David Kafulila: Hali ya uchumi wa kati wa Tanzania na rekodi saba za kimataifa zilizowekwa chini ya uongozi wa Rais Magufuli

David Kafulila: Hali ya uchumi wa kati wa Tanzania na rekodi saba za kimataifa zilizowekwa chini ya uongozi wa Rais Magufuli

Hiki 'kitumbili' nilishaki ' ignore kitambo Sana.

Anachokisahau ni kwamba huyo Magufuli hata Iona Tena ikulu baada ya uchaguzi huu.

CCM wakione angalau wakitupie ganda la ndizi kiache kubwabwaja unafki wake!
 
Ni aibu sana ninyi wapinzani kuwa mnakataa ukweli. Kama world economic forum wanamkubali JPL kuwa amekuwa wa kwanza juu ya kuleta uchumi jumuishi alafu unasema eti mtoa mada aliangalia indicator moja.

Kwani wao WEF hawaajui kuwa hadi inclusive economy iwepo kwenye taifa fulani indicators zote zinakuwa zimekamilika!View attachment 1558920
Mbona umeleta heading sio components? Mkuu siku zote the devil lies in the details..... Sasa tuwe wakweli social security ime cover watu wangapi TZ? Tz ina moja ya lowest social security/insurance penetration sub sahara sababu tuna formal sector ndogo mnoo. Lakini miundombinu tumewekeza pesa nyingi so its obvious inazibeba indicator zote maana wale wanapiga average.

Ni kama GDP tu utaambiwa imekua 8% lakini uhalisia unakuta investment na Net exports ziko below 20% afu expenditure ndio ipo juu!! Sema kwenye average itakua 8% bila kujali ni indicator moja imepaa ama vp.

Ningeomba ulete hapa uchambuzi wa component moja moja alafu ndio tufikie hitimisho je inclusivity imeonekana wapi na wapi sio kuleta heading.

UCHUMI NI COMPONENTS SIO AVERAGE!
 
No sijaweka heading tu. Hayo maelezo yote yanajitosheleza kwa nini Tanzania ilikuwa ya kwanza kwenye uchumi shirikishi. Na nilikuwa nataka kupinga kuwa amebase kwenye miundo mbinu tu.
World economic forum wameweka bayana kuwa infrastracture,free education policy,corruption well fighted and perfoming well social security schemes. Na hii imefanya wananchi wote wa Tanzania kunufaika kazi nzuri iliyofanywa na Ccm. Napinga kuwa mtoa mada amejikita kwenye miundo mbinu.
Kuna haja ya kuanza kuhoji juu ya component moja moja wakati una shuhudia kwa majo afya,elimu ,miundo mbinu na vita dhidi ya ufisadi ulivyowasaidia ?
 
Hongera Kafulila uchumi wa kati wa nchi kudumu kwa mwezi mmoja tu , mmevunja rekodi mapimbi wa kutupa , unamdanganya nani?
IMG_20200828_183448.jpg
IMG_20200828_183430.jpg
 
No sijaweka heading tu. Hayo maelezo yote yanajitosheleza kwa nini Tanzania ilikuwa ya kwanza kwenye uchumi shirikishi. Na nilikuwa nataka kupinga kuwa amebase kwenye miundo mbinu tu.
World economic forum wameweka bayana kuwa infrastracture,free education policy,corruption well fighted and perfoming well social security schemes. Na hii imefanya wananchi wote wa Tanzania kunufaika kazi nzuri iliyofanywa na Ccm. Napinga kuwa mtoa mada amejikita kwenye miundo mbinu.
Kuna haja ya kuanza kuhoji juu ya component moja moja wakati una shuhudia kwa majo afya,elimu ,miundo mbinu na vita dhidi ya ufisadi ulivyowasaidia ?
What I mean weka link hapa alafu nikuonyeshe weakness ya hyo taarifa. Mie binafsi ndio shughuli zangu hizo nmeandaa ripoti kadhaa za kiuchumi trust me uchumi ni sensitive sana na ni rahisi kutwist variable yako fulani iende upande wako.

Kafulila mfano kachagua Moody's ila hajaangalia Net IIP ambayo ina rank based one madeni unayodaiwa na unadai. Nikupe mfano US inadaiwa zaidi ya 100% ya GDP yake ila Tz madeni hayajafika hta 60% ya GDP je huoni kwa haraka haraka utasema Tz tunadeni himilivu kuliko US?

ila ukiangalia component wise utagundua US inadeni kubwa zaidi la ndani yaani imejikopesha toka taasisi zake tofauti na Tz ambapo deni kubwa ni nje!!! So utatoa analysis tofauti pia

Furthermore ukitumia NIIP Approach utagundua Us ina deni dogo sababu ukichukua pesa iliyokopa Vs Iliyokopesha zinacross each other inabaki % ndogo mnoo ya deni. So analysis pia itabadilika

Kwa mfano huu tu kwa hoja ya kafulila kuhusu MOODY's jaribu kuelewa kwamba unaweza twist indicator moja ya uchumi ili kuvutia upande wako. Ila taarifa nzuri ya uchumi ni kuangalia implications kwa pande zote bila kubagua zile zinazoonyesha udhaifu.
 
~Na David KAFULILA.
email: davidkafulila0@gmail.com

02 Septemba 2020.

Julai 1, 2020, ni tarehe itakayokumbukwa katika historia ya Tanzania. Ilikuwa tarehe ya kwanza ya utekelezaji wa Bajeti ya mwisho ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Utawala wa Rais JOHN MAGUFULI; na muhimu zaidi, ni siku ambayo Benki ya Dunia ilitambua na kuitangaza Tanzania kama Nchi ya kipato cha kati kabla ya matarajio iliyojiwekea kufikia 2025.

