David Kafulila atolea ufafanuzi wa Adani kuwekeza katika Miundombinu ya Umeme kwa Ubia

David Kafulila atolea ufafanuzi wa Adani kuwekeza katika Miundombinu ya Umeme kwa Ubia

Kuna kitu gani Khajibahi anakuja kukifanya ambacho REA hawajakifanya!??

Ghafla amekuwa specialist wa uwekezaji Africa Mashariki. Kuna dalili ya kupata kikohozi, bora niendelee kujiuliza.

Hivi binadamu huwa tunaelewa mida inabadilika? Mbona kama tunafanya mambo yale yale kila siku na kujidanganya hakuna madhara yoyote tunayoweza kupata?

Namalizia kuuliza, hivi nani ni dealer wa beer za Widhoke Tanzania? Hizi bia na pale tulipokuwa tunaenda Jmosi enzi zile, East 24, zinanikumbusha Mzee Maarufu ambaye awamu ya tano, kwa kiasi kikubwa alikuwa amewekwa ndani. Walisema zile deals za kuzalisha umeme zilikuwa na mushkeli. Ukiangalia sana, unashangaa shangaa na kuendelea kushangaa. Nani kasema style ya awamu ya tano haitarudi tena?

Anayedhani amesimama.............................
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kampuni mbili kubwa, Adani Group ya India na Gridworks Development Partners LLP ya Uingereza, zimeonesha nia ya kuwekeza katika mradi wa kusafirisha umeme nchini Tanzania kupitia mfumo wa ubia. Mradi huo unalenga kujenga njia za kusafirisha umeme wa juu kwa lengo la kuboresha miundombinu ya nishati nchini Tanzania.

Akizungumza kwa njia ya simu na Jambo TV, David Kafulila, Kamishna wa Ubia wa Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), amefafanua kuwa utaratibu huo unajulikana kama "expression of interests,"ambapo wawekezaji wanaweza kueleza nia yao ya kuwekeza kwenye miradi kwa kushirikiana na serikali.

"Kampuni (Wawekezaji) mbili ambazo zimeomba kufanya mradi wa kusafirisha umeme kwa utaratibu wa ubia, inaitwa expression of interests yaani kwamba inaruhusu mwekezaji kueleza nia yake ya kuwekeza kwenye mradi fulani katika utaratibu wa ubia na serikali" ameeleza Kafulila.

Kafulila ameeleza zaidi kuwa sheria za ubia nchini Tanzania zinaruhusu kampuni kuwasilisha maombi yao kwa hatua za awali, na serikali inaweza kuamua kuitangaza miradi hiyo kwa kampuni zingine kushindana ili kuhakikisha uwazi na ufanisi. Hivi sasa, Adani na Gridworks ndio kampuni mbili zilizowasilisha maombi ya kuwekeza katika mradi huo wa kusafirisha umeme.

Ameongeza kuwa zipo njia nne zinazotumika kuingia kwenye ubia wa umma na binafsi nchini Tanzania. Njia hizo ni pamoja na serikali kutangaza mradi na kuruhusu ushindani (Solicited), mwekezaji kuomba kuandaa mradi (Unsolicited), serikali kutafuta mwekezaji wa moja kwa moja wa haraka hasa baada ya kuwa tayari imeandaa mradi (Direct Negotiation), na ya utaratibu maalum (Special Arrangement). Katika kesi ya Adani na Gridworks, wameomba kuwekeza kupitia njia ya kusudio la mwekezaji (Unsolicited).

Kafulila amesisitiza kuwa maombi yaliyotolewa na Adani na Gridworks ni hatua ya awali, na michakato ya kuchunguza kama kampuni hizo zina sifa stahiki itaendelea. Serikali kupitia TANESCO itazingatia mahitaji ya mradi huo na kuamua kama kutangaza zabuni kwa kampuni zingine au kuendelea na kati ya waombaji wa sasa.

