Dark days 17/03/20...

Dark days 17/03/20...

Katika mjadala huu kuna wanaoamini kwamba muundo wa sasa wa Muungano ni mzuri bila kutueleza ni kwanini.
Tuangaze haraka tu kwa baadhi ya mambo yanayochanganya.

Kuna Waziri Mkuu wa JMT anayependekezwa na Rais na kuthibitishwa na Bunge la JMT. Ndani ya Bunge kuna Wabunge wa kuteuliwa na Rais kutoka Zanzibar, Wabunge 5 kutoka Baraza la Wawakilishi na Wabunge takribani 70 wa kuchaguliwa.

Waziri Mkuu wa Tanzania anayechaguliwa na Wabunge wa pande zote hana mamlaka katika jambo lolote linalohusu Zanzibar. Kwa mantiki , huyu ni Waziri Mkuu wa Tanganyika ingawa anachaguliwa na Wazanzibar pia. Kituko # 1

Katiba ya 1977 inasema ikiwa Rais au Makamu wa Rais hawapo , Waziri mkuu wa JMT atendesha kikao cha Baraza la Mawaziri (Cabinet). Ndani ya Baraza la Mawaziri yupo Rais wa Zanzibar kama Mjumbe. Kikao hicho kikiendelea Mkuu atakuwa Waziri Mkuu wa JMT, si Rais wa Zanzibar . Kituko #2

Rais SSH ameamuru kujengwe Ofisi ya Waziri mkuu wa JMT na Makamu wa Rais wa JMT Zanzibar.
Waziri mkuu hana mamlaka Zanzibar, Ofisi ya nini ? Makamu wa Rais ni mfungua makongamano hana mamlaka Zanzibar Ofisi ya nini. Ofisi hizo zimejengwa kwa kodi za Tanganyika! Kituko# 3

Wabunge wa Zanzibar ndani ya Bunge la JMT wapo katika kamati za kisekta zinazohusu mambo ya Tanganyika.
Utawaona wakishiriki ukaguzi wa shughuli za Utalii, Tamisemi, Kilimo na ufugaji, elimu, Afya, n.k. mambo yasiyo ya Muungano. Hutaona Wabunge wa JMT katika kamati za kisekta wakienda kukagua shughuli Zanzibar! Kituko#4

Zanzibar wanakusanya pesa za 'VISA' za watalii na kubaki huko. Wafanyakazi waUhamiaji wameajiriwa na Serikali ya JMT ambayo mapato yake ni ya Tanganyika. Kwamba, Tanganyika ina gharama za Mishahara ya Wafanyakazi wa Uhamiaji Zanzibar ili wakusanye mapato ya SMZ! Kituko # 5

Bidhaa yenye idhini kutoka shirika la Viwango Tanzania (TBS) haiwezi kutumika Zanzibar hadi iidhinishe na Shirika la Viwango Zanzibar (ZBS). Bidhaa yenye kuidhinishwa na ZBS inaingia Tanganyika na kutumika bila idhini ya TBS. Kituko# 6

Orodha ni ndefu sana, inaendelea. Karibuni mtetee hoja
Nguruvi3 una ufahamu mkubwa sana juu ya mambo ya muungano,
Natamani hoja zako hizi juu ya muungano watanzania wengi wazisikie na kuzijua
 
Kwa wakati huo lakini si usalama wa Tanganyika tu bali pia usalama wa Zanzibar kama tutakavyoona baadaye

Si kweli kwasababu adui huyo angetumia Rwanda, Burundi , Malawai n.k. Kumbuka Tanganyika ina mipaka na nchi 8

Hapana! unakosa point, ni kinyume chake. Kwamba Karume alikuwa under pressure ya Umma Party ya Abraham Babu. Kuna wakati Tanganyika ilibidi ipeleke askari 300 na Karume alipoleta jeuri Nyerere akatishia kuondoa majeshi.
Hii ni kwa ufupi , ni kisa kikubwa lakini elewa kwamba aliyeomba Muungano ni Karume '' Wewe ni Rais mimi ni Makamu' alisema Karume