Katika kujadili mafanikio hayo, ningependa kuongelea mambo saba (7) muhimu yaliotekelezwa ndani ya miaka mitano na kuvunja rekodi kimataifa.

Kwanza, tunapaswa kuzingatia kwamba wakati watu wengi walipokuwa wanawasiwasi na kujiuliza kwamba Rais Magufuli anajenga Taifa la namna gani, mnamo Julai 1, 2020, Benki ya Dunia ilijibu Kuwa Rais Magufuli alikuwa anajenga Taifa la kipato cha kati.

Pili, katika uchambuzi wa 2017 wa Bi Christine Legarde alipohojiwa nchini Ethiopia na Jarida la Quartz, alipokuwa Mkurugenzi wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), alipongeza kwa moyo mkunjufu mafanikio yaTanzania yaliyofikiwa waikati huo chini ya uongozi wa Rais Magufuli.
Mbali na Ethiopia, Nigeria na Kenya, aliitaja Tanzania kama Nchi iliyokuwa imeonesha dalili za wazi kuelekea safari ya mapinduzi ya viwanda kama Vietnam.

Tatu, kama ilivyoelezwa katika mkutano wa jukwaa la uchumi wa Dunia 2018, Tanzania ilishika nafasi ya kwanza katika Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa uchumi jumuishi. Rekodi hiyo imedhibitisha kwamba utawala wa Magufuli ni serikali inayowajali masikini

Hata hivyo Tanzania ilitajwa kuwa ni nchi inayoongoza katika mapambano dhidi ya Rushwa kati ya nchi 37 zilizofanyiwa utafiti Barani Afrika mwaka 2019 hii ni kwa mujibu wa Shirika la the Africans Global Options Survey.

Watanzania wametambua jitihada za mafanikio za muda yaliyofikiwa kutoka, kukodisha Ndege kwa dollar za kimarekani 43 million ikifanya kazi kwa miezi 6 tu na miezi 37 ikiwa haifanyika hii ni kwa mujibu wa ripoti Mkaguzi wa hesabu za serikali ya April,2020

Hivi karibuni jukwaa la uchumi wa Dunia liliitangazaSerikali ya Tanzania kushika nafasi ya 28 kati nchi 136 Duniani kwa matumizi Bora ya fedha za Umma. Ikumbukwe kuwa katika jumuia ya Afrika Mashariki naJumuia ya maendeleo ya kusini mwa afrika, Nchi zilikuwa kama ifuatavyo, Botswana nafai 37,Kenya nafasi ya 70 , Uganda nafasi ya 100, Malawi 106, Msumbiji 118. Rekodi hiyo inathibitisha kuwa Rais Magufuli anajenga Serikali yenye nidhamu ya matumizi ya fedha za umma.

Rekodi ya sita inatokana na Utafiti uliofanywa na African Global Opinion Survey 2019 ambayo inaonyesha kwamba imani ya Watanzania kwa Serikali yao imeongezeka sana. Ripoti imesema kwamba 72% walikuwa na imani na Serikali yao katika kupambana na ufisadi, ikilinganishwa na 13% ya ripoti ya 2015. Hii ni moja ya rekodi za mapinduzi makubwa ulimwenguni.

Rekodi ya Saba inatoka kwa Wakala nambari moja wa Ukadiriaji wa Mikopo, MOODYS ambayo inamiliki asilimia 45 ya hisa ya soko la kimataifa, ilikadiria Tanzania kuwa katika kiwango cha uchumi wa B1 katika ripoti yake ya 2017 ambacho ni kiwango cha juu kuliko nchi yoyote katika Afrika Mashariki (ambayo ilipewa B2). Tathmini hii ni ya kwanza nchini Tanzania tangu uhuru.

# Hizi ni rekodi za ulimwengu na zitabaki kuwa kitambulisho cha Rais Magufuli kimataifa, sembuse diplomasia kubwaⁿ aliyotumia kukabili COVID-19 na kuwaacha wengine ulimwenguni wakishangaa inawezekanaje janga la Corona ambalo lilikuwa likitetemesha ulimwengu wote kweli imeshindwa nchini Tanzania.

Msisitizo wangu hapa ni kwamba umiliki wa Magufuli katika urais wa Tanzania unaonyeshwa na mafanikio makubwa yanayostahili rekodi kubwa ya kimataifa. Ikumbukwe, hata hivyo, kwamba aliingia madarakani mnamo 2015 wakati serikali ilikuwa imekata tamaa sana na haiwezi hata kusimamia muswada wa mshahara wa Utumishi wake wa Umma!
Nimesikitika sana,mi nirifikiri unaeleza vitu ambavyo vinamgusa na kuonekana kwa Mtanzania wa kawaida,
Sababu na tafiti ulizozitoa unataka tuziamini kwa sababu tu zimetajwa au kutolewa na wazungu/taasisi za magharibi?
Wakitaja mazuri wapo sahii!ila wakikosoa Kama Human right watch,hawapo sahihi,tukatae tafiti zao!??
Mi nilitegemea uonyeshe idadi ya vijana waliomaliza Elimu ya juu,na wanaoapata ajira zenye salary kuanzia 600K,
Tunataka tuone wamalize 800000,na 700000 wapate ajira.sio hizi porojo unazoleta
 
Prof Muhongo alimuitaje huyu jamaa? hebu tukumbushane!
 
Back
Top Bottom