"Adani ameleta kusudio awekeze, ni hatua ya awali ya kueleza kusudio, na siyo Adani peke yake ambayo imeomba iwekeze, sasa baadaye kwa mujibu wa sheria TANESCO sasa inaweza ikaamua kutangaza na kampuni zote ambazo zinahitaji zikashindana kutegemea mahitaji yake kwa wakati huo. Sasa hiyo iliyofanyika ya Adani na Kampuni nyingine ya Uingereza ya Gridworks Development Partners LLP, ni kampuni mbili ambazo zimeomba kuwekeza, na sheria inawaruhusu kuomba. Sasa ukiomba, ndiyo michakato inaanza ya kama una sifa au hauna sifa", ameeleza Kafulila.

Adani Group, kampuni inayoongozwa na bilionea Gautam Adani, imekuwa ikiongeza uwepo wake katika ukanda wa Afrika Mashariki, huku Tanzania ikiwa sehemu ya mikakati yao ya kuimarisha miundombinu ya nishati kupitia mradi unaotajwa kuwa na thamani ya takriban dola milioni 900. Tanzania pia iko kwenye mazungumzo na Gridworks Development Partners kuhusu mradi wa dola milioni 300.

Kwa upande wake, Tanzania imeweka kipaumbele katika kuboresha miundombinu ya nishati ili kukidhi mahitaji ya umeme yanayoendelea kuongezeka, hatua inayosaidiwa na miradi kama hii ya ubia. Ushirikiano huu pia ni muhimu kwa kuboresha mfumo wa usafirishaji wa umeme wa juu nchini.View attachment 3116153
Sina imani kabisa na wawekezaji wa kihindi. Mwisho yatakua yaleyale ya IPTL. Wawekezaji kutoka india au uarabuni wanakuja na imani kwamba waafrika ni wajinga tukawapige. Mkakati wao ni kuingia mkataba unasomeka vizuri kisha watahonga vigogo watavuna juu ya kile wenyewe wenye liinchi lao wamewekeza. Hawawekezi kitu chochote cha maana ila kwa mbinu na ubabaishaji wanachuma hadi mkishituka washafanikiwa sana wanakitoa. Mnakumbuka wale wahindi waliletwa na Andrew Chenge wakapewa TRC jinsi walitupiga. Huyo Adani mwenyewe ni tajiri wa kupindukia India na sio kama utajiri wake ni ganha ganha yaani fifty fifty anakowekeza miradi ya uendeshaji bandari na viwanja vya ndege. Kafulila fungua macho sana ama sivyo tutakuja kukulaani.
 
Kuna taarifa nyingi sana huko duniani zinamhusu huyu Adan. Hao waliotoa taarifa zake ni waongo?? Guys , lets be serious. Ebu tuwekeeni maslahi ya nchi mbele kwanza na siyo hii mizuka inayotupanda. Serikali ni watu. Hivyo, ebu tuishauri serikali kwa hekima na siyo kukurupuka. Kafulila ni binadamu kama wengine. Uwezo wake wa kufikiri au kutafuta taarifa unaweza kuwa umekomea hapo. Hiyo ni ishara ya binadamu kwani siyo malaika. Huyu mwekezaji , ni vyema akatizamwa kwa kina.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kampuni mbili kubwa, Adani Group ya India na Gridworks Development Partners LLP ya Uingereza, zimeonesha nia ya kuwekeza katika mradi wa kusafirisha umeme nchini Tanzania kupitia mfumo wa ubia. Mradi huo unalenga kujenga njia za kusafirisha umeme wa juu kwa lengo la kuboresha miundombinu ya nishati nchini Tanzania.

Akizungumza kwa njia ya simu na Jambo TV, David Kafulila, Kamishna wa Ubia wa Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), amefafanua kuwa utaratibu huo unajulikana kama "expression of interests,"ambapo wawekezaji wanaweza kueleza nia yao ya kuwekeza kwenye miradi kwa kushirikiana na serikali.

"Kampuni (Wawekezaji) mbili ambazo zimeomba kufanya mradi wa kusafirisha umeme kwa utaratibu wa ubia, inaitwa expression of interests yaani kwamba inaruhusu mwekezaji kueleza nia yake ya kuwekeza kwenye mradi fulani katika utaratibu wa ubia na serikali" ameeleza Kafulila.