Kwanini Serikali 3 haiwezekani? Hapa ndipo tunahitaji utusaidie. Kwanini Muundo wa sasa unaosema ni suluhisho bado una matatizo tunayoyaon!
mkuu Rwanda Burundi sijui Kongo ni land country hazina uwiano wa kiusalama kabisa kama unabisha Kwa nini usa, urusi UK na nchi zingine kubwa Huwa wanataka kutawala visiwa hivi vilivyiko baharini? hiv unajua visiwa vya shelisheli mautania ni vya kimkakakati? Kwa ajiri ya usalama wa nchi zao?

sass jiulize nchi ziko mbali y zihitaji hivyo visiwa? ndicho mwl alichokitaka, mwal hakuwa kama mm au ww ambae alitegemea . com kupata information, na ndyo mataifa makubwa yanavyo fanya hayategemei . com ila . com inarahisisha tu kupata information amka mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika mjadala huu kuna wanaoamini kwamba muundo wa sasa wa Muungano ni mzuri bila kutueleza ni kwanini.
Tuangaze haraka tu kwa baadhi ya mambo yanayochanganya.

Kuna Waziri Mkuu wa JMT anayependekezwa na Rais na kuthibitishwa na Bunge la JMT. Ndani ya Bunge kuna Wabunge wa kuteuliwa na Rais kutoka Zanzibar, Wabunge 5 kutoka Baraza la Wawakilishi na Wabunge takribani 70 wa kuchaguliwa.

Waziri Mkuu wa Tanzania anayechaguliwa na Wabunge wa pande zote hana mamlaka katika jambo lolote linalohusu Zanzibar. Kwa mantiki , huyu ni Waziri Mkuu wa Tanganyika ingawa anachaguliwa na Wazanzibar pia. Kituko # 1

Katiba ya 1977 inasema ikiwa Rais au Makamu wa Rais hawapo , Waziri mkuu wa JMT atendesha kikao cha Baraza la Mawaziri (Cabinet). Ndani ya Baraza la Mawaziri yupo Rais wa Zanzibar kama Mjumbe. Kikao hicho kikiendelea Mkuu atakuwa Waziri Mkuu wa JMT, si Rais wa Zanzibar . Kituko #2

Rais SSH ameamuru kujengwe Ofisi ya Waziri mkuu wa JMT na Makamu wa Rais wa JMT Zanzibar.
Waziri mkuu hana mamlaka Zanzibar, Ofisi ya nini ? Makamu wa Rais ni mfungua makongamano hana mamlaka Zanzibar Ofisi ya nini. Ofisi hizo zimejengwa kwa kodi za Tanganyika! Kituko# 3

Wabunge wa Zanzibar ndani ya Bunge la JMT wapo katika kamati za kisekta zinazohusu mambo ya Tanganyika.
Utawaona wakishiriki ukaguzi wa shughuli za Utalii, Tamisemi, Kilimo na ufugaji, elimu, Afya, n.k. mambo yasiyo ya Muungano. Hutaona Wabunge wa JMT katika kamati za kisekta wakienda kukagua shughuli Zanzibar! Kituko#4

Zanzibar wanakusanya pesa za 'VISA' za watalii na kubaki huko. Wafanyakazi waUhamiaji wameajiriwa na Serikali ya JMT ambayo mapato yake ni ya Tanganyika. Kwamba, Tanganyika ina gharama za Mishahara ya Wafanyakazi wa Uhamiaji Zanzibar ili wakusanye mapato ya SMZ! Kituko # 5

Bidhaa yenye idhini kutoka shirika la Viwango Tanzania (TBS) haiwezi kutumika Zanzibar hadi iidhinishe na Shirika la Viwango Zanzibar (ZBS). Bidhaa yenye kuidhinishwa na ZBS inaingia Tanganyika na kutumika bila idhini ya TBS. Kituko# 6

Orodha ni ndefu sana, inaendelea. Karibuni mtetee hoja
mkuu kunamambo unayachanganya hapa nayo ni Muundo wa Muungano na uhalali wake na utendeji/au watendaji wa kiserikali.

