Daudi Ballali's Death

Status
Not open for further replies.
Balali hana rekodi yoyote ya public!
Kuna issues mkuu
 
Balali kafa ndio lakini nimesikitika zaidi kwamba kafa tangu ijumaa iliyopita serikali imebana habari mpka ilipoona imejulikana ndio leo BOT wanatoa kijitaarifa! Hivi watz hii serikali ipo kwa ajili ya nani?Enzi za Benm serikali ilikuwa 'out looking' rather than 'in looking', sasa tuna serikali ya kihuni ambayo inajua mwananchi ni wa kudanganya tu!! UUuuuuuuuuuuuuuwiiiiiii........shame upon the fuckin gov of JK.
Natamani kutokuwa mtz...lakini nitakuwa mm..wapi?najisikia aibu kwa upuuzi huu....Mungu angekuwa bado anaumba land zaidi ningehamia haraka ile angeumba next.....Jamani hatuwezi demand mwili wa Balali urudishwe bongo tuuone au ndo tutakubali fix hilo?
 

Na Balali naye alitishwa na nani?
Hizo signarures zao zinatosha kuwafungilia mbali!
Then kama wanataka kusema ni Balali aliwashurutisha kusaini then makosa ni ya marehemu kwa upande wake..Na kwa upande wao hawawezi kuja na usemi eti wametishwa!
Wanakuja na barua!
Kutishwa hiyo ni hearsay!
Signatures of approvals is what matters
 
Na pia Serikali itoe TAMKO kuwa walimuhoji lini marehemu!
Kwasababu walikuwa hawamuhitajiThen wakamuhitaji baada ya kifo?
Ama walikuja kugombea newz alizaocha Balali ama ni kufacilitate whatever they seem to be doing?

kwa kifupi hii ishu hadi hapa ilipofikia ni very shaky and the same time tricky. Think of a tactic kuwakamata hao waliosaini barua, either way they have a higher chance (99.9%) kuescape. Trust me. Everything they say, will rely on Ballali (thats if kama hao watu watakamatwa).. in this case, kama watakamatwa then ujue it wont take long kabla ishu nzima haijazimwa.

Maana wakikamatwa anyway soon (maybe in the next 4 months) tokea kifo cha ballali, basi ujue COLD CASE CLOSED ! Kwanza utasikia ushahidi wa kutosha hakuna, shahidi mkuu hayupo, so hata kama ni kweli, but regarding to law policies hata kama mtu amekosa and no one is there to testify HUWEZI KUMUHUKUMU !
 
Poleni sana wana ndugu,Mwili wake unaletwa kuagwa lini maana siku hizi mhh?.Hii inaonyesha katika kipindi cha miezi 6 iliyotolewa na Kikwete na kwa mafisadi kujihami yatakuwa yametokea mambo mengi makubwa.
 
JMUSHI
watakamatwaje wakati shahidi nkuu HATUNAYE !!

ishuz zote anazo Ballali, kama kuna volunteer anayeweza kumfuata ballali huko alipo, basi aende na kama ataweza kurudi na majibu itakuwa bomba !

Kwani Ballali ndiye alikuwa mtendaji wa kila kitu cha BoT? 😕 si kuna makabrasha kibao ambayo baadhi yake yalitumiwa na Ernst & Young kufikia conclusion kwamba $133 million zimeibwa na kuingia CCM, meremeta, Tangold, mifukoni mwa mafisadi n.k.? Hao Ernst & Young hawakuongea na Ballali ili kufikia conclusion hiyo na hiyo ni katika kipingi cha mwaka mmoja tu wa 2005/2006. Wangeanza tangu Ballali alipoingia BoT 1998, basi si ajabu hiyo amouny ingeongezeka mara 10.

Wahusika wote bado wana kesi ya kujibu na ripoti ya Ernst & Young imeeleza hivyo. Kama Ballali kaenda kufichwa nchi nyingine na kupewa jina jipya na vitambulisha vipya, haizuii kabisa kuafikisha mahakamani mafisadi wengine walioshiriki katika ufisadi huo na hatimaye kuwafilisi mali zao zote ndani na nje ya nchi. Kamwe msijidanganye kwamba kumficha Ballali ndio mwisho wa sakata hili.
 
EPA haiwezi kufa hivihivi kwani wale wananorudisha na waliforge documents wanaweza kushitakiwa hata kama balali hayupo, tunasubiri tamko la serikali rasmi watwambie kuwa hawawezi kuwashitaki watu wa EPA kwa kuwa Balali amekufa, tutahoji iwapo balali alisafiri na nakufa na ofisi ya serikali kama BOT.
 

hilo jibu la ballali alitishwa na nani analo BALLALI MWENYEWE- ambae in this case - KAFA ! ndio maana nasema, hapa mambo ni magumu, na kama watatumia sheria kama inayopaswa kufuatiliwa, consider this case DONE !
 

if so, mbona muda wooooooooote huo humu JF pamoja na serikali ilikuwa ikimsubiri mtu mmoja (BALLALI) ilihali tulikuwa tukifahamu fika kwamba kesi inaweza kuendelea bila ya ballali ??
 
Kada ofisi kama BOT haindeshwi na mtu mmoja, kuna makabrasha kibao ofisini yanayoonyesha jinsi wizi ulivyofanyika hivyo usiwe na wasiwasi tuko njia mmoja kuakikisha kila kitu kiko wazi hata deepgreen tutajua hata kama balali amekufa.
 

