Darweshi ni nani?

Grand Master Dulla

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2012
Posts
411
Reaction score
148
{NO OFFENSE GUYS}Habari zenu waungwana nawasalimu sana,hoja yangu iliyonileta hapa leo ni kitu kinachonitatiza na chenyewe ni:miaka ya 80 na 90 kulikuwa kuna mzee mmoja maarufu sana nchini akifahamika kama darwesh[kuswali mnareke] ambaye mungu alimpa uwezo mkubwa sana,moja ya maajabu yake alikuwa anaweza kwenda Maka kwa dakika tu nyinyi mkitoka hapa na ndege mnamkuta kashafika na anawapokea na makarama mengine mengi sana mungu aliyomjaria,sasa nia yangu haswa ni kutaka kujua huyu mzee sasa hivi je yuko wapi? na kwa wale mliobahatika kuona maajabu yake mnaruhusiwa kufunguka,na kwa yeyote mwenye la kusema anakaribishwa ila tu nawaomba sana tuchangie kwa upendo na upole kwa maana si jambo zuri kusimanga wala kutukana dini ya mwenzako,dhumuni ni kuhifadhi histori,kwenu wadau...
 
Kuna mmoja alivuma miaka ya 90 kama mganga alikuwa akitibu ukimwi. Aliishi moshi maeneo ya dsm street jina lake kamili lilikuwa:shaaban darweshi .. Sijui ndo mwenyewe??
 
Eti mkipanda ndege pamoja mnamkuta ameshafika ninyi bado. Aiseee Mkuu, katika ulimwengu wa roho kuna mipaka yake na kuna sehemu mambo hayaendi kirahisi hivyo.

Kifupi hamna uchawi huo.
 
Mleta mada. Kuhusu yule bwana maarufu "Kuswali mnaleke" miaka ile ya 80-90 ulikuwa ni utapeli wa kutupwa wa kundi fulani la wajanja kutoka Mtwara na Newala wakimtumia yule bwana mwenye mapepo kwa kivuli cha dini. Kati ya sifa/miujiza yote ulizozisikia hakuwahi kuwa na hata nusu ya mojawapo hakuna ushahidi wa wazi hadi leo. Wajanja wajasiriamali walimtumia mwisho wakamtosa kama yule Mtoto Sheikh Sharifu. Ila alitingisha sana mikoa ya kusini miaka ile huyu Bwana.
 
tuchangie kwa upendo na upole kwa maana si jambo zuri kusimanga wala kutukana dini ya mwenzako,dhumuni ni kuhifadhi histori,kwenu wadau...
hivi hapa umeongelea dini?, kuwa serious usiamshe hisia ili watu watapike harafu uanze kulalama
 
Eti mkipanda ndege pamoja mnamkuta ameshafika ninyi bado. Aiseee Mkuu, katika ulimwengu wa roho kuna mipaka yake na kuna sehemu mambo hayaendi kirahisi hivyo.

Kifupi hamna uchawi huo.
Acha ubishi inawezekana.
 
Namfahamu vizuri huyo Darwesh kwa jina jengine Shekh rocket. Hana karama zozote ni maamuma wa mwisho. Safari zote as hijja anapata misaada kutoka kwa mashia. Nilikuwa nae hema moja Makkah 2015. Utashangaa matusi yanavyomtoka ktk kulingania. Dish lake limecheza.
 