kwenye muudo hujazungumzia ngoja niache tuje kwenye utendaje,

ikubalike kuwa jina Tanganyika lilikufa kimuudo na kuzaliwa Tanzania Kwa Tanganyika, Kwa hyo utendaji wa vitambulisho na kazi za watendaji WA Tanganyika(Tanzania) unabaki kuundwa na watanzania ambao kiuhalisia ni watanganyika, Kwa hyo ukimsikia mtu anasema mtanzania Kwa kawaida tu utajua anamaanisha nini

Sasa basi yapo mambo si ya kimuundo yaan hayapo kwenye makubaliano, miongoni mwa hayo ni swala la utendaji wa WM direct humuoni ila indirect inamwona kupitia wizara ambato ambazo nazikuta zipo pote!

pengine uwe na haja nyingine uzingatie TU kuwa ndoa yatu ni ya kipekee huikuti duniani pote,

B

Ndoa yetu ni ya kipekee, huikuti Dunian popote. Ni ndoa ya ajabu, au tuseme ni ndoa ya hofu na mashaka kila wakati.
Lakin hii ndoa inaonekana ni salama kwa sbb hatujapata viongozi wanaojua kunyoosha mstari. Mtu wa kawaida tu, mwenye elimu ya form four akikaa na kuangalia muungano huu, atashangaa na kuwashangaa waasisi,
Huu muungano una kasoro nyingi. Tukiendelea kupata viongozi mbumbumbu kama hawa tulio nao, tujiandae kupata misuko suko huko baadae. Kama Magu angetawala kipindi salama bila janga la corona nadhan ndo tungeshuhudia makubwa kwenye kipindi hiki cha pili kuhusu suala la Muungano..Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuvumilia kuona upuuzi huu wa wabunge wa Zanzibar kushiriki kwenye maamuzi yanayohusu Tanganyika tu, huwezi kuvumilia kuona sheria zilizopitishwa na bunge la Jamhuri ya muungano, haziwezi kutumika Zanzibar mpaka bunge lao liziridhie..

Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuona makusanyo ya visa yanayofanywa na wafanyakazi wa Muungano, yawe ya Zanzibar.

Mambo ni mengi, hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kukubali upuuzi huo. Dunia hii imebadiika sana. Sababu za muungano walizoziona akina Nyerere, hazipo tena. Kuendelea kudhan zipo ni kujidanganya na kukaribisha hali mbaya ijayo.

Miaka ya 90 akina malecela waliamua kuunda serikali ya Tanganyika kwa pressure ya G55 baada ya Zanzibar kujiunga na OIC. Lakin Nyerere alitumia nguvu kubwa kupinga, na kumuondoa Malecela kwenye Uwaziri mkuu. Lakin hoja yake ilikuwa ni serikali tatu means kuvunja muungano, na yeye hawezi kukubali Muungano uvunjike wakat yupo hai, Hili lilitokea kwa wabunge wa 1990, sembuse wa 2025.

Mimi natabiri, kuwa uchaguzi ujao, kama utakuwa huru na haki, tutapata wabunge wengi wa upinzani, na suala la Muungano litaibuka huko, na litakuwa very hot, na kuna uwezekano wa Muungano kuvunjika. Mambo mengi makubwa yatatokea kwenye kpindi cha 2025-2030. Hii ni kama Samia atagombea tena uchaguzi ujao na akashinda.

Massage yangu ni kuwa, hakuna Mtanganyika mwenye akili timamu anaweza kuendelea kunyamazia huu upuuzi wa huu Muungano na hasa wazanzibar.
Tunajua kuwa Magu alikuwa anavunja Serikali ya Zanzibar na kubaki na serikali moja. Na mipango yote ilikuwa imekamilika, utekelezaji ulikuwa ushaanza. Lakin hatunae tena na waliobaki kila mmoja anajidai hajui na hapendi hiyo mipango.

