Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa mabadiliko ya tabia ya nchi yanayoendelea kuikumba Dunia nzima ni muhimu kuendelea kuwekeza katika vyanzo mbalimbali vya nishati hii kama ambavyo serikali yetu imekuwa ikifanya . Ndio maana tunaendelea kuwekeza katika umeme wa maji,gas,jua,upepo n.k.ili ikitokea tumekwama Sehemu basi Taifa lisiingie gizani.Fursa iliyopo ni umeme wa jua au upepo...Tutashukuru sana wakija kuwekeza kwenye maeneo hayo
Kwani alifanya kwa upendo au alifanya kwa sababu analipwa mshahara!?! Sio uzalendo! Anajua kuwa anapewa kibunda chake!Siyo kweli.haya mambo ni ya wazi na siyo siri .na ndio maana hapo kila kitu kipo wazi hadi kiasi cha pesa .hata hivyo ningependa kukwambia kuwa Mheshimiwa kafulia ni mtu muadilifu na Mzalendo asiyetiliwa mashaka na mtanzania yeyote yule .Au umesahau mambo makubwa aliyosimamia katika Taifa hili? Umesahau misimamo yake ya kizalendo na yenye maslahi kwa Taifa letu?
Ondoa wasiwasi wako.Skendo ya umeme nyingine kwa badaye
Ova
Amekuwa akifanya kwa uzalendo wa dhati kwa Taifa letu.Kwani alifanya kwa upendo au alifanya kwa sababu analipwa mshahara!?! Sio uzalendo! Anajua kuwa anapewa kibunda chake!
Ahh Mkuu kwamba unataka kusema ukitoa mshahara wake na pesa zingine bado atafanya kazi?! Au unamzungumzia Kafulila yupi!?Amekuwa akifanya kwa uzalendo wa dhati kwa Taifa letu.
Escrow part IISkendo ya umeme nyingine kwa badaye
Ova
Ndugu zangu Watanzania,
Kampuni mbili kubwa, Adani Group ya India na Gridworks Development Partners LLP ya Uingereza, zimeonesha nia ya kuwekeza katika mradi wa kusafirisha umeme nchini Tanzania kupitia mfumo wa ubia. Mradi huo unalenga kujenga njia za kusafirisha umeme wa juu kwa lengo la kuboresha miundombinu ya nishati nchini Tanzania.
Akizungumza kwa njia ya simu na Jambo TV, David Kafulila, Kamishna wa Ubia wa Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), amefafanua kuwa utaratibu huo unajulikana kama "expression of interests,"ambapo wawekezaji wanaweza kueleza nia yao ya kuwekeza kwenye miradi kwa kushirikiana na serikali.
"Kampuni (Wawekezaji) mbili ambazo zimeomba kufanya mradi wa kusafirisha umeme kwa utaratibu wa ubia, inaitwa expression of interests yaani kwamba inaruhusu mwekezaji kueleza nia yake ya kuwekeza kwenye mradi fulani katika utaratibu wa ubia na serikali" ameeleza Kafulila.
Kafulila ameeleza zaidi kuwa sheria za ubia nchini Tanzania zinaruhusu kampuni kuwasilisha maombi yao kwa hatua za awali, na serikali inaweza kuamua kuitangaza miradi hiyo kwa kampuni zingine kushindana ili kuhakikisha uwazi na ufanisi. Hivi sasa, Adani na Gridworks ndio kampuni mbili zilizowasilisha maombi ya kuwekeza katika mradi huo wa kusafirisha umeme.
Ameongeza kuwa zipo njia nne zinazotumika kuingia kwenye ubia wa umma na binafsi nchini Tanzania. Njia hizo ni pamoja na serikali kutangaza mradi na kuruhusu ushindani (Solicited), mwekezaji kuomba kuandaa mradi (Unsolicited), serikali kutafuta mwekezaji wa moja kwa moja wa haraka hasa baada ya kuwa tayari imeandaa mradi (Direct Negotiation), na ya utaratibu maalum (Special Arrangement). Katika kesi ya Adani na Gridworks, wameomba kuwekeza kupitia njia ya kusudio la mwekezaji (Unsolicited).
Kafulila amesisitiza kuwa maombi yaliyotolewa na Adani na Gridworks ni hatua ya awali, na michakato ya kuchunguza kama kampuni hizo zina sifa stahiki itaendelea. Serikali kupitia TANESCO itazingatia mahitaji ya mradi huo na kuamua kama kutangaza zabuni kwa kampuni zingine au kuendelea na kati ya waombaji wa sasa.
"Adani ameleta kusudio awekeze, ni hatua ya awali ya kueleza kusudio, na siyo Adani peke yake ambayo imeomba iwekeze, sasa baadaye kwa mujibu wa sheria TANESCO sasa inaweza ikaamua kutangaza na kampuni zote ambazo zinahitaji zikashindana kutegemea mahitaji yake kwa wakati huo. Sasa hiyo iliyofanyika ya Adani na Kampuni nyingine ya Uingereza ya Gridworks Development Partners LLP, ni kampuni mbili ambazo zimeomba kuwekeza, na sheria inawaruhusu kuomba. Sasa ukiomba, ndiyo michakato inaanza ya kama una sifa au hauna sifa", ameeleza Kafulila.