Duh hivi huyu mzee hadi humu anajadiliwa aiiseeee...
Swali lako la Daruweshi ni nani ushajibiwa hapo juu japo kaongeza vikorombwezo ambavyo vimekufanya akajaza upepo hadi ukatoa povu.
Kilugha na kimaana Daruweshi ni mtu mpenda dini asiyekuwa na elimu.
Na kuhusu huyu mzee kwa mara ya mwisho nilishuhudia mwenywe mkoani Mbeya msikiti wa BLOCK Q Mtaa wa Soweto jamaa mmoja aliejitia uhadhiri na ni mkongoman alijitambulisha kama Sheikhe Ukasha aliongea mengi ila mwishoni akasema anawaletea zawadi wanaMbeya nayo ni kuwapelekea sheikhe mwenye makarama na kwa Afrika wako wawili ni yy kuswali mnaleke na mwingine yupo Nigeria (ila huyu hakusema anaitwaje)
Na akasema huyu kuswali mnaleke anafika Mbeya kwa mara ya kwanza hajawahi kufika Mbeya b4 ila kwa hapo alisimama muumini mmoja akamuweka sawa kuwa alishawahi kupita miaka ya nyuma akiwa anaelekea Zambia kwenye muhadhara jamaa akajifanya alitatizika kwa hilo.
Mbaya zaidi wengi wao waumini yale maneno walikuwa wanapokea kwa kuyaamini na hilo nililibaini baada ya mijadala ya nje ya msikiti kila kundi lilikuwa linajadili kimlengo wa kuyaamink yale yaliyosemwa...
E.g
=Ukimuelekeza matatizo yako anasema tu FATEEEHAAA..
=Kuwa anaweza kupaa (japokuwa mwenyewe anakataa)
=Halali kitandani..
Na haya ni machache aliyokayasema ila ss tulisikia mengi zaidi ya haya ila ikaja kubainika ni uzushi hata km zamani tulikuwa tunaamini.
Na siku zilivyosonga mbele akaanza kuonekana ni kweli ni mtu asiye na elimu kwa kuwa hata ulinganizi wake alikuwa anachumpa mipaka.
Na kwa ss huwa anapatikana sana Dar es salaam na kwa mikoa ya pwani 90% wanamfaham kiuhalisia wake shida ipo mikoa ya kanda nyingine ambako wapiga dili wanamtumia vibaya mzee wa watu ili wapate pesa na haishiwi kusafirishwa mikoa ya Kagera, Kigoma, Iringa,Sumbawanga n.k
Ila ubora ni kuutafuta ukweli ili usiwe na shaka na unachoaminishwa.
Nawasilisha.......
 
Kwakweli mimi pia nimesikia mengi kuhusu huyo darwesh hasa viroja alivyofanya akiwa mikoa ya kusini, Kwamba aliwahi kuwekwa mahabusu lakini ikawa ikifika muda wa swala anatoka kimiujiza, anarudi tena mahabusu anaomba wamfungulie aingie tena mahabusu.
Pili, kwamba kuna kijiji walimdhihaki basi akawalaani ikaja mvua sio ya kawaida ikabadirisha mkondo wa mto maji yakapita katika hicho kijiji tena usiku wa manane na kuleta madhara makubwa ya vifo na kukifuta hicho kijiji katika uwepo wake.
Ni hayo pamoja na mengi tumesikia masimulizi ya mtu huyo, na kwamba mpaka sasa huyo bwana yupo dar es salaam.
 
Darweshi ni muunganiko wa maneno mawili ya Kiarabu.
Dar=nyumba
Wesh=tupu/empty.
Kwahiyo darweshi ni mwendawazimu anayetangaza dini fulan (dini yoyote).
Samahani kwa maneno haya.
Mimi mzee huyu namfahamu sana,aliheshimika sana miaka ya 90 huko kwetu Lindi na Mtwara.
Nikimwaga sana mengi kuhudu udarweish na Kuswali Nnaleke najua tachafua hali ya hewa humu.
 
shikamoo alhaji .......
 
Kuswali Mnaleke au Darweshi ni mtu ambae hana muujiza wowote. Kikubwa hana elimu ya dini na kwa kuthibitisha hilo wkt analingania anatumia lugha ya matusi. Namfahamu vizuri saana kwani sote tu wenyeji wa kijiji cha Mumburu wilayani Masasi
 
Kuna mmoja alivuma miaka ya 90 kama mganga alikuwa akitibu ukimwi. Aliishi moshi maeneo ya dsm street jina lake kamili lilikuwa:shaaban darweshi .. Sijui ndo mwenyewe??
Mkuu namkumbuka mtoto wake aisee.Tulimkuta Korongoni primary.walikuwaga na farasi aisee.Yule mazaa tulikuwa tunamwogopa kwelikweli,alikuwa anavaaga kininja wakati wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…