Lakin ki ukweli Mtanganyika mwenye akili timamu hawezi kukubali kuendelea na huu upuuzi wa huu Muungano. Kwa aliyoyafanya Samia, ni either Muungano uvunjike wakat wa utawala wake kama ilivokuwa kwa Mwinyi lakin akaokolewa na Nyerere, au CCM imfie mikononi mwake, yeye awe ndo rais wa mwisho kutoka CCM.
 
mkuu walio na ndoa wanaju Sana hasa wale wakongwe yapo mambo unayakubali kuishi nayo kwenye ndoa japo hupendi ili kuleta matangamano,

ukileta ujuaji Kila kitu kwenye ndoa utajikuta umesababisha mgogoro mkuu ambao utaishia kuvunja ndoa na kuharibu Amani, upo msemo WA kiswahili unasema Amani inapswa kulindwa kwa ghalama yoyote ile maana ukiipoteza Amani kuirudisha itakughalim,

ndicho kinachofanyika Tanganyika, kwa kuwa watanzania(watanganyika) hawana tatzo na ghalama wala huhitaji kutilia shaka juu ya kuilinda Amani,

zanzibar ni nchi ya kimkakati haitakaa kuwa huru ikitoka nje ya tazania il ndani ya tz inuhuru ulio na mipaka, mwenye maamzi wa Nini kifanyike kule ni mtanzania na hawawezi kufanya chochote bila Tanzania,

ipo hotuba ya late president mkapa aliulizwa awali wakati huo na chombo kikubwa Sana cha habari wakati huo late maalim ni maalim kwel kwel kama alokuwa tayari kufanya kazi na chama cha upinzani ikiwa mshindi atatoka huko, alijibu kwa ufupi Sana, na watu hawakumuelewa alisema nanukuu "ngoja tuone" mwisho wa kunukuu

mkuu si unaju nini kilitokea? na sasa Amani tel

B
 
mkuu Rwanda Burundi sijui Kongo ni land country hazina uwiano wa kiusalama kabisa kama unabisha Kwa nini usa, urusi UK na nchi zingine kubwa Huwa wanataka kutawala visiwa hivi vilivyiko baharini? hiv unajua visiwa vya shelisheli mautania ni vya kimkakakati? Kwa ajiri ya usalama wa nchi zao?

sass jiulize nchi ziko mbali y zihitaji hivyo visiwa? ndicho mwl alichokitaka, mwal hakuwa kama mm au ww ambae alitegemea . com kupata information, na ndyo mataifa makubwa yanavyo fanya hayategemei . com ila . com inarahisisha tu kupata information amka mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza elewa kwamba visiwa ni sehemu ya ''tactical movement' ya mataifa makubwa lakini siyo 'absolute'
Kulikuwa na ' cold war ' na hilo linaweza chagiza uwepo wa Muungano , swali, je sababu zile bado zipo?

Ikiwa utasema Zanzibar ni eneo la kimkakati, nimeuliza hapa maswali haya
1. Kuna Marine base kubwa sana ya US pale Mombasa, je, hiyo siyo tishio?
2. Moja ya balozi kubwa sub sahara ni ile ya USA iliyopo Dar es Salaam. Je , hilo si tishio?

Lakini pia dunia ya sasa imebadilika, si ya bunduki na magobore. Dunia ya sasa ni 'intelligence'
Tuliwahi kuzungukwa na Wareno na Makaburu lakini tulipita kipindi hicho salama kwasababu ya intelejensia kali

Wakati wa Rais Bill Clinton, Marekani ilihisi kiwanda cha kutengeneza dawa pale Sudan kilikuwa mali ya Osama
Meli za Marekani katika bahari ya mediterenia zilituma kombora lililosafiri masafa makubwa.
Utashangaa kombora lilipiga kiwanda hicho baada ya mtu wa mwisho kufunga kiwanda.

Hiyo ndiyo kazi ya intelejensia, kwamba, walijua mtu wa mwisho anatoka saa ngapi, kuna wafanyakazi wangapi, kombora linasafiri kwa kasi gani, litatua saa ngapi. Haya hayawezekani kwa intelejensia ya kamari hivyo hata ukiwa na Zanzibar bado utakuwa vulnerable tu kwasbabu dunia ya leo si ya 1905 au 1945 au 1975.
 
