Kuna habari kuwa mwenda zake alikuwa amesha set kuwa katika uongozi wake ataunganisha serikali mbili na kuwa moja, na Zanzibar ikiunganisha visiwa vya pemba, unguja na mafia itakuwa mkoa mmoja wenye wilaya 4, moja pemba, unguja wilaya mbili na ya nne mafia.
Hizi habari, amewahi kuzisema Maalim, tena hadharan. Akasema atapambana kwa hali na Mali kuhakikisha hilo halitokei,
Lakin pia habari za ndan zinasema move ilikuwa kumchukua rais wa Zanzibar kumfanya kuwa ndie mgombea urais wa 2025 ili kuwatuliza Wazanzibar. Bahati mbaya hatuko nae. Mungu ailaze roho yake mahali pema pepon.
Habari za ndan zinasema Leo lilikuwa kui neutralize kabisa, mipango ilikuwa tayar, kuhakikisha wafanyakazi wote wa serikali za miji ya zanzibar kuletwa Tanganyika na kule kupelekwa watanganyika. Wanafunzi wengi kuletwa bara na wa bara kupelekwa kule.
Bahat mbaya mwamba wa kufanya mambo makubwa hayupo.
Ni wazi kuwa aliyetunyang'anya JPM mapema alitukatili sana. Alitunyima mabadiliko makubwa sana.
Wazo la kuwa na serikali moja Nyerere alikuwa nalo na alisema ' Kuunda nchi moja kutaifanya Tanganyika ionekane imeimeza Zanzibar'' akiwa na maana imepoteza 'utaifa' kwasababu Tanganyika ni kubwa.
Wazo la Mwalimu lilikuwa kuchukua muda ili kutengeneza serikali ya pamoja ''Blending'
Alianza na kuunganisha vyama, halafu akaongeza mambo ya Muungano kidogo kidogo ili kufikia mahali tunakuwa nchi moja. Mkataba wa Muungano wa 1964 ulikuwa na mambo 11 , yakaongezeka hadi kufikia 22 na Wazanzibar wanasema zaidi ya 33 ukiyamnyumbulisha
Kuongezwa kwa mambo ya Muungano kuliinufaisha Zanzibar kuliko Tanganyika. Kwa mfano, Elimu ya Juu haikuwa jambo la Muungano lakini kupitia mambo 22 Wazanzibar wamenufaika sana na elimua ya Juu, Kati na hata ya sekondari hadi leo n.k. Mfano, kuna nafasi zaidi ya 1000 za mikopo ya elimu ya juu (HESLB) mahsusi kwa Zanzibar.
HESLB ni mfuko wa Tanganyika , Zanzibar wana ZHESLB. Kwa idadi ya watu milioni 1.5 hizo ni nafasi nyingi sana.
'Chukua idadi ya watu ya Mkoa wowote halafu angalia wanafunzi wangapi wanapata HESLB ukilinganisha na Zanzibar.
Zama za nyuma kabla ya mikopo, Wazanzibar walisoma Katika vyuo vya Tanganyika Bure. Angalia Safu yote ya viongozi wa Zanzibar waliopita na Waliopo, ni zao la vyuo vya Tanganyika wakiwemo wanaopinga Muungano.
Orodha ni ndefu , inatosha tu kwa mfano huo
Kwa hali ilivyo Serikali moja italeta matatizo makubwa kama yale ya UK na Scotland, Eritrea na Ethiopia, Timor Mashariki na Indonesia, Oganden na Somali, Biafra na Nigeria , Quebec na Canada, Puerto Rico na USA, Taiwani na China n.k
Kuna mambo yanayoweza kushindwa kwa kupigwa mabomu lakini Utaifa na Imani haviwezakani kabisa
Hata Mwalimu Nyerere Mwaka 1967? alisema '' Kama Zanzibar hawataki Muungano hatawapiga mabomu''
Kuna ushahidi mambo yanapofanyika kwa nia njema na uwazi hupunguza au kuondoa matatizo ya nchi zilizoungana. Mfano, Scotland walipewa kura ya maoni ikiwa wanabaki UK au wanajitoa. Kura ikasema wabaki na tangu wakati huo wenye hoja ya kuondoka wanatatizo kubwa kuihuisha
Quebec ilipewa kura ya maoni na iliamua kubaki ndani ya Canada tena kura ya maoni mara mbili.
Tangu wakati huo hoja imekuwa ngumu sana kuuibua tena.
Timor walipewa kura kama Eritrea na waliamua kuondoka na sasa wanaishi na majirani zao kwa amani.
Ni kwa muktadha huo kuna hoja kwamba Muungano haulindwi kwa bunduki au deraya za kijeshi.
muungano ni makubaliano ya pande husika. Katika Muungano mdogo hupewa haki ya kuamua, na hapa kwetu ni Zanzibar. Hivyo Zanzibar wapewe kura ya maoni kuamua ikiwa wanataka Muungano au la.
Bila kutengua kitendawili hicho hakuna muundo wa serikali wa aina yoyote utakaotoa jibu la tatizo.