==
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha ubia nchini Tanzania PPPC Bwana David Kafulila akiwa katika mahojiano na kituo maarufu zaidi cha utangazaji cha ITV kwenye kipindi cha DK 45 amesema haya,
Pamoja na mambo mengine mengi Kafulila anasema kama Kuna kitu Rais Samia anaweza kujivunia ni kufanikiwa kutekeleza Miradi yote iliyoachwa na Mtangulizi wake bila kuacha hata mradi mmoja,
Kafulila anasema awamu ya 5 ndio awamu ilianzisha Miradi mikubwa pengine kuliko wakati wowote wa uhai wa Taifa la Tanzania na baada ya Kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya 5 haikudhaniwa kama Miradi hiyo lukuki Rais anayefuata angeweza kuitekeleza Miradi yote hiyo Kwa BOQ zile zile Kwa sababu ya kukosekana Kwa consistency toka awamu moja na awamu nyingine.
Hata hivyo Mkurugenzi Kafulila anasema baada ya Kifo cha Rais awamu ya tano palihitajika Rais mwenye maguvu, Uwezo , maamuzi na utayari zaidi ya ili kwanza kukamilisha Miradi yote iliyoanzisha na Mtangulizi wake lakini pili ni kuanzisha Miradi mingine mipya na huyo mwenye hizo sifa na uwezo huo ni Rais Samia Suluhu Hassan Kwani ni yeye kamaliza Miradi yote ya awamu ya 5 na kaanzisha Miradi mingine mipya ya awamu ya 6.
Msikilize Kafulila kwani kaongea mambo mengi tena Kwa kina.
View attachment 3359513