mkuu kunamambo unayachanganya hapa nayo ni Muundo wa Muungano na uhalali wake na utendeji/au watendaji wa kiserikali.
Watendaji wa Muungano hutenda kufuatana na Muundo 'structure''. Hakuna shaka muundo na utendaji ni pacha.
kwenye muudo hujazungumzia ngoja niache tuje kwenye utendaje,
Labda uzungumzie ili utusaidie kuelewa. Kama unajua kitu tubadilishane maarifa
ikubalike kuwa jina Tanganyika lilikufa kimuudo na kuzaliwa Tanzania Kwa Tanganyika, Kwa hyo utendaji wa vitambulisho na kazi za watendaji WA Tanganyika(Tanzania) unabaki kuundwa na watanzania ambao kiuhalisia ni watanganyika, Kwa hyo ukimsikia mtu anasema mtanzania Kwa kawaida tu utajua anamaanisha nini
Tanganyika haijakufa. Katiba ya 1977 inasema '..Tanzania bara ni iliyokuwa Jamhuri ua Tanganyika kabla ya Muungano' Tanzania visiwani ni ililyokuwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar kabla ya Muungano.

Tanzania ni uzao wa nchi mbili, hakuna Tanzania bila Zanzibar au Tanganyika.
Kusema Tanganyika ilikufa ni mbinu za Wanasiasa kuficha ukweli na ililenga kujenga Utaifa zaidi.

Halikuwa jambo baya lakini Wazanzibar wanapoukataa Utanzania na kuupenda pale tu wanapotaka mafao na fursa kunalazimisha Watanganyika wadai Utanganyika wao.

Sasa basi yapo mambo si ya kimuundo yaan hayapo kwenye makubaliano, miongoni mwa hayo ni swala la utendaji wa WM direct humuoni ila indirect inamwona kupitia wizara ambato ambazo nazikuta zipo pote!
Katika Muungano lazima kila jambo lianishwe kwa nukta, bila hivyo kuna matatizo yanajitokeza.
Tunachokiona ni matokeo ya Waasisi kutoangalia mbali wakidhani kizazi cha 1960 kitarithisha mambo kirahisi.

Watanganyika hawana tatizo na Muungano, wana tatizo na jinsi ambavyo eneo dogo na watu wachache wana 'abuse' resource kuliko eneo jingine la Muunagano , na eneo hilo halina mchango wowote kwa ustawi wa nchi.

Kwa mfano, Tanzania imeingia mkataba na kampuni za Australia kuchimba madini kwa takribani Trilioni 1.5. Uchimbaji utaendelea, kodi zitaendelea kuchukuliwa. Kwasababu Tanganyika haipo, rasilimali ni za JMT.

Trilioni za Australia ni mali ya Tanganyika na Zanzibar. Kwa uataratibu huo Zanzibar itapewa 4.5% wa pato la Tanganyika ikiwemo fedha za Australia. Kiwango hicho ni kikubwa kuliko pesa zinazopelkwa Ulanga , Karagwe n.k. kunakotoka madini hayo.

Kibaya zaidi ni kwamba Zanzibar wamekataa rasilimali zao zisiwe za JMT kama mafuta, gesi, bandari , Utalii n.k.

Zanzibar yenye eneo dogo na watu wachache sana kulinganisha na mikoa kama Dar, Arusha , mwanza, Mbeya inapewa 4.5% ya Pato la Tanganyika kiasi ambacho ni sawa na makusanyo ya kodi ya SMZ.

Tujiulize ukiacha maeneo yanayotoa madini kutokuwa na mgao kama wa ''4.5%' ni mkoa upi unaopata 4.5% ?

Abuse ya Muungano, kuna WABUNGE wa Zanzibar wanaokuja kwa ajili ya Zanzibar lakini wanalipwa na kodi za Tanganyika na wanapewa pesa za mfuko wa jimbo kutoka Tanganyika .
Majimbo ya Zanzibar hayatembelewi na Mbunge wowote wa JMT akiwemo si sehemu ya Muungano!

'Abuse' nyingine, SMZ inakusanya visa kutoka kwa Wageni kulipa posho Wazee wa Zanzibar na kulipa Masheha. Wanaokusanya pesa za visa ni watumishi wa JMT wanaoitwa Uhamiaji wanaolipwa na JMT a.k.a Tanganyika

Watanganyika hawalalamiki kuonewa na Zanzibar , huo utajuwa ujinga.
Watanganyika wanasema viongozi wanafuja raslimali zao kwa kuruhusu 'abuse' yakatika Muungano.
Ilitokea huko nyuma tukawa na G55 na sasa inajirudia tena kwa kasi.

