David Kafulila atolea ufafanuzi wa Adani kuwekeza katika Miundombinu ya Umeme kwa Ubia

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Kampuni mbili kubwa, Adani Group ya India na Gridworks Development Partners LLP ya Uingereza, zimeonesha nia ya kuwekeza katika mradi wa kusafirisha umeme nchini Tanzania kupitia mfumo wa ubia. Mradi huo unalenga kujenga njia za kusafirisha umeme wa juu kwa lengo la kuboresha miundombinu ya nishati nchini Tanzania.

Akizungumza kwa njia ya simu na Jambo TV, David Kafulila, Kamishna wa Ubia wa Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), amefafanua kuwa utaratibu huo unajulikana kama "expression of interests,"ambapo wawekezaji wanaweza kueleza nia yao ya kuwekeza kwenye miradi kwa kushirikiana na serikali.

"Kampuni (Wawekezaji) mbili ambazo zimeomba kufanya mradi wa kusafirisha umeme kwa utaratibu wa ubia, inaitwa expression of interests yaani kwamba inaruhusu mwekezaji kueleza nia yake ya kuwekeza kwenye mradi fulani katika utaratibu wa ubia na serikali" ameeleza Kafulila.

Kafulila ameeleza zaidi kuwa sheria za ubia nchini Tanzania zinaruhusu kampuni kuwasilisha maombi yao kwa hatua za awali, na serikali inaweza kuamua kuitangaza miradi hiyo kwa kampuni zingine kushindana ili kuhakikisha uwazi na ufanisi. Hivi sasa, Adani na Gridworks ndio kampuni mbili zilizowasilisha maombi ya kuwekeza katika mradi huo wa kusafirisha umeme.

Ameongeza kuwa zipo njia nne zinazotumika kuingia kwenye ubia wa umma na binafsi nchini Tanzania. Njia hizo ni pamoja na serikali kutangaza mradi na kuruhusu ushindani (Solicited), mwekezaji kuomba kuandaa mradi (Unsolicited), serikali kutafuta mwekezaji wa moja kwa moja wa haraka hasa baada ya kuwa tayari imeandaa mradi (Direct Negotiation), na ya utaratibu maalum (Special Arrangement). Katika kesi ya Adani na Gridworks, wameomba kuwekeza kupitia njia ya kusudio la mwekezaji (Unsolicited).

Kafulila amesisitiza kuwa maombi yaliyotolewa na Adani na Gridworks ni hatua ya awali, na michakato ya kuchunguza kama kampuni hizo zina sifa stahiki itaendelea. Serikali kupitia TANESCO itazingatia mahitaji ya mradi huo na kuamua kama kutangaza zabuni kwa kampuni zingine au kuendelea na kati ya waombaji wa sasa.

"Adani ameleta kusudio awekeze, ni hatua ya awali ya kueleza kusudio, na siyo Adani peke yake ambayo imeomba iwekeze, sasa baadaye kwa mujibu wa sheria TANESCO sasa inaweza ikaamua kutangaza na kampuni zote ambazo zinahitaji zikashindana kutegemea mahitaji yake kwa wakati huo. Sasa hiyo iliyofanyika ya Adani na Kampuni nyingine ya Uingereza ya Gridworks Development Partners LLP, ni kampuni mbili ambazo zimeomba kuwekeza, na sheria inawaruhusu kuomba. Sasa ukiomba, ndiyo michakato inaanza ya kama una sifa au hauna sifa", ameeleza Kafulila.

Adani Group, kampuni inayoongozwa na bilionea Gautam Adani, imekuwa ikiongeza uwepo wake katika ukanda wa Afrika Mashariki, huku Tanzania ikiwa sehemu ya mikakati yao ya kuimarisha miundombinu ya nishati kupitia mradi unaotajwa kuwa na thamani ya takriban dola milioni 900. Tanzania pia iko kwenye mazungumzo na Gridworks Development Partners kuhusu mradi wa dola milioni 300.

