David Kafulila anakumbukwa na wakulima wa Simiyu kwa kupaisha bei ya Pamba kufikia Tsh. 2200 kwa kilo katika historia ya Taifa letu alipokuwa RC

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Uongozi ni kuacha alama zinazoishi katika Maisha na mioyo ya watu, ni kuacha kitu kitakacho simuliwa vizazi kwa vizazi,ni kuacha rekodi ambayo itaimbwa na kuzungumzwa na watu kwa miaka mingi hata kama wewe utakuwa haupo uongozini au Duniani lakini utaendelea kuishi na watu japo hupo Duniani au madarakani.

Uongozi siyo habari ya umeongoza miaka mingapi au umekaa miaka mingapi. kinachomfanya mtu akakumbukwa na watu ni kazi alizozifanya kwa muda alipokuwa na madaraka au hai na faida ya uhai wake kwa watu na uongozi wake ulivyogusa maisha ya watu.

Ndio maana leo hii viongozi na watu kama John F Kennedy, Dr Martin Luther King Junior, BoB Marely, Abraham Lincolin wanaendelea kukumbukwa na watu wengi sana Duniani kwote licha ya kwamba walikufa miaka mingi na waliishi miaka michache Duniani kabla ya kufikia uzee wao. Ndio maana pia viongozi kama Edward Moringe Sokoine wanakumbukwa na Taifa letu japo walikaa madarakani kwa Muda mfupi lakini historia zao na majina yao yameganda na kunasa katika mioyo ya watanzania kutokana na mikono yao na kazi zao kugusa maisha ya watu na kuleta matokeo Chanya.

Hii maana yake nini? Unaweza kuongoza kwa miaka mingi, kukaa madarakani au kwenye cheo fulani kwa miaka mingi na bado usikumbukwe na yeyote yule pale ambapo utaondoka leo. Unaweza kuondoka leo kwenye ukuu wa mkoa au uwaziri au uwaziri mkuu au uspika au ukurugenzi wa taasisi fulani halafu kesho watu wakasahau kabisa kama ulikuwepo kwenye nafasi fulani. Kwanini? Kwa sababu uongozi wako na uwepo wako kwenye kiti haukugusa wala kubadilisha maisha ya watu au mtu yeyote yule, kwa hiyo ulikuwa kama mvuke au moshi tu ambao umekuja na kupita.

Mheshimiwa David Kafulila licha ya kukaa katika nafasi ya Ukuu wa mkoa Wa Simiyu kwa muda mfupi lakini bado anaendelea kukumbukwa na wana Simiyu kama mkuu wa mkoa aliyeleta tabasamu, furaha, matumaini na kuwainua kiuchumi kwa kupaisha Bei ya pamba yao ambayo kwa karibu 70% ya pamba yote Tanzania inatokea Simiyu kufikia bei ya 2200 kwa kilo, bei ambayo haikuwa kutokea tangia Nchi yetu ipate uhuru. Leo anakumbukwa na kusemwa kuwa hapa Simiyu kilipita na kulipita CHUMA David Kafulila aliyeleta Nuru kwa wakulima na maendeleo kwa kaya za wanasimiyu.

Jiulize wewe kiongozi uliyepo kwenye cheo fulani au wadhifa fulani ukiondoka leo kwenye nafasi uliyopo watu watakukumbuka kwa lipi? Umegusa maisha ya watu wangapi? Umeleta tabasamu kwa kaya ngapi? Wangapi wamepata nuru kutoka gizani? Wangapi wamepata matumaini kupitia mikono yako? Wangapi wanatamani urejee au urudishwe au uongezewe muda au kukuombea dua na maombi mema ya kurejea au kupata cheo kikubwa au nafasi fulani? Utakumbukwa kwa lipi ndugu yangu? Au unaisha na kufanya kazi ilimradi tu watoto wako wapate ugali mezani? Umebadilisha maisha ya wangapi?

Wangapi wanaona uwepo wako hapo ulipo ni baraka na mlango wa wao kutokea kimaisha na kuinuka kiuchumi? Wangapi wanakukumbuka kwa mema?

Gusa maisha ya watu, Leta tabasamu kwa watu,washa taa kwenye mioyo ya watu,inua watu,shika mikono ya watu uwainue juu,wape matumaini watu ili siku moja Ukumbukwe kama ilivyo kwa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere,Nelson Mandela,kwame Nkrumah, Keneth Kaunda, Winnie Mandela na wengine wengi sana. Lakini pia ukifanya vyema utaungwa mkono ukiwa bado hai kama ilivyo kwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Unamsifia hivo Kwa mbwembwembwe na uongo mwanaume mwenzio.
Mbona unatupa wasiwasi dogo
Ilitakiwa uonyeshe kwa hoja nzito na zenye ushahidi kiwa ni wapi nimepotosha.Unabisha kuwa pamba haikuuzwa 2200 kwa kilo wakati Mheshimiwa Kafulila akiwa mkuu wa mkoa? Je wakulima wamewahi kuuza kwa bei hiyo kabla ya Mh Kafulila kufika?
 