Hivi unatoaje pesa hazina Dar es Salaam kwenda kujenga Ofisi ya Waziri mkuu na Makamu wa Rais wa JMT Zanzibar tukijua Ofisi zitakuwa na Watumishi na matumizi lakini viongozi hao hawana la kufanya Zanzibar?

Hii ni ku abuse fedha na kodi za Watanganyika bila sababu kwa kisingizio cha Muungano!

pengine uwe na haja nyingine uzingatie TU kuwa ndoa yatu ni ya kipekee huikuti duniani pote,

B

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna upekee kuna ubababaishaji tu , Muundo wa Muungano ni hivyo! period.
 
Nasikia watu wanasema bendera nusu mlingoti nikiuliza kimya hawajibu kuna nini jamani.....
 
Shukurani sana mkuu msakaa jr ila nafikiri Rais Tsheked akiamua kuwa na urafiki na Urusi pamoja na kundi la Wagnar group Mmarekani na vibaraka vyao hapo Congo anakalishwa chini.
Unadhani kwa nini bibi huyu Mkuu wa Kurugenzi ya intelijensia ya USA kaamua kufanya ziara ya kukutana na Tshekedi?

Hayo, uyasemayo yapo na yanaendelea mpaka muda huu.

Kama unakumbuka mwaka jana, zilifanyika ziara mfululizo Kagame akifuatia baada ya Tshekedi kutoka Tanzania, Tsh alikuwa ameomba nini kwa Tanzania?
 
Nakubaliana na wewe kabisa kuhusiana na KATIBA ya 1977 ikisema bayana Tanganyika itakuwa Tanzania Bara na Zanzibar itakuwa Tanzania visiwani

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Aliomba nini?

ulisha wahi kusikia mtanganyika anajitambulisha kuwa ni mtanganyika? unajua ni kwa nin?

mkuu muundo wa sasa wa serikali ndyo Bora x1000 kuliko muundo mwingine wowote utakao pendekezwa, kama huu haukubariki maana yake Muungano ufe! na ukifa atakae athirika zaidi ni Zanzibar kwa kuwa atalazimika kuwa mkimbinzi kwenye ardhi yake mwenyewe..

nlisema hapo juu narudia tena hii ndyo ndoa(muungano) pekee duniani ambayo watu wanakuja kujifunza kwetu, kwamba nchi inakuwa na Marais wawili lkn mkuu wa majeshi1,

hapo ndipo upekee unapokuja kwamba mkuu wa majeshi wa Tanzania ndyo anapokea order kutoka Kwa mtu 1 tu bila kujari hyo event imetokea Zanzibar au Tanzania!

ila rais wa Zanzibar anayo mamlaka kwake TU na kwa baadhi ya mambo, mengine nae anayaona na kuyaacha yafanyike hawezi kuyabadili, Wala kuyasemea na huo ndio muungano,
umependa imeze hujapenda imeze hvyo hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unadhani kwa nini bibi huyu Mkuu wa Kurugenzi ya intelijensia ya USA kaamua kufanya ziara ya kukutana na Tshekedi?

Hayo, uyasemayo yapo na yanaendelea mpaka muda huu.

Kama unakumbuka mwaka jana, zilifanyika ziara mfululizo Kagame akifuatia baada ya Tshekedi kutoka Tanzania, Tsh alikuwa ameomba nini kwa Tanzania?
Aliomba nn Felix kutoka Tanzania ?
 
Unadhani kwa nini bibi huyu Mkuu wa Kurugenzi ya intelijensia ya USA kaamua kufanya ziara ya kukutana na Tshekedi?

Hayo, uyasemayo yapo na yanaendelea mpaka muda huu.

Kama unakumbuka mwaka jana, zilifanyika ziara mfululizo Kagame akifuatia baada ya Tshekedi kutoka Tanzania, Tsh alikuwa ameomba nini kwa Tanzania?
Mkuu hata sijui aliomba nini, ila Tanzania haiwezi kuwafanya Wacongo uporaji wa rasilimali zao kutoka mataifa ya magharibi kupungua au kuisha bali Mrusi na Kundi lake la Wagner kwa makubaliano maalum.
 
