Wasalaaam, Soma hii Mzumbe Public Lecture kwa makini sana uelewe kwanini serikali zote duniani kwa sasa zinakimbizana na PPP,
Mikopo yote (serikali, sekta binafsi, kaya) imefikia zaidi ya USD trilioni 300, wakati uchumi wa dunia ni takribani USD trilioni 115 — Deni hili ni karibu mara tatu ya uchumi wa dunia.
===
Mkurugenzi wa Kituo cha Ubia nchini Tanzania (PPPC), David Kafulila, akizungumza katika Chuo Kikuu cha Mzumbe, ameeleza kwa kina nafasi ya Public-Private Partnership (PPP) katika kukabiliana na changamoto ya deni la taifa na mahitaji ya ustawi wa wananchi.
Kauli ya Kafulila Mzumbe,
“Tunapozungumza ubia, Ubia, kama nilivyozungumza, ni mkataba wa muda mrefu kati ya kampuni binafsi na serikali kwa ajili ya kutekeleza kile ambacho serikali ilikuwa na wajibu wa kukifanya. Ni wajibu wa serikali kujenga hostel.”
Serikali, kwa maana ya chuo, ikiingia makubaliano na kampuni binafsi kujenga na kuendesha hostel, huo ni ubia. Fedha ambazo chuo au serikali ingetumia kujenga hostel zinaweza kuelekezwa kuboresha vifaa vya maabara, kwa mfano. Fedha ambazo zingetumika kujenga hostel zinaweza pia kuboresha ubora wa walimu wake.
Ni wajibu wa serikali kujenga barabara, lakini kampuni binafsi inaweza kujenga barabara ya kulipia. Tafsiri yake ni kwamba serikali inaokoa fedha ambazo ingewekeza kwenye barabara na kuzielekeza kwenye maeneo ambayo sekta binafsi haina motisha ya kuwekeza.
Ni wajibu wa serikali kujenga miradi ya umeme, kusafirisha na kuzalisha. Ni wajibu wa serikali kujenga madaraja na huduma mbalimbali za msingi kwa wananchi.
Kimsingi, kwa mujibu wa katiba, jukumu la kwanza la serikali ni ustawi wa watu wake. Ndio jukumu la serikali.
Ustawi na Mahitaji
Kwa hiyo, ukiwa kiongozi wa nchi, maana yake unaona jukumu lako la kwanza mbele yako ni ustawi wa watu. Katika kujenga huo ustawi, kuna hesabu ya kile unachokusanya na mahitaji ya ustawi huo.
Duniani kote, na hasa kutokana na mapinduzi ya taarifa, serikali nyingi zimezidiwa na mahitaji ya wananchi na kushindwa kutumia kodi na mikopo pekee kukidhi matarajio hayo. Hii ndiyo sababu uchumi wa dunia leo unaendeshwa kwa mikopo.
Takwimu za Mikopo
Ripoti zinaonyesha kuwa mikopo yote duniani imegawanyika katika makundi matatu:
Mikopo ya serikali.
Mikopo ya makampuni binafsi.
Mikopo ya kaya (household).
“Mimi nakopa kwa ajili ya kufanya, nakopa kwa ajili ya kulipia watoto wangu ada. Nakopa kwa ajili ya kujenga nyumba yangu,” alisema Kafulila.
Ukijumlisha mikopo yote, ni zaidi ya dola za Kimarekani trilioni 300, wakati uchumi wa dunia ukiwa takribani trilioni 115. Kwa picha hiyo, ni wazi kuwa mikopo yote duniani ni karibu mara tatu ya uchumi wa dunia.
Uchambuzi wa Deni
Hii ni mikopo yote ya sekta binafsi, kaya na serikali. Lakini mikopo ya serikali ilifikia takribani trilioni 115 wakati uchumi ulikuwa juu kidogo, Hivyo, mikopo ya serikali zote duniani ilikuwa karibu asilimia 90 ya uchumi wa dunia.
Mantiki nyingine ni kwamba uchumi wa dunia unaendeshwa kwa mikopo (debt financed).
Mikopo ya serikali zote za Afrika ilikuwa takribani asilimia 67 ya uchumi wa bara la Africa. Na mikopo ya Tanzania, ya serikali ya Tanzania, kwa uchumi wake, ikichukuliwa kwa jumla, ilikuwa asilimia 47 ya uchumi wa taifa.
Lakini ukifanya uthamini shaji wa thamani ya mkopo wa Tanzania kwa uchumi (Net Present Value – NPV), ilikuwa asilimia 40.
“Hivyo kama deni la serikali lote ni trilioni 114 na mikopo yote ni asilimia 47 ya uchumi, unaweza kujiuliza kwa nini Wizara ya Fedha inaonyesha deni ni asilimia 42 ya uchumi ni kwa sababu ya kukopa mikopo nafuu,” alihitimisha Kafulila.
Kafulila alisisitiza kuwa PPP ni njia ya kupunguza utegemezi wa mikopo na kodi pekee, huku ikihakikisha miradi ya maendeleo inaendelea kutekelezwa kwa masilahi ya wananchi na sekta binafsi.
Chanzo: yay_tanzania