Ilitakiwa uonyeshe kwa hoja nzito na zenye ushahidi kiwa ni wapi nimepotosha.Unabisha kuwa pamba haikuuzwa 2200 kwa kilo wakati Mheshimiwa Kafulila akiwa mkuu wa mkoa? Je wakulima wamewahi kuuza kwa bei hiyo kabla ya Mh Kafulila kufika?
Kwaiyo amekufurahisha?
 
Sijatembea maeneo mengi ya nchi hii ila kwa yale machache niliyofika Simiyu ni moja wapo, Simiyu ni sehemu ambayo mkulima wa pamba, mahindi, alizeti, choroko,dengu, mbaazi na mtama mwekundu anahitaji msaada mkubwa sana kwenye swala la bei, wakulima hawa wanalima kwa moyo sana ila linapokuja swala la bei ni huruma tupu hakuna wanachotaka bei niza chini sana. Ushirika inabidi upewe nguvu sana ili mkulima apate bei nzuri,vyama vya ushirika ambavyo vipochini ya chama kikuu vina hali mbaya sana,
 
Kafulila tumemchoka na tabia yake ya kulipa watu Ili wamsemee mitandaoni.

Na wewe Dalali punguza njaa itakuponza. Siyo wanaume wote wanaokutumia Wana Nia njema!! Ukishaona wanaanza kukulipia na Kodi ya nyumba basi jiandae kuanza kupika na kufua nguo zao
 
Nakuunga mkono na naamini wahusika wanapaswa kuchukua na kupokea ushauri wako.
 
Nakuunga mkono na naamini wahusika wanapaswa kuchukua na kupokea ushauri wako.
 
Naona wivu na ile roho yako ya Wivu bado inaendelea kukusumbua kila uchwao. Hilo ni pepo linalotakiwa kuombewa na kukemewa. Nenda ukapate maombi kwa watumishi wa Mungu. Fanya vyema nawewe usifiwe na kupongezwa badala ya kuwa na wivu na chuki binafsi kwa wachapa kazi na WAZALENDO aina ya Mheshimiwa Kafulila.
 
Bei ya pamba haipangwi na Mkuu wa Mkoa wewe chawa mchafu
Unafahamu kuna wakulima walikuwa wanakopwa Pamba zao lakini Mheshimiwa Kafulila alipiga marufuku na hata bei pia aliifanya hivyo baada ya kuona bei ilivyo kwenye soko la DUNIA,lakini baadhi ya wafanyabiashara wakawa wanataka kununua kwa bei ya chini? Mara ngapi tumeona hata serikali ikiwakemea wafanyabiashara wa mazao fulani kununua kwa bei fulani baada ya kugundua wananunua kwa bei ya chini?
 
Bei ya pamba haipangwi na Mkuu wa Mkoa wewe chawa mchafu
Kwa yoyote anayehusika na kupanga wajaribu kuliangalia hili swala la bei, kwa sasa hivi maeneo ya mwandoya wageni ni wengi, gesti zinajaa maeneo ya vyakula watu wanafanya bishara ukiuliza utaambiwa wamekuja kununua pamba, kwa nini bei isipande ili mkulima apate angalau kifuta jasho??
 
Nakukumbusha Tena, Pamba inalimwa nchi nzima na Bei yake hutangazwa na Bodi ya Pamba Tanzania.

Huyo shoga yako Kafulila hajawahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanzania nzima. Kaa chini utafakari na Kisha jisahihishe. Wewe ni mwanaume pengine una mke na watoto, andika vitu ambavyo una uelewa navyo.

Mara nyingi huwa nakuunga mkono, lakini Kwa hili la kuwapigia debe wanaotaka madaraka Kwa njia za kipumbavu Sikuungi mkono. Tumbo linakudhalilisha
 
Wewe una hoja nzuri. Siyo yule chawa
 
Bei ya pamba haipangwi na Mkuu wa Mkoa wewe chawa mchafu
Unajua mamlaka aliyonayo Mkuu wa Mkoa?
Mkuu wa Mkoa ni Rais wa Mkoa,
Sasa kama Pamba ilitoka kuuzwa TZS 800 hadi 2,200 na Leo hayupo bei ni 1,000 why tusiamini Kuna uhuni kule wakulima wanafanyiwa?
 
Ngoja Nikufumbue tu akili yako hiyo . Ni kuwa ningependa kukwambia ya kuwa 70% ya pamba yote unayoiona hapa Tanzania inatokea Mkoani Simiyu.
 
Unajua mamlaka aliyonayo Mkuu wa Mkoa?
Mkuu wa Mkoa ni Rais wa Mkoa,
Sasa kama Pamba ilitoka kuuzwa TZS 800 hadi 2,200 na Leo hayupo bei ni 1,000 why tusiamini Kuna uhuni kule wakulima wanafanyiwa?
Huyo hawezi kuelewa unachomueleza maana akili yake imepofushwa na wivu na chuki binafsi.
 
Soma vizuri siumeambiwa Simiyu Pamba ni 70%
Ila ni kweli Kafulila aliwabana walanguzi bei ikafika 2,200
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…