Kafulila ameeleza zaidi kuwa sheria za ubia nchini Tanzania zinaruhusu kampuni kuwasilisha maombi yao kwa hatua za awali, na serikali inaweza kuamua kuitangaza miradi hiyo kwa kampuni zingine kushindana ili kuhakikisha uwazi na ufanisi. Hivi sasa, Adani na Gridworks ndio kampuni mbili zilizowasilisha maombi ya kuwekeza katika mradi huo wa kusafirisha umeme.

Ameongeza kuwa zipo njia nne zinazotumika kuingia kwenye ubia wa umma na binafsi nchini Tanzania. Njia hizo ni pamoja na serikali kutangaza mradi na kuruhusu ushindani (Solicited), mwekezaji kuomba kuandaa mradi (Unsolicited), serikali kutafuta mwekezaji wa moja kwa moja wa haraka hasa baada ya kuwa tayari imeandaa mradi (Direct Negotiation), na ya utaratibu maalum (Special Arrangement). Katika kesi ya Adani na Gridworks, wameomba kuwekeza kupitia njia ya kusudio la mwekezaji (Unsolicited).

Kafulila amesisitiza kuwa maombi yaliyotolewa na Adani na Gridworks ni hatua ya awali, na michakato ya kuchunguza kama kampuni hizo zina sifa stahiki itaendelea. Serikali kupitia TANESCO itazingatia mahitaji ya mradi huo na kuamua kama kutangaza zabuni kwa kampuni zingine au kuendelea na kati ya waombaji wa sasa.

"Adani ameleta kusudio awekeze, ni hatua ya awali ya kueleza kusudio, na siyo Adani peke yake ambayo imeomba iwekeze, sasa baadaye kwa mujibu wa sheria TANESCO sasa inaweza ikaamua kutangaza na kampuni zote ambazo zinahitaji zikashindana kutegemea mahitaji yake kwa wakati huo. Sasa hiyo iliyofanyika ya Adani na Kampuni nyingine ya Uingereza ya Gridworks Development Partners LLP, ni kampuni mbili ambazo zimeomba kuwekeza, na sheria inawaruhusu kuomba. Sasa ukiomba, ndiyo michakato inaanza ya kama una sifa au hauna sifa", ameeleza Kafulila.

Adani Group, kampuni inayoongozwa na bilionea Gautam Adani, imekuwa ikiongeza uwepo wake katika ukanda wa Afrika Mashariki, huku Tanzania ikiwa sehemu ya mikakati yao ya kuimarisha miundombinu ya nishati kupitia mradi unaotajwa kuwa na thamani ya takriban dola milioni 900. Tanzania pia iko kwenye mazungumzo na Gridworks Development Partners kuhusu mradi wa dola milioni 300.

Kwa upande wake, Tanzania imeweka kipaumbele katika kuboresha miundombinu ya nishati ili kukidhi mahitaji ya umeme yanayoendelea kuongezeka, hatua inayosaidiwa na miradi kama hii ya ubia. Ushirikiano huu pia ni muhimu kwa kuboresha mfumo wa usafirishaji wa umeme wa juu nchini.View attachment 3116153
Ubia serikali na kampuni binafsi ndio kwenye serikali fisadi mwekezaji anakula faida kwa ujanja anaofanya. Kwa mfano mishahara na marupurupu, kutoa kandarasi kwa kampuni zake yaani inside trading na kadhalika na public yaani serikali ndio anabakia na madeni na kuambiwa kampuni imepata hasara kila mwaka hakuna gawio huku mwenzake kashakula gawio.
 
