Dark wealth, dark path, is the only way to rich

Tafuta taratibu utapata, njia ya giza ina utajiri lakini umejaa mateso, mahangaiko na taabu tupu.

Nje utaonekana kama una nuru lakini moyoni kunawaka moto.

Wazazi/walezi wako hawakuwa wajinga kuacha kukutoa kafara ili wawe matajiri.
Kuna kipindi kuna mtaalamu fulani alikuja kutoka bush akaja town kufanya mambo, basi akafanya mambo yake akawa anataka kumaliza jamaa mmoja akamfuata tukiwa pamoja na mimi nikasikia akamwambia anataka kua tajiri kwa namna yoyote sijui walifanya nini ila ulipita mwaka mmoja tu jamaa akawa tajiri kweli ila utajiri wa hivi ni mbaya kuna kitu unaambiwa ufanye km kutekeleza damu yako iwe inaishi kwa mateso sehemu yaan unatia mimba kisha mtoto humuangalii tangu akiwa mtoto ukimrudia tu utajiri unayeyuka na masharti mengine magumu kuna vitu jamaa alikua anavifanya kisa tu apate utajiri na vyote ni giza tupu
 

Kijana soma Biblia​

Kumbu Kumbu la Torati 8:18​


Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
We naye elimu yako ya kuunga unga haijakusaidia..embu soma vizur huo mstari wako .."akupaye nguvu"
Mtu anayekupa nguvu ndio mwenye milki za utajiri na mali za dunia ?
 
Kisha The Devil akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia."

Akamfukuza..ila ajabu ni kwamba hakumpinga kauli yake kwamba mali na utajiri ni vya kwake.
 
wewe ndio ibilisi mwenyewe, shindwa pepo
 
Unadanganya tu watu, tafuta mtaji, fungua biashara inayoeleweka, na unayoielewa, isimamie pata hela.
Hela wekeza kwenye madili haya. The more the money , the more the profit.
Hamna cha shetani, njia pekee ya utajirii ni more transactions.
Tupo sisi tulianza na laki nne mtaji na return ya 210,000 kwa mwezi biashara uchwara kabisa za mitaani.
Sahvi tunapigania deals kubwa zaidi. One deal profit kubwa tu. Unasema uchawi. Fck you.
Acheni kuandika ujinga humu. Mitandaoni.
 
Tafuta taratibu utapata, njia ya giza ina utajiri lakini umejaa mateso, mahangaiko na taabu tupu.

Nje utaonekana kama una nuru lakini moyoni kunawaka moto.

Wazazi/walezi wako hawakuwa wajinga kuacha kukutoa kafara ili wawe matajiri.
Shida iko Hivi! Ndo maana wengi wanaenda shortcut wakidhani watafanikiwa maisha yao yote. Utajiri wa shetani una gharama za makafara ya kuua na utajiri ule huwa ni wa muda maana ni Kiini macho.

Wengi wanakimbia kumwomba Mungu utajiri sababu Utajiri wa Mungu sio wa kila mtu anaweza. Mungu ili aweze kukupa utajiri Lazima akupitishe kwenye Hekima zake( Ili dhahabu ing'ae lazima ipite kwenye Moto). Kwahiyo Wengi hiyo hawataki.
Mungu hataki akikupa utajiri uanze kuutapanya mwisho wa siku huna hata mia. Mungu anataka akikupa utajiri unakua ni Baraka kwa vizazi vyako vyote.

Watu wanaenda shortcut sababu wa ukipitishwa kwenye hekima za Mungu lazima ujitambue kua wewe ni nani na ni wapi unakoelekea/Maono yake.

Yeye shetani anagawa tu hata sahizi ukiitaji unaibuka tajiri. Utajiri wa Mungu Una mchakato sana.Ila ukibarikiwa unakua ni utajiri wa vizazi na vizazi.
 
Utajiri kwa njia za giza ni kweli unapatikana, lakini hauna utulivu wala furaha ya kutosha ndani yake.

Mwanzoni utafurahia, lakini Shetani akianza kukaza nati, hakika hakuna rangi utaacha kuiona.
 
Umenifungua macho
 
Yesu ni mwana wa Mungu! Alikua anajua fika kuwa shetani ana mjaribu maana hana huwezo huo wa kumpa utajiri.
Utajiri wa shetani ni Kiini macho huwa ni utajiri wa Muda fulani tu.
 
Wewe bado fukara unatukana ovyo mitandaoni unatukana usiowajua ..unautajir gani wewe fukara bado una muda wa kuja kutukana usiowajua humu , wewe endelea na biashara za walalahoi hizo unapata vimilioni ukitukana watu ndio unajiona tajiri fala wewe huna hela wewe nahujui lolote
 
Aiseeh.. hatari sana! Kwahiyo mambi ya mwilini tukampigie magoti shetani???

Mungu hayuko hivo!
Unaujua utajiri?🤔
Achana na pesa za kubadilisha mboga hizo utapata ila kua tajiri sahau
Mungu atakupa utajiri wa rohoni na ghala lako halitokaukiwa chakula wala maji.

Luka 16:13, Yesu alisema juu ya "ukwasi" (neno la Kiaramu kwa "utajiri"): "Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana, ama atamchukia huyu na kumpenda huyu, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali."
 
Yesu ni mwana wa Mungu! Alikua anajua fika kuwa shetani ana mjaribu maana hana huwezo huo wa kumpa utajiri.
Utajiri wa shetani ni Kiini macho huwa ni utajiri wa Muda fulani tu.
Kisha The Devil akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia."

Akamfukuza..ila ajabu ni kwamba hakumpinga kauli yake kwamba mali na utajiri ni vya kwake.
 
Ndo maana tunamwambia jamaa hapo utajiri wa shetani ni kiini Macho wenyewe hao waliomfanyia huo utajiri hawautaki hata ishi yao sio ya kufurahia.
Utajiri huo ukiyeyuka kama hutasikia jamaa Kafa au kawa kichaa nimekaa pale. Asipojisalimisha kwa Yesu ndo habari yake kwisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…