Kwa upande wake, Tanzania imeweka kipaumbele katika kuboresha miundombinu ya nishati ili kukidhi mahitaji ya umeme yanayoendelea kuongezeka, hatua inayosaidiwa na miradi kama hii ya ubia. Ushirikiano huu pia ni muhimu kwa kuboresha mfumo wa usafirishaji wa umeme wa juu nchini.
Screenshot_20241005-173231_1.jpg
 
Tuanzie hapa
Sie tumefeli wapi hadi tutake ubia. Maana uzalishaji tumefanikiwa , je usambazaji tunahitaji a complete overhaul ya haraka hadi tuhitaji usd 900 mio. Je hatuwezi kwenda kwa awamu na huku tukiendelea kutoa huduma hii public goods. Hawa jamaa wanaweza kuingia kwenye procurement kama wauzaji tu sio waendeshaji. Imagine nguzo , chuma ya liganga na cement za nguzo ipo , nguzo mufindi na transformer zatengenezwa kigamboni
 
Aidani Hawa ndio wametaka Kununua Airport ya Kenya mpaka wakenya waka undergo Strike
Kinachoangaliwa na kuzingatiwa na tunachopaswa kuzingatia ni mkataba wenye maslahi kwetu kama Taifa.na siyo habari za kuangalia nini kilitokea kenya.sisi ndio wenye Nchi na tunayo nafasi na uhuru wa kumwambia muwekezaji juu ya kile ambacho tungependa afanye na kutekeleza. Nafikiri umesoma namna Mheshimiwa David Kafulila alivyo toa maelezo mazuri na ya kina. Kwamba ikionekana hajakidhi vigezo basi watachukua hatua zingine.
 
expression of interests,"ambapo wawekezaji wanaweza kueleza nia yao ya kuwekeza kwenye miradi kwa kushirikiana na serikali.
Expression of interests siyo sealed deal, na sioni haja ya serikali kuitangaza. Kwasabb hii ni sawa na mwanaume amsifie binti halafu babake aanze kuwaambia majirani kuwa binti yangu ataolewa na fulani (mwanaume aliyemsifia). Ni ujinga.
 
Ridiculous.

Wanachokuja kuwekeza ni nini wakati Nchi imesha wekeza matrilioni ya fedha humo?

Ni nini haswa hawa wawekezaji wanaleta ambacho hakipo kwenye huo mfumo wa Usambazaji wa Umeme?

Itoshe, nilishasema hapa wakati tunailalamikia serikali na Uwekezaji wa DP World Bandarini.

Ukoloni mamboleo is Real.

=========
Hatahivyo. Kuna shida gani wakipewa kampuni za wazawa kufanya 'Distribution"?
 
Tuanzie hapa
Sie tumefeli wapi hadi tutake ubia. Maana uzalishaji tumefanikiwa , je usambazaji tunahitaji a comple overhaul ya haraka had tuhitaji usd 900 mio. Je hatuwezi kendal kwa phases na huku tukiendelea kutoa huduma public goos. Hawa jamaa wanaweza kuingia kwenye procurement kama wauzaji tu sio waendeshaji. Imagine nguzo , chuma liganga na cement za nguzo mufindi na transformer kigamboni
Mheshimiwa Kafulila alishatoa ufafanuzi sana na kueleza sana juu ya faida na umuhimu wa kufanya miradi kwa mfumo wa ubia.kwa sababu mfumo huu unaipunguzia mzigo wa gharama serikali kwa kukomba pesa zote za walipa kodi.Mfumo huu wa ubia unasaidia kuipunguzia gharama serikali na kuipa uhuru wa kufanya mambo mengine mbalimbali ya kimaendeleo kuliko kama ingetoa pesa zote mabilioni kwa mabilioni na kuweka eneo moja tu.
 
Tuanzie hapa
Sie tumefeli wapi hadi tutake ubia. Maana uzalishaji tumefanikiwa , je usambazaji tunahitaji a comple overhaul ya haraka had tuhitaji usd 900 mio. Je hatuwezi kendal kwa phases na huku tukiendelea kutoa huduma public goos. Hawa jamaa wanaweza kuingia kwenye procurement kama wauzaji tu sio waendeshaji. Imagine nguzo , chuma liganga na cement za nguzo mufindi na transformer kigamboni
Acha wanaume wachapakazi wawekeze tupate umeme wa bila tatizo. Hawa Tanesco waliisha oza
 
Expression of interests siyo sealed deal, na sioni haaja ya serikali kuitangaza. Kwasabb hii ni sawa na mwanaume amsifie binti halafu babake aaanze kuwaambia majira I kuwa binti yangu ataolewa na fulani (mwanaume aliyemsifia). Ni ujinga.
Kipi ambacho hujaelewa katika maelezo hayo mazuri yaliyotolewa na Mheshimiwa David Kafulila
 
Ridiculous.