Shahidi mkuu siyo Ballali bali ni receipts zilizotumika katika kuiba pesa hizo na kuingia katika bank accounts mbali mbali za akina meremeta, tangold, Anna Muganda, na makampuni mengine ya kifisadi. Kuna wahasibu, makarani n.k ambao kwa namna moja au nyingine walihusika katika kutengeneza hizo payment voucher ambazo zilisainiwa na watu mbali mbali labda akiwemo Ballali ambao pia wanaweza kutoa ushahidi wa kuwatia mafisadi hatiani. Narudia tena Ernst & Young hawakumhoji Ballali bali walipitia makabrasha mbali mbali ili kufikia conclusion yao kwamba wizi wa $133 millioni ulifanyika na watuhumiwa wote walio hai wana kesi ya kujibu pamoja na yule aliyepokea pesa hizo kwa niaba ya chama cha mafisadi ambao nao walipata mgao wao wa mabilioni.
 
are you convinced that bila ya ballali case itakuwa solved ?? and if so, basi naweza kusema muda wote tulikuwa tunacheza cheza na kumentateini ballali !
 

Baada ya kutoka hapo!! nikiwa ni mwingi wa mawazo huku nikitafakari ni namna gani mtu ambaye si ajabu ana mchango mkubwa katika ufukara wangu, anazikwa kwa heshima kubwa namna hiyo na mazishi yake kuhudhuriwa na watu wengi kiasi hicho, ghafla najikuta nimefika kwenye mataa ya kuelekea Oysterbay ambapo namkuta Askari Trafic akiwa amekazana kuamuru magari yaelekee Mwenge bila ya kujali kuwa yalikuwa yamejaa kwenye foleni.

Lakini wakati nashangaa ya Trafic yule, ghafla King'ola kikasikika. Awali nilidhani kuwa ni Ambulance inamuwahisha mgonjwa kwenye ile Hospitali inayofanya upasuaji wa juu chini chini juu.

Kumbe si ambulance, bali ulikuwa msafara wa Mkubwa unapita kuelekea Mwenge ukitokea Mjini " Mh!!!!" Nikaguna. "Si wakubwa wote nimewaacha pale kwenye mazishi ya BAZAZI", sorry I min Balali, nikajisemea mwenyewe, "Sasa imekuwaje huyu tena anapita mitaa hii na saa hizi".

Sikuwa peke yangu katika mshangao ule, yawezekana hata yule Traffic hakutarajia msafara ule kwani badala ya kuuelekeza msafara ule ulikokuwa ukielekea, alijikuta akiuelekeza njia ya Kinondoni yalikokuwa yakifanyika mazishi ya BAZAZI. He!!! jamani inakuwaje namwita yule marehemu Bazazi badala ya Balali? "Makubwa madogo yana nafuu" Nikajisemea kimoyomoyo.

Alikuwa ni Bw. BEN CHENKAPA A.K.A MMEMWENZA NA PESAMBILI sijui alikuwa anaenda wapi kwani kwa mujibu wa kumbukumbu zangu, anaishi Sea View. Na sasa sijui anaenda wapi huko? Nikajiuliza mwenyewe bila ya kupata jibu.

Lakini huyu jamaa si alikuwa Swahiba mkubwa wa BAZAZI, SASA INAKUWAJE hajahudhuria kwenye mazishi yake.

"Ah!! labda anaogopa kuzomewa na waombolezaji make hata kuonekana kwake siku hizi, amekuwa kama lulu". Nikajisemea na kisha nikavuka zangu barabara huyooooooo!!!!! Ufukweni.
 

Chiefmtz,

Mkapa anakuja marekani kwa kujificha utadhani muuza madawa. Hawezi kutokea hata kwa maji ya dawa......
 
Chiefmtz,

Mkapa anakuja marekani kwa kujificha utadhani muuza madawa. Hawezi kutokea hata kwa maji ya dawa......

Hivi tukimpa mwaliko wa kuja kupokea Medali ikiwa ni kama kutambua mchango wake wa kuanzisha NGO ya kupambana na Ukimwi aka kudumisha UFISADI, hawezi kweli kutokea na kwa jinsi anavyopenda sifa?


"HUYU NDIYE MWANA NIMPENDAYE"............MKAPA
 

Attachments

  • Balali.jpg
    11.6 KB · Views: 40
Hivi tukimpa mwaliko wa kuja kupokea Medali ikiwa ni kama kutambua mchango wake wa kuanzisha NGO ya kupambana na Ukimwi aka kudumisha UFISADI, hawezi kweli kutokea na kwa jinsi anavyopenda sifa?


"HUYU NDIYE MWANA NIMPENDAYE"............MKAPA

Nadhani hilo litakuwa wazo zuri sana!
 
if so, mbona muda wooooooooote huo humu JF pamoja na serikali ilikuwa ikimsubiri mtu mmoja (BALLALI) ilihali tulikuwa tukifahamu fika kwamba kesi inaweza kuendelea bila ya ballali ??

Nani aliyekwambia sirikali ilikuwa inamsubiri Ballali? 😕
Hivi hukusikia Mwanasheria Mkuu na Mkuu wa Polisi walipozungumza kwamba wahusika wa ufisadi wa EPA ni matajiri wakubwa hivyo wakikamatwa nchi inaweza kulipuka? Sikuwahi kusikia kama walisema wanamsubiri Ballali, kama una ushahidi wa hilo liweke hapa jukwaani.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…