Adani Group, kampuni inayoongozwa na bilionea Gautam Adani, imekuwa ikiongeza uwepo wake katika ukanda wa Afrika Mashariki, huku Tanzania ikiwa sehemu ya mikakati yao ya kuimarisha miundombinu ya nishati kupitia mradi unaotajwa kuwa na thamani ya takriban dola milioni 900. Tanzania pia iko kwenye mazungumzo na Gridworks Development Partners kuhusu mradi wa dola milioni 300.
Kwa upande wake, Tanzania imeweka kipaumbele katika kuboresha miundombinu ya nishati ili kukidhi mahitaji ya umeme yanayoendelea kuongezeka, hatua inayosaidiwa na miradi kama hii ya ubia. Ushirikiano huu pia ni muhimu kwa kuboresha mfumo wa usafirishaji wa umeme wa juu nchini.View attachment 3116153
Na hii ndo shida ambayo viongozi wengi wanaiona ila hawataki kuionesha! Hapo tutegemee bei kuruka juu zaidi.Tatizo na kukurupuka ni ujinga nchi kuwekeza kwenye usambazaji maana huwezi kufuta mikataba ya hivi . Uwekezaji ni kwenye uzalishaji ! Yaani mwekezaji akikuwekea waya kwenye kijiji bei haitaweza kushuka ni wizi ndiyo maana Tanesco inatakiwa kumiliki usambazaji na kuruhuru uwekezaji kwenye uzalishaji. Tusikubali huu uwekezaji hauna manufaa.
Ndio atafanya vyema kabisa bila shida wala kuhitaji malipo. Hivi unafahamu mwalimu Nyerere aliacha kazi ya ualimu iliyokuwa ikimpatia mshahara nakwenda kufanya kazi ya kujitolea kwa ajili ya kutafuta uhuru wa Nchi hii? Sasa huyo ndio role model wakeAhh Mkuu kwamba unataka kusema ukitoa mshahara wake na pesa zingine bado atafanya kazi?! Au unamzungumzia Kafulila yupi!?
Hatuleti muwekezaji kama Taifa kuja kuongeza bei bali kuja kushusha bei na kurahisisha maisha ya watanzania, hususani kipindi hiki ambacho Mheshimiwa Rais anapambana kuhakikisha watanzania tunatumia nishati safi kwa ajili kupikiaNa hii ndo shida ambayo viongozi wengi wanaiona ila hawataki kuionesha! Hapo tutegemee bei kuruka juu zaidi.
Hapi hakuna bishara ni sawa na mtu kuomba kazi ambayo haipo jalafu unatoka hadharani kutangaza kuwa nafasi ya kazi fulani wameomba watu elfu 10 wakati hiyo kazi haipo!Hiyo ni biashara na hakuna uhitaji wa siri. Ndio maana Mheshimiwa Kafulila amesema kuwa ikionekana kuwa kampuni hizo hazikidhi vigezo na mahitaji ya serikali.basi hatua za kutangaza zaidi tenda hiyo itafanyika ili kuruhusu ushindani zaidi na kumpata mtu sahihi na mwenye kukidhi matarajio ya serikali.
Duuh Mkuu! Mbona hapo maji marefu sana yaani Mwalimu ndo role model wa Kafulila!?? Serious kabsaNdio atafanya vyema kabisa bila shida wala kuhitaji malipo. Hivi unafahamu mwalimu Nyerere aliacha kazi ya ualimu iliyokuwa ikimpatia mshahara nakwenda kufanya kazi ya kujitokea kwa ajili ya kutafuta uhuru wa Nchi hii? Sasa huyo ndio role model wake
Mapambio yaendelee!Hatuleti muwekezaji kama Taifa kuja kuongeza bei bali kuja kushusha bei na kurahisisha maisha ya watanzania, hususani kipindi hiki ambacho Mheshimiwa Rais anapambana kuhakikisha watanzania tunatumia nishati safi kwa ajili kupikia
Mheshimiwa Kafulila ni Mwanafunzi mtiifu wa Mwalimu Nyerere aliyewataka vijana kuwa waadilifu , wachapakazi na wazalendo kwa Taifa letu.Duuh Mkuu! Mbona hapo maji marefu sana yaani Mwalimu ndo role model wa Kafulila!?? Serious kabsa
Mimi sipigi mapambio bali naongea ukweli.Mapambio yaendelee!
Acha matusi yako .kama hujasoma andiko na kuelewa ni bora ukaomba usomewe na ueleweshwe. Mheshimiwa Kafulila amefafanua vizuri sana na kwa hoja.Hapi hakuna bishara ni sawa na mtu kuomba kazi ambayo haipo jalafu unatoka hadharani kutangaza kuwa nafasi ya kazi fulani wameomba watu elfu 10 wakati hiyo kazi haipo!
Kafulila mjinga sana kwa hilo aweza iingiza serikali matatani kisheria
Kutangaza majina ya watu walioonyesha expression of interest huwa mchakato unakuwa umeshapitiwa na kamati mbalimbali na serikali kuridhia ndipo ubatoka hadharani kutamka
Biashara haipo halafu unatoka hadharani kutangaza kuwa fulani na fulani wameomba tenda ya biashara ambayo haipo kwa wakati huo nini hicho?