OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Kwangu nadhani ili Tanzania tuweze kupiga hatua, VAR ni kitu cha baadaye sana. Kwanza inabidi tuwekeze kwenye kuendeleza kiwanda chetu cha michezo kabla ya masuala mengine ambayo yanaweza kufanyika baadaye sana.
Ni wazo zuri kufunga VAR lakini kwangu wazo zuri zaidi kwa sasa ni kuwekeza kwenye miundombinu ya michezo kama nchi. Ni ngumu kwenda na vitu vyote kwa wakati mmoja, lazima kuwe na vipaumbele kwenye uwekezaji.
Tutengeneze kwanza mifumo ya kuendeleza soka la vijana, kwa maana ya kuwa na ‘proper academies’ na kupata wataam waliobobea kwenye eneo hilo sio kuwa na vituo vya kulelea watoto.
Ni viwanja vingapi Tanzania vina miundombinu rafiki ya kufungwa teknolojia ya VAR? Kama timu bado zinacheza mechi za Ligi Kuu kwenye viwanja vilivyojaa maji bado tunahitaji VAR kuwa kipaumbele kwa sasa?
Mataifa ambayo yanatumia VAR tayari yamepiga hatua kubwa kwenye maeneo mengine, tukubaliane kama nchi kwamba kuna mambo mengi ya kufanya kabla ya kufikiria kutumia VAR baada ya kupata usumbufu unaotokana na makosa ya waamuzi.
My Take
Fikiria huyu ndio waziri wa fedha anayemshauri Rais masuala ya fedha na uchumi. Hawa ndio walituletea tozo bila tafiti,leo wanataka kuleta VAR bila wiwanja. Utopolo ni utopolo tu