Wanachokuja kuwekeza ni nini wakati Nchi imesha wekeza matrilioni ya fedha humo?

Ni nini haswa hawa wawekezaji wanaleta ambacho hakipo kwenye huo mfumo wa Usambazaji wa Umeme?

Itoshe, nilishasema hapa wakati tunailalamikia serikali na Uwekezaji wa DP World Bandarini.

Ukoloni mamboleo is Real.

=========
Hatahivyo. Kuna shida gani wakipewa kampuni za wazawa kufanya 'Distribution"?
Acha uoga ndugu yangu mtanzania.
 
Expression of interests siyo sealed deal, na sioni haaja ya serikali kuitangaza. Kwasabb hii ni sawa na mwanaume amsifie binti halafu babake aaanze kuwaambia majira I kuwa binti yangu ataolewa na fulani (mwanaume aliyemsifia). Ni ujinga.
Uko sahihi vitu vingine vinatakiwa kutangazwa vikiwa vimeiva sioni sababu ya kuanza kutangaza expression of interest za watu mapema hivi

Ilitakiwa kuwa confidential mpaka pale serikali itakapoonyesga kuwa ina uhitaji watu wakete expression of interest zao

Sijaekewa kisa cha Kafulila kuanza ku wa expose mapema namna hii wakati serikali yenyewe haijaonyesha uhitaji eneo hilo

Lengo lake la kubwa expose ni nini hasa?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kampuni mbili kubwa, Adani Group ya India na Gridworks Development Partners LLP ya Uingereza, zimeonesha nia ya kuwekeza katika mradi wa kusafirisha umeme nchini Tanzania kupitia mfumo wa ubia. Mradi huo unalenga kujenga njia za kusafirisha umeme wa juu kwa lengo la kuboresha miundombinu ya nishati nchini Tanzania.

Akizungumza kwa njia ya simu na Jambo TV, David Kafulila, Kamishna wa Ubia wa Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), amefafanua kuwa utaratibu huo unajulikana kama "expression of interests,"ambapo wawekezaji wanaweza kueleza nia yao ya kuwekeza kwenye miradi kwa kushirikiana na serikali.

"Kampuni (Wawekezaji) mbili ambazo zimeomba kufanya mradi wa kusafirisha umeme kwa utaratibu wa ubia, inaitwa expression of interests yaani kwamba inaruhusu mwekezaji kueleza nia yake ya kuwekeza kwenye mradi fulani katika utaratibu wa ubia na serikali" ameeleza Kafulila.

Kafulila ameeleza zaidi kuwa sheria za ubia nchini Tanzania zinaruhusu kampuni kuwasilisha maombi yao kwa hatua za awali, na serikali inaweza kuamua kuitangaza miradi hiyo kwa kampuni zingine kushindana ili kuhakikisha uwazi na ufanisi. Hivi sasa, Adani na Gridworks ndio kampuni mbili zilizowasilisha maombi ya kuwekeza katika mradi huo wa kusafirisha umeme.

Ameongeza kuwa zipo njia nne zinazotumika kuingia kwenye ubia wa umma na binafsi nchini Tanzania. Njia hizo ni pamoja na serikali kutangaza mradi na kuruhusu ushindani (Solicited), mwekezaji kuomba kuandaa mradi (Unsolicited), serikali kutafuta mwekezaji wa moja kwa moja wa haraka hasa baada ya kuwa tayari imeandaa mradi (Direct Negotiation), na ya utaratibu maalum (Special Arrangement). Katika kesi ya Adani na Gridworks, wameomba kuwekeza kupitia njia ya kusudio la mwekezaji (Unsolicited).

Kafulila amesisitiza kuwa maombi yaliyotolewa na Adani na Gridworks ni hatua ya awali, na michakato ya kuchunguza kama kampuni hizo zina sifa stahiki itaendelea. Serikali kupitia TANESCO itazingatia mahitaji ya mradi huo na kuamua kama kutangaza zabuni kwa kampuni zingine au kuendelea na kati ya waombaji wa sasa.

