Jazia nyama mkuu kwahuyo kamanda aliyestaafu na baadhi ya op huko porini
Sent from my CPH1923 using
JamiiForums mobile app
Vitu vingine naogopa kuongea sana nisije nikavuka mstari mwekundu maana dah ulimi uliponza kichwa.
Kuna kamanda amestaafu anaitwa sabuni Toffy ile ya kufulia nguo ,hiyo hiyo mkuu [emoji846]
Huko bwana kuna kipindi kulikuwa na ujambazi sana magari kutekwa tekwa hovyo, askari wananyang'anywa hadi bunduki halafu zinatumika kutupiga sisi wenyewe.
Ukifuatilia unakuta ni watu wanavuka mipaka wanaingia kutoka nje na wanafanya yao,yaani hiyo njia kama mnaianza kuna kibao kinasema "sasa unaanza kuingia pori la..."Kama mlikuwa mnapiga story kila mmoja kimyaaaaa, unawaza sijui nitamaliza salama?
Roho mkononi mwenye kuomba anaanza, tasibihi mkononi, Rozary, wa njia ya msalaba ilimradi kila mmoja anamlilia muumba wake.
Walivyozidi ikabidi wampeleke huyo Kamanda kufanya utalii kwenye mapori yote, yeye mwanzo hakuwa anaenda front anawatuma tu vijana wake.Wakienda na kurudi hawaji na majibu ya uhakika sana maana baada ya muda unasikia tena wapuuzi wameanza tena.(wameteka) na kuua.
Akaona huu ujinga, akaita vijana wake kadhaa akasema kuanzia sasa mimi sikai ofsini tunaenda wote, vijana wanashangaa boss uko serious? Akawaambia twendeni na msiseme tunaenda wapi.
Kabla hawajafika zikaanza kulia,nao wakajibu ila upande wa maharamia ukaonekan una nguvu zaidi. Akaita Landrover kwa simu ya upepo kutoka makao makuu ya mkoa, ikaja iko loaded.
Mkuu tumefika, akawaambia nipishe niwaonyeshe, yeye mwenyewe akapanda juu weeeh, unaambiwa hadi kuku walikuta ni manyoya tu. Salamu zikapelekwa kwa wengine kwamba tulichofanyiwa si kwa akili hizi za hawa jirani zetu tulivyodhani wako, sivyo kumbe, adabu.
Akaendelea kuwajengea uwezo hadi sasa ukisikia ni kwamba aidha wamekufa wakijaribu au walikimbia kuko shwari. Kumbuka huyu alipelekwa huko na born town. Sasa hapa mtu atasemaje jeshi la Polisi ni dhaifu, hatuyajui mengi wanayoyafanya.
Jamani makamanda nimeamua kuongelea mazuri yenu ambayo wananchi hawayajui ndio maana wakati mwingine wanaleta dharau, ila kama mtaona naenda kinyume tafadhali niambieni nifunge kinywa changu.
Nimeongea kwa kifupi sana hilo tukio maana nilisimuliwa ila ni la kweli siku hizi kuko shwari, so Mr born town hawaachi kumlaum na kumlaani kule aliweka intelijensia kali ambayo ilitibua mambo yao mengi.
Utasikia Chi...mbaya sana,hovyo sana, wengi hawawezi kutamka herufi ya jina lake la kwanza.