Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Nimemsikia Waziri wa Ujenzi, Abdalla Ulega akigombana na Makandarasi wa kichina wanaotekeleza miradi kadhaa ya DART(Dar es salaam Rapid Bus Trasnport), inayohusu ujenzi wa barabara za mwendo kasi wa mavbasi jijini Dar es salaam.
Bahati mbaya kwamba waziri Ulega ameyarithi matatizo yaliyokuwepo nyuma.
Waziri aliyemtangulia alisaini miradi mingi ya DART jijini, bila kuwa na strategic execution plan.
Miradi hiyo kama ifuatavyo:
-Airport-KAMATA/JAMHURI RD
-Bibi Titi rd
-Azikiwe rd
-Alihassan Mwinyi Rd-Morocco
-Morocco-Mwenge
-Ubungo-Mwenge
-Kimara -Mwenge
-Mwenge-Tegeta
-Tegeta-Boko
Hiyo ni miradi tisa(9), na yote inafanyika kwa wakati mmoja.
Hili kwa jiji la Dar es salaam inashangaza , ukifikiria msongamano wa magari na ufinyu wa njia za mchepuko(Diversions)
Kulikuwa na ulazima gani kuifanya miradi hii kwa pamoja,.
Hilo anaweza kujibu Waziri Mbarawa, inaelekeea kuna kitu nyuma ya pazia hapa.
Halafu utekelezaji wa miradi ya miji yote hufanyika kwa kiwango kikubwa usiku.
Sasa hawa wenzetu wa kampuni za kichina, hawafanyi kazi mchana wala usiku.
Kwenye picha ni Bibi Titi rd, wafanyakazi hapo wanabarizi tu, hakuna kinachoendelea
Hapa somo lazima liwepo.
Mbaya zaidi miradi karibu yote ya WORLD BANK ni wachina wanapewa.
Wachina wanajulikana kwa kuhonga ili kupata miradi, na WORLD BANK nao si malaika, tunajua wako corrupt.
Serikali iwasikilize wadau wake.