Umeongea ukweli.Mtu unamkuta eti Afisa misitu wakati kwake hana mti hata mmoja atajua umuhimu wa miti kweli huyu na kuitunza kwa upendo?
Viongozi wengi ni wachafu nenda ofisini kwake unakuta limeza lichafu, kuta zmechakaa, paa la nyumba limeachama, vioo vya madirisha vimepasuka ameweka kipazia uijue rangi yake mpaka upime DNA,kuta zina nyufa na ni mazalia ya popo, mitaro maji yamekuwa ya kijani lakini yeye yupo tu na kitambi chake anakula chapati na supu ya upupu eti sorry niko na majukumu ya taifa.
Unajiuliza wewe uliyefuata huduma hapo ninaweza kusubiri kwa muda gani mpaka amalize kabla sijatapika (samahani linaleta kinyaa) nisepe zangu niondokane na kadhia hii, yeye yupo miaka yote hapo. Siyo kwamba hana bajeti utakuta inatengwa lakini inapigwa. Na huyu ni mfanyakazi wa NHC,Wakala wa majengo n.k
Siyo wote lakini wengine wanajitahidi sana kama watu wa Afya(Hospitals, dispensary,),TAMISEMI mjirekebishe.