Hayo hayawezi kufanyika wala kutokea .hakuna janja janja kwa sasa
 
Mheshimiwa Kafulila alishatoa ufafanuzi sana na kueleza sana juu ya faida na umuhimu wa kufanya miradi kwa mfumo wa ubia.kwa sababu mfumo huu unaipunguzia mzigo wa gharama serikali kwa kukomba pesa zote za walipa kodi.Mfumo huu wa ubia unasaidia kuipunguzia gharama serikali na kuipa uhuru wa kufanya mambo mengine mbalimbali ya kimaendeleo kuliko kama ingetoa pesa zote mabilioni kwa mabilioni na kuweka eneo moja tu.
Sawa kama wapo tayari tuwape economic zone waendeshe. Tuwape chuma cha liganga watengeneze bidhaa za chuma hapa Tanzania kama ni kweli wanatupenda. Umenunua gari halafu unampa mtu swinging aendeshe akuletee mapato tena anaweza kukwambia leo sijapata. Na ukiingia mkataba na anaweza kukunyoosha kwa kigezo cha future profits.
 
WEKA WI-FI ZA T¡G0 ZINA SPEED KUBWAA MNOO!
HUU SIO MDA TENA WA KUWAZA KUISHIWA NA DATA, ROUTER NI BEI NAFUU SANA!

⚫KWENYE BISASHARA YAKO WEKA WI-FI

⚫KWENYE SHULE WEKA WI-FI
⚫KANISANI WEKA WI-FI

⚫KAZINI WEKA WI-FI
⚫KWENYE KAMPUNI WEKA WI-FI

⚫NYUMBANI KWAKO WEWE NA FAMILIA YAKO WEKA WI-FI
⚫CHUONI WEKA WI-FI

⚫UNA SECURITY CAMERA FUNGA WI-FI

⚫SEHEM ZINGINE AMBAZO SIJAZITAJA WEKA WI-FI

TUMIA DATA UNLIMITED, YANI BILA KUWAZA KUA GB ZITAISHA?

NJOO NIKUPE ROUTER ZENYE UWEZO MKUBWA TECNOLOJIA YA 5G SPEED HADI 200mbps, NA UNAWEZA KULIPA KIDOGO KIDOGO !

MKOA WOWOTE ULIPO DELIVERY NI FREEE!!

GHARAMA NI NAFUU, SPEED KUBWAA (pia laini pekeyake bila router nakuwezeshea bando unlimited kwa bei poa)
NICHEKI: 0717700921
 
Ukweli ni kwamba kafulila alienda India kuchukua mgawo wake wa Rushwa kutoka kwa Aidan ili ampe kazi ya kusambaza umeme kiujanja ujanja kupitia ppp
Ameumbuka na Aidani wake
 
Hawezi kurudi tena hapa yeye wala chawa wake, hadi mwezeshaji asafishwe kule US, huku shitholeni hutasikia kitu japo wa Nairobi walichukua hatua
 
Tuanzie hapa
Sie tumefeli wapi hadi tutake ubia. Maana uzalishaji tumefanikiwa , je usambazaji tunahitaji a complete overhaul ya haraka hadi tuhitaji usd 900 mio. Je hatuwezi kwenda kwa awamu na huku tukiendelea kutoa huduma hii public goods. Hawa jamaa wanaweza kuingia kwenye procurement kama wauzaji tu sio waendeshaji. Imagine nguzo , chuma ya liganga na cement za nguzo ipo , nguzo mufindi na transformer zatengenezwa kigamboni
UHI sio tatizo

Chanmaana ni nani anafaa kuwa mbia?
 
UMEME WA PPP TANZANIA KWA TANESCO KULIPA KWA DOLA ZA KIMAREKANI , HATARI MBIA ANAWEZA KUZIMA UMEME

Adani Anapunguza Ugavi wa Nishati kwa Bangladesh kwa Nusu kutokana Bili Zinazodaiwa: Ripoti​

Hadithi na editor@republicworld.com (Dawati la Dijiti)
•3 miezi
1739437791467.png

Dhaka: Kampuni ya India ya Adani Power Jharkhand Limited (APJL), kampuni tanzu inayomilikiwa kabisa na Adani Power, imepunguza nusu ya usambazaji wake wa umeme kwa Bangladesh kwa sababu ya bili ambazo hazijalipwa za dola milioni 846, kulingana na ripoti ya vyombo vya habari vya ndani siku ya Ijumaa..

1739437983326.jpeg
 
Back
Top Bottom