DAVID KAFULILA amekosa heshima kwa Watanzania

DAVID KAFULILA amekosa heshima kwa Watanzania

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,610
Bwana David Zachary Kafulila ameamua kutoshiriki vikao vya bunge maalum la katiba kwa makusudi kabisa, hilo ni tusi kwa watanzania.

Toka tarehe 17/02/2014, David Kafulila ameanza kusoma Masters ya International Business Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (full time) na alianza kuonekana eneo la chuo kikuu toka mwezi wa kwanza pale alipokuwa akifatilia admission letter. Hivyo Kafulila kwa mapenzi yake, utashi wake na dharau zake kwa watanzania ameamua kutohudhuria vikao vya bunge maalum la katiba.

Naomba Kafulila anijibu maswali haya
1. kwanini hutaki kuhudhuria vikao vya bunge maalumu katiba?
2. unataka wananchi wakuelewe vipi, hasa wa kigoma?
3. ina maana katiba si jambo muhimu kwako?
4. wananchi wa kigoma wakikuadhibu 2015 katika uchaguzi mkuu unadhani watakuwa na makosa?
NAWASILISHA
 
Nenda kwake kaongee naye mada zingine kama za walevi vile.
 
Mbona ktk vikao vya awali alikua anahudhuria, tena alikua mchangiaji mzuri tu. Halafu Bunge hili la katiba linawatu wengi sana lakini mahudhurio hafifu, je umewaandika na wengine wasio hudhuria?
 
Huyo kafulila ni muhuni tu. Anarafuta umaarufu tu. Katiba si kitu cha kuletea upuuzi upuuzi.
 
Sasa kama tarehe ya kuanza kusoma imeangukia hiyo tarehe uliyosema unataka ahairishe?? Ishike sana elimu asipotee!!! Soma mbunge, bunge atalikuta tu. Opportunity never comes twice.
 
Kafulila wakora walikusema sana wewe form six huna degree naona umeamua kukata mzizi wa fitna kwa kukamata na Masters kabisaaa huku wachongaji wakibaki na degree zetu zileeeee za tia maji tia maji!
 
Wabongo bana kila siku mnampigia Mnyika kelele arudi shule leo Kafulila karudi shule mnamsema na huyo Mnyika angeamua kufata ushaur wenu si mngemsema. Hamueleweki kama k ya Nyani
 
Wabongo bana kila siku mnamoigia Mnyika kelele arudi shule leo Kafulila karudi shule mnamsema na huyo Mnyika angeamua kufata ushaur wenu si mngemsema. Hamueleweki kama k ya Nyani
umenena vizuri sana qeen of sheba, lakini unafanana na jina lako queen? Mfalme sulemani aliishiwa nguvu kabisa wakati huo...labda nimechanganya...yawezekana ni cleopatra ....
 
Bwana David Zachary Kafulila ameamua kutoshiriki vikao vya bunge maalum la katiba kwa makusudi kabisa, hilo ni tusi kwa watanzania.

Toka tarehe 17/02/2014, David Kafulila ameanza kusoma Masters ya International Business Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (full time) na alianza kuonekana eneo la chuo kikuu toka mwezi wa kwanza pale alipokuwa akifatilia admission letter. Hivyo Kafulila kwa mapenzi yake, utashi wake na dharau zake kwa watanzania ameamua kutohudhuria vikao vya bunge maalum la katiba.

Naomba Kafulila anijibu maswali haya
1. kwanini hutaki kuhudhuria vikao vya bunge maalumu katiba?
2. unataka wananchi wakuelewe vipi, hasa wa kigoma?
3. ina maana katiba si jambo muhimu kwako?
4. wananchi wa kigoma wakikuadhibu 2015 katika uchaguzi mkuu unadhani watakuwa na makosa?
NAWASILISHA

Kafulila anajitambua sana ndio maana ameamua kuacha posho na kwenda kuongeza masomo.wewe unafikiri ubunge ni wa maisha? Au unafurahishwa na wabunge wa ndio ndio bungeni ambao kila hoja kwao ni 100%?
 
Bora yeye amaeamua kwenda kusoma, kuna wengine walikatisha ziara za kibunge na kwenda kujirusha DUBAI.
 
Back
Top Bottom