"Adani ameleta kusudio awekeze, ni hatua ya awali ya kueleza kusudio, na siyo Adani peke yake ambayo imeomba iwekeze, sasa baadaye kwa mujibu wa sheria TANESCO sasa inaweza ikaamua kutangaza na kampuni zote ambazo zinahitaji zikashindana kutegemea mahitaji yake kwa wakati huo. Sasa hiyo iliyofanyika ya Adani na Kampuni nyingine ya Uingereza ya Gridworks Development Partners LLP, ni kampuni mbili ambazo zimeomba kuwekeza, na sheria inawaruhusu kuomba. Sasa ukiomba, ndiyo michakato inaanza ya kama una sifa au hauna sifa", ameeleza Kafulila.

Adani Group, kampuni inayoongozwa na bilionea Gautam Adani, imekuwa ikiongeza uwepo wake katika ukanda wa Afrika Mashariki, huku Tanzania ikiwa sehemu ya mikakati yao ya kuimarisha miundombinu ya nishati kupitia mradi unaotajwa kuwa na thamani ya takriban dola milioni 900. Tanzania pia iko kwenye mazungumzo na Gridworks Development Partners kuhusu mradi wa dola milioni 300.

Kwa upande wake, Tanzania imeweka kipaumbele katika kuboresha miundombinu ya nishati ili kukidhi mahitaji ya umeme yanayoendelea kuongezeka, hatua inayosaidiwa na miradi kama hii ya ubia. Ushirikiano huu pia ni muhimu kwa kuboresha mfumo wa usafirishaji wa umeme wa juu nchini.View attachment 3116153
Adani ni kampuni Ile ambayo wanataka kuendesha Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta Nairobi?
 
Hapa kafulila umechemka ,yaani kusafirisha tu serikali kupitia REA hawawezi? Wizzy Wiizy.

Kama DERM ameweza kutengeneza nguzo na kuna kampuni hapa hapa nchini zinatengeneza transforma na nyaya ,kwanini tusiwape hao na serikali iwe inawalipa kidogo kidogo kuliko kwenda kumpa muhindi aliyefukuzwa kenya kuja kutupiga kama HABINDA SINGI?
 
Hapa kafulila umechemka ,yaani kusafirisha tu serikali kupitia REA hawawezi? Wizzy Wiizy.
Amechemka vipi ndugu yangu mtanzania.ulitakiwa ueleze kwa hoja. Hata hivyo Mheshimiwa David Kafulila ametoa maelezo yaliyonyooka kabisa na ya kueleweka vyema. amesema kuwa hiyo ni hatua ya awali kabisa ambapo baadaye serikali itakaa na kuchambua maombi yao na kama wanastahili kupewa mradi huo.
 
Uko sahihi vitu vingine vinatakiwa kutangazwa vikiwa vimeiva s9oni sababu ya kuanza kutangaza expression of interest za watu mapema hivi

Ilitakiwa kuwa confidential mpaka pale serikali itakapoonyesga kuwa ina uhitaji watu wakete expression of interest zao

Sijaekewa kisa cha Kafulila kuanza ku wa expose mapema namna hii wakati serikali yenyewe haijaonyesha uhitaji eneo hilo

Lengo lake la kubwa expose ni nini hasa?
Hiyo ni biashara na hakuna uhitaji wa siri. Ndio maana Mheshimiwa Kafulila amesema kuwa ikionekana kuwa kampuni hizo hazikidhi vigezo na mahitaji ya serikali.basi hatua za kutangaza zaidi tenda hiyo itafanyika ili kuruhusu ushindani zaidi na kumpata mtu sahihi na mwenye kukidhi matarajio ya serikali.
 
Tegeta Escrow is loading............................
Siyo kweli.haya mambo ni ya wazi na siyo siri .na ndio maana hapo kila kitu kipo wazi hadi kiasi cha pesa .hata hivyo ningependa kukwambia kuwa Mheshimiwa kafulia ni mtu muadilifu na Mzalendo asiyetiliwa mashaka na mtanzania yeyote yule .Au umesahau mambo makubwa aliyosimamia katika Taifa hili? Umesahau misimamo yake ya kizalendo na yenye maslahi kwa Taifa letu?
 
Back
Top Bottom