Mwl.RCT
JF-Expert Member
- Jul 23, 2013
- 14,624
- 20,666
Dassault Rafale ni ndege ya kivita ya Ufaransa yenye uwezo wa kufanya kazi katika anga, ardhi, na baharini. Iliundwa na kampuni ya Dassault Aviation na ilianza kutumika mnamo mwaka 1986. Ni ndege ya kwanza ya Ufaransa ya kizazi kipya na ina sifa kubwa kwa utendaji wake.
Ndege hii ina silaha za kisasa, kama makombora, mabomu, na mizinga. Ina mfumo wa elektroniki wa juu, ikiwa ni pamoja na radar na mifumo ya kudhibiti elektroniki. Inaweza kugundua na kushambulia malengo ya adui kwa haraka na ufanisi. Pia ina mfumo wa kujilinda dhidi ya silaha za adui.
Dassault Rafale inalinda usalama wa Ufaransa katika mazingira mbalimbali. Inafanya ulinzi wa anga, upelelezi, na operesheni za kimataifa. Ina uwezo mkubwa wa mashambulizi na ulinzi na inaweza kukabiliana na adui yeyote.
Ndege hii pia imetambuliwa kimataifa na imeuzwa kwa nchi nyingine duniani. Imethibitisha uwezo wake katika vita na imekuwa chombo muhimu katika usalama wa kimataifa.
==
F-35 inaondoa maana ukiondoa stealth. Kila kitu kwenye fighter hiyo kinategemea stealth capabilities. Ina weapons integration ndogo kuliko Rafale sababu sio ndege ya kufanya kazi kubwa za mara kwa mara bali kazi ngumu na za uchache.
Ina datalink & communication nzuri na electronic warfare nzuri, ina variant nzuri zaidi kwa aircraft carrier.
Rafale naiona nzuri zaidi ya Typhoon.
1. Rafale ina carrier based variant ambayo India wamenunua mwaka jana or juzi. Typhoon haina uwezo huo (moja ya sababu Ufaransa ilijitoa kwenye hiyo programu na kwenda yenyewe na Rafale)
2. Rafale ni system ya nchi moja, unahitaji kuwa na mahusiano mazuri na Ufaransa tu ili uinunue. Typhoon mpaka Ujerumani, Uingereza, Italy na Spain wakubali maana consortium inawahusu wote waliichangia. Kununua silaha ni geopolitics nyingi na kuna sintofahamu kubwa mbelen, Iran walinunua F-14 Tomcats hawapewi support tangu mapinduzi ya Shah, Ukraine wana Soviet weapons nyingi wanapata shida components ziko Russia, Russia wana melivita ambazo ziliundwa shipyards za Ukraine na wana powerplants za helicopter walikuwa wanachukua components Ukraine. Kuhusisha silaha yako kwa nchi nyingi ni hatari zaidi kuliko nchi moja.
3. Rafale naona ina performance nzuri na overall capabilities nzuri zaidi ingawa zinashindana vikali na Typhoon. Kwenye tender Rafale Iiko more likely kushinda kama vitu vingine viko constant.
Tatizo lake ni bei yake kubwa sababu mgawanyo wa cost of production ni kwa Ufaransa tu, ila Typhoon waligawana nchi nne. Hata MBT ya Ufaransa ile Lecrerc ni bei ghali sana kuliko vifaru vyote vya NATO ila haimaanishi ndio kina uwezo mkubwa kuzidi vingine.