Wakuu hili suala la muungano linaumiza sana hisia za watu hasa ukizingatia vifungu vilivyochambuliwa na wadau hapo juu👆 na kina NGURUVI, Nguruvi3.

Kiukweli hizi kasoro zinachoma, more painful kwa sisi watu wa bara huku, yaani hapa kifua kinafurukuta kwa gadhabu ile mbaya! Ila hii hali naitafsiri kama hisia(emotions) tu, ni kweli vitu kwa ground vipo hivyo lakini tusichukue maamuzi magumu kwa msisimko wa hisia kwa ambavyo vinarekabisika. Hili dude linahitaji strategic plans makini sana & in a diverse way zitakazo angazia hatima ya vizazi vijavyo.

Intelligence will... katika hili naona itakua positive na ita-make sense kama itachagua kudumisha muungano, na pengine muungano upo hadi leo kwa sababu ya hihi intelligence... waliona ni busara zaidi kuriko usiwepo.

Pendekezo langu ni kwamba tusijikite kuuvunja bali tujikite kuuimarisha huu muungano kwa;

1) Kuboresha vifungu vinavyotafrika kama kero za muungano kuendana na hali halisi ili muundo wa serikari mbili ama tutu uweze kua na afya zaidi pande zote. Haya mabadiliko yaanzie kwenye sheria mama na yasomane mpaka kwenye sheria za serikali zote.

3) Muundo wa serikali mbili uondolewe uletwe muundo wa serikari moja usio na MAKANDOMAKANDO/KONAKONA WALA (MBA)3 = MBAMBAMBA, yaani nchi inakua ya serikali moja JMT, harafu Kagera Kigoma Mtwara Tanga Zanzibar Dar es salaam nk... Inakua mikoa na mapato yatagawanywa kulingana na potential iliyopo mkoa husika.

Huu upande wa pili wa shilingi ni fikra zangu binafsi usizingatie saana.👇👇👇

Kuna watu wanaishi kwenye familia mambo safi mahitaji yanapatikana kwa wakati wazazi wao wananguvu ya kiutawala na uchumi yaani wanaheshimika mtaani kwao, sasa hawa watoto ama wajukuu wanawaona walala hoi kama wazembe hivi, hawana plan wanahisi mambo yao yako poa kwasababu mikakati, elimu waliyokua nayo (wanazani ni uwezo wao binafsi).

Wanafikia hatua wanaamini uchawi haupo wengine wanasema hakuna Mungu(Nguvu ya Mungu), yaani wanaamini completely kua waganga na watumishi wa MUNGU ni matapeli wanatuigizia tu. Kumbe wasijue watangulizi (ancestors) wao kuna harakati walifanya zinazowaweka salama hadi leo kiasi kwamba wasione changamoto yoyote duniani hapa, hata wakikutana na changamoto siku moja wanaona ni coincidence tu, kiufupi duniani kuna sarakasi nyingi sana ukiona unautulivu wa kiafya kiuchumi tambua sio bule kuna nguvu ipo nyuma yako. Hili suala sio lahisi kulielezea/kuthibitisha mtu akaelewa/akaamini ni mpaka limtokee yeye mwenyewe, ali-experience by direct observation, tafauti na hapo mtu wa namna hii atakuona wewe ni mjinga unaeshindwa kufikilia mambo kwa kina, au una ufinyu wa akili.

Nachotaka kulielezea hapa ni kwamba mambo mengine ni ya kiroho haijalishi ni👉🌗☯️. Nguvu ya kiutawala. Rabbon.

Na ndio maana mataifa makubwa migongano yao mikubwa asilimia kubwa hua inahusisha territories zilizozungukwa na maji bahari kwa kiasi kikubwa kama visiwa(Taiwan, Hong-Kong, Hawai).... peninsula(Korea zote).

Ivi marekani na urusi huku Middle East & far east hua wanatafuta nini? hasa marekani na wakati yeye ni bara lingine kabisa.

Kuna nukuu ya Baba wa Taifa ile nukuu ukii- listen between the pitches utapata kitu, kua "watakao watenge/wabagua wenzao ile zambi ya ubaguzi haitaishia pale inaendelea... .. ." siikumbuki vizuri nukuu. Ila sizanzi kama alizungumza kwa bahati mbaya.
 
Back
Top Bottom