguka hii branch yenye matawi zaidi ya 2o mguu kwa mguu nyumba kwa nyuma hii yote ni kusugua na stil waya kutu za mr bright.
Kinachoniuma ilikuwaje na mimi nikajikuta kwenye hiyo team ta kusugua kutu? Wakuu nikiwaza sasa hivi najikuta nacheka, hivi huyu mr new culture anatuonaje sisi mpaka atutumie kama dodoki? Nasikitika sana kwa nini sikujua huu upuuzi
Nakumbuka kwenye ile ndoto tulikuwa na wimbo ketu,......... mr bright, mr bright , ana ka mtima keupe, ana ka ngozi ka mtume, na kichwani kwake kuna mchele mweupe, tiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiriiiiiiiiiiiiiiiiiiiii lazima alale kwenye hekaru nyeupe.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Jamami jamani nyie hawa wapuuzi walijuwa kutuchezea.
Lakini kitu nilichojifunza kwenye ile ripot ya kuachia ngazi kabisa mr bright hakuwa na hatia so wakati tunamsugua na stil waya huko kwenye matawi tulikuwa sahihi.
Kilichoniuma ni mimi kujikuta chini ya mpuuzi mmoja mr culture .lakini hata hivyo kwenda kule kulinisaidia kujua upuuzi wanaoufanya akina, kijana msema sana na mr new culture.
Kingine nilichoona kwenye ile ndoto, kijana msema sana, aliyekuwa kapoteza daftari lake hivi karibuni, hakupenda mr new culture ampokee mr bright kwa wakati ule. Alikubali shingo upande. Mambo yaliisha aliye pata u CEO akapata maisha yakaendelea.
Lakini baada ya mwaka moja kijana msema sana akanasa kwa mr born in town. Je wewe ungekuwa late CEO mzalendo unaona wateja wa kampuni wakichezewa na mr born in town, mr new culture, na kijana msema sana je ungekaa kimya?
Kwakweli hata mimi ningemfundisha adabu.kwa kufatia rules za uongozi zilivyo ngumu. Baada ya kuota haya yote nikastuka usingizini.